TRC: Tumepokea maoni ya Afande Sele kuhusu ratiba ya Treni ya SGR kutoka Morogoro

TRC: Tumepokea maoni ya Afande Sele kuhusu ratiba ya Treni ya SGR kutoka Morogoro

TRC, kama vichwa na mabehewa haviwatoshi, mseme tuwanunulie vingine.
Mficha uchi hazai na sisi tunataka shirika lizalishe.
 
Mnasogeza muda ama mnasogeza huduma Kwa jamii??...poor black skin..alafu unakuta Lina kitambi na linakaa ofisini .😔
 
Nimesoma mkuu...

Sisi wapanda treni kila weekend.
Tunapata hasara sana.
Unajua hata hiyo ya 120k Dom Dar Dom ni hovyo tu.
Hakuna Value for money, haswa unapolinganisha services za 31.5k vs 120k
Mbaya zaidi hizo za 120k ndio zina route nyingi zaidi.
Ni za vibopa wenye familia dar
 
Upumbavu tu,mali ni zetu na bado tunaweka mifumo ya kututesa sisi wenyewe.
 
Kwa hiyo treni inayotoka Dodoma saa 11:15 inayosimama hapo Morogoro saa 3 takriban na dakika 50, hiyo ndiyo nauli yake shilingi 50,000 anayoisema Afande Sele.
Sijaelewa
 
Dodoma treni ilikuwa inaondoka saa 11:15 alfajiri, tukaongeza treni ya saa 1:35. Treni hiyo sasa ndiyo inasimama Morogoro saa 3:50. Treni hiyo inachukua nafasi ya ile treni iliyokuwa inaondoka Morogoro saa 3:50.

Treni hiyo ndiyo ambayo nauli yake ilikuwa 13,500. Treni hiyo imesogezwa mbele sasa inaondoka saa 8:15 hapo hapo Morogoro kwa nauli hiyo hiyo 13,500.
Hapa mwanangu panavuruga kishenzi naona km simuelewi anaongea siasa ama nini?
 
Kwa hiyo treni inayotoka Dodoma saa 11:15 inayosimama hapo Morogoro saa 3 takriban na dakika 50, hiyo ndiyo nauli yake shilingi 50,000 anayoisema Afande Sele.
Sijaelewa
Nahisi Afande Sele yupo sahihi ila hawa wakuda wanajaribu tu kujitetea kitu ambacho hakipo maelezo yao yenyewe yanajigongagonga
 
afandesele kaongea mambo mengi bila plan, ukihoji mambo bila plan majibu yake ndo kama hayo yaliyotolewa
Ukiwa unasoma soma mpaka mwisho usiishie katikati na kuanza kuropoka, ficha ujinga wako
Kwa hiyo treni inayotoka Dodoma saa 11:15 inayosimama hapo Morogoro saa 3 takriban na dakika 50, hiyo ndiyo nauli yake shilingi 50,000 anayoisema Afande Sele.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Yani Mwigulu anahujumu sana SGR na akina Abood shenzi kabisa mzee wa mikoromo
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Sahihi kabisa;

Ili zibalance lazima routes mbili zianzie Morogoro - DSM, DSM - Morogoro; lakini ikitokea routes zikiqnzia Dom - Dar, Dar - Dom; ortherwise ni ngumu sana; na hapo bado zikija routes za mwanza na kigoma miaka ya mbeleni.
nakubali, ila hata hii moro - dar ordinary kna muda hata kwenye mfumo yalikua hayajai vizuri, lakini kama imefika stage ukiitaka lazima ubook kabla maana yake demand imeongezeka , hata kuongeza ruti inakua rahisi,
 
Baada ya Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Selemani Msindi "Afande Sele" kutoa maoni yake kuhusu ratiba ya treni ya SGR kutokea Mkoano Morogoro kuelekea Dar es Salaam. ufafanuzi umetolewa na Shirika la Reli Tanzania (SGR).

Alichokisema Afande Sele kipo hapa ~ Afande Sele: TRC mliwaza nini kuondoa ruti ya Elfu 13, 500 Asubui Morogoro-Dar na kuweka ya 50,000 ambayo wananchi wengi hawaimudu?

TAMKO LA TRC...
"Mimi ni Fredy Mwanjala, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Shirika la Reli Tanzania, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Mhandisi Machibya Shiwa, napenda kutoa ufafanuzi wa tuhuma ama taarifa potoshi hizi zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya jamii eti Shirika la Reli Tanzania limeondoa ruti ya shilingi 13,500 kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya hapo kuweka ruti ya shilingi 50,000. Habari hizo ama tuhuma hizo si za ukweli, ufafanuzi uko hivi.

Shirika la Reli Tanzania linapokea maoni, linapokea ushauri na mitazamo katika ubreshaji wa uendeshaji wa treni zake za umeme za SGR. Katika maboresho hayo ya ruti ndefu, kulikuwa kuna ongezeko la ruti kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda Dodoma na zote zinasimama Morogoro.

Dodoma treni ilikuwa inaondoka saa 11:15 alfajiri, tukaongeza treni ya saa 1:35. Treni hiyo sasa ndiyo inasimama Morogoro saa 3:50. Treni hiyo inachukua nafasi ya ile treni iliyokuwa inaondoka Morogoro saa 3:50.

Treni hiyo ndiyo ambayo nauli yake ilikuwa 13,500. Treni hiyo imesogezwa mbele sasa inaondoka saa 8:15 hapo hapo Morogoro kwa nauli hiyo hiyo 13,500.

Kisha, kuna safari ya kurudi kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ambayo inakuwa ni saa 10:30 mpaka saa 10:40 kurudi Morogoro kwa nauli ile ile ya 13,500.

Kwa hiyo treni inayotoka Dodoma saa 11:15 inayosimama hapo Morogoro saa 3 takriban na dakika 50, hiyo ndiyo nauli yake shilingi 50,000 anayoisema Afande Sele. Tunaendelea kupokea maoni, mitazamo, ushauri, hata hayo yaliyozungumzwa na Afande Sele akidai anazungumza kwa niaba ya wananchi wa Morogoro ni maoni, ni mtazamo, ana haki ya kutoa maoni, ana haki ya kuzungumza, ana haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na sisi, kwa kuwa ni shirika sikivu, tunasikia maoni ya Watanzania, tunapokea kwa ajili ya maboresho ya wakati ujao...
 

Attachments

  • 840b190b47e515c1912247fe7c29a668_1791351081324.mp4
    10.7 MB
Back
Top Bottom