Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Walio haribu reli ni MaCCM na ufisadi wao.
Katiba mpya ni muhimu kusimamia uchumi wetu,bila kujali ni Rais gani anatawala!!
Magufuli akitoka awaachie MaCCM wanauwa miradi yote, kumbuka enzi za Nyerere na Sokoine!!
KAMA MHS MAGUFULI ANASIKIA KATIBA NZURI ITALINDA UCHUMI WA NCHI NA MAENDELEO ANAYOPIGANIA!!
 
Kuna watu hawajui hili. Ni kitu gani kimebadili mwelekeo wa CCM katika awamu hii ya tano tofauti na zilizopita hasa awamu ya tatu na nne? Upigaji? Ni Kwa sababu watu nchi nzima wameanza kujua faida ya upinzani. Mtu akijua hana mpinzani Hana haja ya kuboresha huduma za jamii, atafanya mambo yake kwa sababu ana uhakika atachaguliwa. Hata 2020 jamaa mkimpa kura zote mjiandae na kivumbi cha 2020-2025 hii ya sasa 2015-2020 ilikuwa cha mtoto!
Moja kati ya faida ya upinzani...kama upinzani ingekua haujakomaa Arusha na Moshi hii reli isingelifufuliwa.
Serikali ya ccm inaumiza kichwa wafanye nn ili wapiga kura wabadilishe mwelekeo kwenye chaguzi zijazo..Mwisho wa siku watu wanapata maendeleo.

Action and Reaction are equal and opposite.

NOTE; MOSHI NA ARUSHA ENDELEENI KUCHAGUA UPINZANI MUPATE MAENDELEO.
 
Itapunguza malori ? Yan upakie tani 60 mara mbili kwa wiki upunguze malori ???? Akili zenu hua mnaziweka wapi
Najua inauma sana.....

Haya yanafanyikia kwenu na watu wanashabikia

Watu ambao mnataka wamchukie JPM kwa nguvu zote

Mna hamu hata muwazuie wasipande...ila waaapi



Ulicho miss kwenye statement yangu nimeongelea usafiri wa treni kwa ujumla

Ziko za mizigo pia ndugu, na zitaanza tu


Pole
 
Cost analysis Tanzania tutasubiri sana. Hakuna tunalo lifanya kwa economic benefit (cost effective)... Political eye tu.
Mabehewa 20 × abiria 80 = abiria 1600
Capacity 1600 - waliosafiri 294 = loss (1306 × nauli per person)

Tusikate tamaa tutangulize uzalendo tusafiri kwa reli yetu hata kama ni narrow gauge
 
Wapi Tanzania? Utasubiri sana.
These numbers are so scaring! I hope TRC watafanyia kazi (wanajua wanachofanya!). Tuwape muda.

Muhimu tu tufike mahali tuache kuchanganya kanuni za biashara na siasa.
 
Najua inauma sana.....

Haya yanafanyikia kwenu na watu wanashabikia

Watu ambao mnataka wamchukie JPM kwa nguvu zote

Mna hamu hata muwazuie wasipande...ila waaapi



Ulicho miss kwenye statement yangu nimeongelea usafiri wa treni kwa ujumla

Ziko za mizigo pia ndugu, na zitaanza tu


Pole
Treni ya mizigo labda iishie tanga, prictically kule haifanyi kazi

Biashara kubwa inayofanyika kati ya mikoa ya kaskazn hiyo na huku ni mazao ya chakula...mengi yanayotoka kule yanahitaj kuwepo sokon saa 11 alfajiri, hata magari ya mizigo mengi yanayopita hiyo barabara ni fuso, na ule ukanda kule pia unajitosheleza kwa vitu vingi au kama hakipo wanaingia Kenya hapo..n karibu
 
Kwanini upande gari za magazeti wakati ndege zipo, acha hizo we panda tu treni kieleweke siyo kuficha umaskini wako kwenye gari za magazeti. Treni tutapanda tu hata we mwenyewe usikute ni miongoni mwa hao 290 waliowasili salama huko moshi
 
Unasafiri Siku 2 kutoka Dar hadi Moshi, safari ya Masaa 8???🤣🤣
 
Kwenye master plan ya SGR, Kaskazini haipo, ndio maana tunapendekeza Magufuli aongezwe tern ili ule wa nyongera ndipo a plan hiyo SGR ya Kaskazi.
P
Tanzania hakuna master plan ya kitu chochote. Inategemea anayekula atatokea kanda ipi. Au P unajifanya hujamsikia mheshimiwa akiagiza daraja la Busisi likimbizwe lisije likasimamishwa njiani akiondoka?

Kaskazini tuna figisu sana. Nakuhakikishia SGR itafika muda si mrefu mkuu akiondoka.
 
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
Hahahaaa wachaga bana bila kusahau nyimbo za jimmy reeves na bony emm
 
Watu wanasema treni gani inatumia masaa 17,bora wakapande gari za magazeti!
Hivi behewa moja la treni linauwezo wa kubeba abiria wangapi? Nadhani wakianza kusafirisha sementi, nodno na mabati kwa njia ya treni kutakuw ana nafuu katika bei. Ingawa wenye malori wataanza kulia kwa kukosa mizigo ya kutosha
 
Kuna wapumbavu naona wanatoa pongezi.

Wakati wenzetu wanaumiza vichwa kuja na mode of transportation itayo cover distance ndifu ndani ya muda mchache sisi tunazindua treni za mwaka 1945.
Taarifa iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Kamwele pamoja Shirika la Reli Tanzania ni kwamba abiria walikuwa 700 na treni ilitumia muda huo kwa sababu za kiusalam maana njia ilikuwa haijatumika miaka mingi pia walichukua tahadhali ya mvua. Lakini wakishajiridhisha na usalama wa njia treni itaongeza mwendokosai na mabewa yataongezwa. Pia treni itafika hadi Arusha badala ya kuishia Moshi.
 
Hivi behewa moja la treni linauwezo wa kubeba abiria wangapi? Nadhani wakianza kusafirisha sementi, nodno na mabati kwa njia ya treni kutakuw ana nafuu katika bei. Ingawa wenye malori wataanza kulia kwa kukosa mizigo ya kutosha
Mzigo ndio ulianza kabla ya abiria mkuu
 
Back
Top Bottom