TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

Inaonesha hakukuwa na tahadhari yoyote kuwa licha ya reli hiyo kupita kwenye maeneo ya viumbe hao bado tunasubiria matokeo ndiyo tustuke.
Reactivity versus Proactivity...
Reactivity anaongoza
 
View attachment 3057277

TAARIFA KWA UMMA
HITILAFU YA UMEME KATI YA KILOSA NA KIDETE

Dar es Salaam, Tarehe 31 Julai 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linaomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili (2) siku ya tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system). Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku.

Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma, na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku.
Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Jamila Mbarouk
MKUU WA KITENGO CHA UHUSIANO
Kwahiyo Kadogosa ametudanganya au ameleta vichwa ambavyo havina specs zilizotakiwa? Maana kama umeme ungezima, tungetegemea automatic switch on kwenda kwenye nishati nyingine, ili safari iendelee.

Ndio maana inakuwa ngumu sana kuwaamini viongozi wa sasa. Wengi wanasema mambo wasiyomaanisha
 
Kumekucha!
Wameisha anza hujuma zao. Wanafikiri watanzania hawana akili na hawakumbuki kauli zao wanazoziongea mbele ya waandishi wa habari.

Tuliambiwa tren zetu zina mifumo miwili,
1) umeme
2) mafuta
Ukikatika umeme injini inapiga kazi kwa mafuta.

Na walisema haitakuja kutokea umeme ukakosekana kwenye tren hiyo. Ukikosekana maana yake inchi nzima iko gizani.

Sasa tunawauliza kwa nini wasitumie diesel baada ya umeme kukatwa?
Na je wamewalipa fidia abiria kwa hasara waliyoipata?

Hawa wanahujumu mradi kwa makusudi.
Inawezekana siyo hujuma, labda ni matokeo ya ujinga na uzembe.
 
Kuna machache sana aliyoyaweza lakini mengi zaidi ameboronga vibaya sana.
 
Mbaya zaidi Ngedere na bundi ni wanya endelevu yaani wanazaliana hivyo hili tatizo tutaenda nalo mpaka hao viumbe uzao wao uishe
 
Shida ni kwamba wanashidwa kufanya uchunguzi wa kina kujua nini kinatokea, kitu kama hichi kikitokea kama china au India muhusika anashughulikiwa kweli kweli
Nimejipa wakati nisome michango yote katika mada hii. Huu ndio mchango muhimu kuliko zote nilizo kwisha soma hadi sasa.

Lingekua jambo zuri sana, TRC wakafanya uchunguzi huo wa kina na kuja na taarifa sahihi juu ya sababu iliyoleta htilafu, na wakaainisha watakavyo fanya kuhakikisha tatizo kama hilo linadhibitiwa lisitokee tena; au kama halizuiliki kutafutwe njia za ziada kuhakikisha huduma haiathiriki kwa muda mrefu.
 
Mpaka saivi Kadogosa bado yupo ofisini?? Kama ndiyo anatakiwa kujiuzuru haraka sana.
 
Inavyo elekea hata tatizo lililo sababisha ni la kubuni tu, hawana uhakika. Katika hali ya namna hiyo hawawezi kuwa na "suluhisho la kudumu."
Sasa kwa nini wanajichosha kufanya press conferences?Such a waste of time and calories!
 
Back
Top Bottom