Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Hii Treni ilihujumiwa na ccm na sasa wanajifanya kuifufua halafu wanataka wasifiwe hahaa mabingwa wa kutengeneza tatizo halafu kuja kulitatua kwa mbwembwe.
Kweli kabisa, Hakuna chama kingine chochote cha siasa kilishawahi kutawala nchi hii ni CCM pekee, matatizo yote ya nchi hii yamesababishwa na CCM hii hii..hata hii reli ilihujumiwa na CCM, shirika la ndege pia lilihijumiwa na CCM.

Ni kuweka historia sawa!!
 
Kwa watu wenye shughuli zao, it's true hawata panda hiyo treni, watapanda mabasi, lakini walala hoi ambao wao hawana haraka, na huwa wanashindwa kwenda mgombani kutokana na kupaa kwa nauli, treni hii ni mkombozi mkubwa sana kwao.
P
Isitoshe unakata bia mwanzo mwisho hadi Moshi. Kwenye mabasi tulikuwa tunalishwa soda tu kama watoto wadogo.
 
Watu wanasema treni gani inatumia masaa 17,bora wakapande gari za magazeti!
Ni ufinyu wa mawazo kwa watu wanaosema hivyo. Kusafiri na treni na kusafiri na magari ya magazeti ni vitu viwili tofauti. Hata kusafiri na basi ni tofauti na treni. Kwa mfano ukiwa na familia yenye watoto wadogo, wazee au mgonjwa treni ni usafiri mazuri zaidi hasa kama una uwezo kuchukuwa chumba cha kulala. Mabasi yawepo, kuna watakayoyahitaji, ndege ziwepo, kuna abiria wake na treni iwepo nayo ina abiria wake. Yote haya ni kulingana na mahitaji ya msafiri na uwezo wake. Nchi zote zilizoendelea mambo ni namna hiyo yanakwenda.
 
Halafu kumbukumbu zikifutika vichwani utasikia eti Kaskazini tunabaguliwa katika awamu hii.
Kwani Kaskazini kulikuwa na Shida ya Usafiri? Mabasi ya Grade zote yapo, Private za kumwaga, Fuso na Malori ya kumwaga. Ukishindwa Surface Transport ya Road Ndege Daily. Massa 8 from DSM umeshawasili Moshi. Ukitaka pitia Bagamoyo Road yapo, ukitaka pitia Moro Road yapo. Hii shida inayoondolewa na Train ni ya kufika wapi?
 
 
Ye akapande magazeti aachie wengine,
Kuyafufua maendeleo yaliokuwepo kabla si maendeleo ,ni kufufuka kutoka Kuzimu.
Akijenga Standard Gage hapo tutaita maendeleo,na akijenga ya umeme tutaita,revolution,akijenga ya mwendo kasi,tutaita extra infrastructure evolution.
serikali kutimiza wajibu wake si jambo la kusifiwa,kwa kuwa ndo kazi yake.lakini ikiacha ,yafaa ilaumiwe kwa kuacha wajibu wake.
Kwa hili CCM ianajipambanua kivitendo na ubabaishaji uliozoeleka.
 
Awamu ijayo itabidi tuweke standard gauge kuelekea huku kaskazini
Kwenye master plan ya SGR, Kaskazini haipo, ndio maana tunapendekeza Magufuli aongezwe tern ili ule wa nyongera ndipo a plan hiyo SGR ya Kaskazi.
P
 
Sijuhi ni kwa nini napata hisia kuwa hii treni muda si mrefu itasababisha janga la kitaifa!!
Sijuhi tu yaani!!

SPOP PROPHECY OF DOOM.

Acha kuwa mtabiri wa maafa.

Kurejeshwa kwa huruma ya usafiri wa reli ni jambo jema sana. Tumwombe na kumtanguliza Mwenyezi Mungu Aendelee kutupigania ili jambo hili jema lilete nafuu kwa abiria na wasafirishaji mizigo.
 
Je gharama ni Sawa?

Vip kuhusu mzingira ya safari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…