TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

Sasa ngedere wamehusikaje kwenye uharibifu unaosemwa? Na kama wamedanganya kwa ngedere, nina sababu gani ya kuamini kuwa bundi ndo wamesababisha uharibifu?

1. Je waliwakuta bundi wamefia kwenye nyaya za umeme?
2. Wamewakuta ngedere wamefia kwenye nyaya za umeme?
Tusubiri labda watatoa ufafanuzi zaidi pamoja na picha kuonyesha Bundi wamefanya huo uharibifu yaani ndege aharibu waya yenye umeme sidhani akicheza vibaya atafia pale na kudondoka chini na ni mara chache sana..jamii ya ngedere wanajua hatari labda watoto wao..
 
I thought the train has power backup for atleast one hour for emergency situation,

Sasa unasimamaje porini, ikitokea emergency itakuwaje?
 
Kutokana na hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya SGR iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili huku ngedere, bundi wakitajwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), hitilafu hiyo ilitokea jana Julai 30, 2024.

“Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya WI ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system).

Aidhaa, hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) na mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto hiyo na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma ambapo iliwasili mkoani humo saa 7:57 usiku.

Chanzo: mwananchi_official

Kuna muda hadi huwa najiona nimekuwa Mtanzania kwa bahati mbaya hasa kutokana na Upuuzi wanaoufanya Watanzania wenzetu wengine na ambao unatuaibisha mno kwa Watu wa Mataifa mengine. Kwahiyo hawa Bundi na Ngedere muda wote wa Majaribio ya hii Treni ya SGR uliofanyika kwa miezi karibia Mitatu walikuwa hawadandii Nyaya za Umeme ila walikuwa wakisubiria Treni ianze Safari zake rasmi ndiyo waanze Kuchezacheza kwa kurukaruka katika Nyaya za Umeme?

Kuna muda huwa napatwa mno na Jazba na Upumbavu uliotamalaki ila sema tu huwa naamua Kujikaza / Kupuuza.
 
20240731_123452.jpg
 
Back
Top Bottom