TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

Ngedere bundi ile fiksi
Kulikuwa na shida ya umeme
Abiria ndivyo wanavyosema

Ova
Itabidi abiria tuwe tunatembea na testa tuu yaani umeme wa majumbani hauwezi sumbuliwa na ndege ndio uwe ule mkubwa hawa jamaa wametuona viazi sana aisee na sababu zao za kitoto...
 
Lakini ni afadhali kigogo wakijieleza kuliko kukaa kimya tu, au kuropoka tu na mambo mengine ya kisiasa tu.

Kidogo wanaonyesha kama kujutia tukio (contrite); kuliko kujiona vichwa ngumu.
Wawe wakweli sasa.Bundi,popo sijui ngedere wanasingiziwa tu.Insufficient electricity was the cause.Blah blah nyingi mwisho waonekane wehu waliopendeza mavazi tu.
 
Nimejipa wakati nisome michango yote katika mada hii. Huu ndio mchango muhimu kuliko zote nilizo kwisha soma hadi sasa.

Lingekua jambo zuri sana, TRC wakafanya uchunguzi huo wa kina na kuja na taarifa sahihi juu ya sababu iliyoleta htilafu, na wakaainisha watakavyo fanya kuhakikisha tatizo kama hilo linadhibitiwa lisitokee tena; au kama halizuiliki kutafutwe njia za ziada kuhakikisha huduma haiathiriki kwa muda mrefu.
Wao wamekurupuka na kusema ngedere na bundi
 
Kuna machache sana aliyoyaweza lakini mengi zaidi ameboronga vibaya sana.
Tuna angalia dhamiri ...dhamira yake ilikuwa njema kuna tofauti ya mtu kushindwa jambo katika dhamiri njema na mtu mwovu asiye na dhamiri njema kama huyu najisi mvaa mashungi
 
Inawezekana siyo hujuma, labda ni matokeo ya ujinga na uzembe.
Uzembe upi?
Hawakujua ku operat kwa kutumia mafuta kama walivyosema?
Kwani hao operator's waliwapeleka Korea kufanya nini?
 
Afadhali hata walivyomsingizia bundi.Sasa ngedere usiku kwenye nyaya za umeme wapi na wapi?Wanataka turudi darasa la nne tujikumbushe jinsi ngedere anavyotumia masaa yake 24 kila siku?
Hawa watu wangekuwa ni watu makini wangepata fundisho hapa.
Huu uropokaji wa hovyo hovyo tu hautusaidii chochote katika nchi hii.

Sasa ni wazi wamejiropokea tu bila ya kupima ujinga unaoonyeshwa na kuropoka huku. Tabia ya namna hii ndiyo inayotakiwa kupigwa vita isiwepo tena katika utendaji wa ofisi hizi.
 
Hawa watu wangekuwa ni watu makini wangepata fundisho hapa.
Huu uropokaji wa hovyo hovyo tu hautusaidii chochote katika nchi hii.

Sasa ni wazi wamejiropokea tu bila ya kupima ujinga unaoonyeshwa na kuropoka huku. Tabia ya namna hii ndiyo inayotakiwa kupigwa vita isiwepo tena katika utendaji wa ofisi hizi.
Unaweza kukuta hata mropokaji mwenyewe kakurupushwa tu aongee na wanahabari.Anaongea kama kasuku anakula pilipili.
 
hao ngedere na bundi hawakutumwa na wenye mabasi.
Tayari usha ingiza ajenda zenu. Wapewe waarabu, siyo?

Himiza hiyo serikali ya 'Chura Kiziwi' yenyewe waje waarabu kuiendesha!
Hapo tena wala huna haja ya kuuliza, wala usiwape ingia nao ubia tu kama mama Samia alivyofanya bandarini, kiasi amewapa Waarabu mazayuni wa Dubai, kiasi amewapa wahindi, kiasi tumebaki nayo wenyewe. Tushindane sasa tuone nani atamka kidedea.

Nna uhakika ukiwapa Waarabu hapo, nadiriki kusema ndani ya miaka 10 ijayo watatandaza SGR Tanzania nzima.
 
Nna uhakika ukiwapa Waarabu hapo, nadiriki kusema ndani ya miaka 10 ijayo watatandaza SGR Tanzania nzima.
Nimekupa ushauri, mwambie mama aanze na kubinafsisha uendeshaji wa serikali yake; kwa sababu matatizo yote yanatokea huko. Wewe hapa unapindisha na kuweweseka na mambo mengine kabisa yasiyo husika.
 
Kuna sehemu nimeona katika utetezi wanasema, hii kukatika kwa umeme sio Tanzania tu.
Kama vile wanavyojitetea kwamba wizi wa serikalini sio Tanzania tu.
 
Back
Top Bottom