DOKEZO Treni ya SGR ya Dar - Dodoma imesimama Morogoro kwa Saa Mbili, kisha imezima tena kabla ya kufika Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi ni mmoja wa Wasafiri wa Treni ya SGR, nilikata tiketi ya kuondoka asubuhi ya Saa 12:00 leo Januari 8, 2025 lakini ulipofika muda huo safari ikasogezwa mbele kwa nusu saa.

Safari yangu ni kuelekea Dodoma, matarajia ya kuwasili yalikuwa Saa 3:30 asubuhi baada ya hapo ilikuwa nielekee kwenye kikao sehemu fulani ambacho kilipangwa kuanza Saan ne kamili asubuhi.

Safari ilianza vizuri tu na kwa mwendo wa kasi, ilipofika maeneo fulani ambayo siyakumbuki kasi ikaanza kupungua.

Tulipofika Morogoro tukasimama hapo muda mrefu, hadi muda huu saa tano bado tupo Morogoro na hatujui nini kinaendelea.

Safari iliyotarajiwa kufikia tamati saa tatu na nusu, hadi sasa nis aa tano bado tupo Morogoro.

===============

UPDATES...
IMESIMAMA TENA KABLA YA KUFIKA DODOMA

Ilipofika Saa tano na dakika 40 flani hivi Treni ikawashwa tukaendelea na safari, muda wa saa saba na nusu Mchana kabla ya kufika Dodoma, mzigo umezima tena, hatujajua hapa ni wapi ila ndio tunasikilizia kujua nini kinaendelea.

Abiria wote tumeambiwa tushuke kwenye Treni, hatujui nini kinachoendelea.

Imagine niliamka saa tisa ili niwahi Treni ya Saa kumi na mbili na saa tatu na nusu niwe nimefika, mpaka sasa saa saba na nusu mchana hatujafika Dodoma, si bora ningepanda basi nijue moja.

TUNASHUKA, TUNAPANDISHWA KWENYE MABASI
Abiria wote baada ya kuambiwa tushuke, tumeambiwa kuna mabasi ambayo yanakuja kutuchukua hapa tulipo kutupeleka Dodoma Mjini kwa kuwa inaonekana kuna kama Kilometa zaidi ya 20 kabla ya kufika Dodoma.
 
Attachments

  • IMG-20250108-WA0022.jpg
    IMG-20250108-WA0022.jpg
    81.3 KB · Views: 3
  • IMG-20250108-WA0023.jpg
    IMG-20250108-WA0023.jpg
    80.8 KB · Views: 2
  • IMG-20250108-WA0021.jpg
    IMG-20250108-WA0021.jpg
    78.8 KB · Views: 3
Inaonekana kuna kipande njia iba tatizo.wanawafikisha abiria hadi hapo halafu wanapanda bus kufika Dodoma. Wa Dodoma wanafikishwa hio sehemu kwa bus halafu wanapanda treni kuelekea Dar.
Tusubiri taarifa ya TRC.
Mmmh kuna faida inapatikana hapo kweli??
 
Mimi ni mmoja wa Wasafiri wa Treni ya SGR, nilikata tiketi ya kuondoka asubuhi ya Saa 12:00 leo Januari 8, 2025 lakini ulipofika muda huo safari ikasogezwa mbele kwa nusu saa.

Safari yangu ni kuelekea Dodoma, matarajia ya kuwasili yalikuwa Saa 3:30 asubuhi baada ya hapo ilikuwa nielekee kwenye kikao sehemu fulani ambacho kilipangwa kuanza Saan ne kamili asubuhi.

Safari ilianza vizuri tu na kwa mwendo wa kasi, ilipofika maeneo fulani ambayo siyakumbuki kasi ikaanza kupungua.

Tulipofika Morogoro tukasimama hapo muda mrefu, hadi muda huu saa tano bado tupo Morogoro na hatujui nini kinaendelea.

Safari iliyotarajiwa kufikia tamati saa tatu na nusu, hadi sasa nis aa tano bado tupo Morogoro.

===============

UPDATES...
IMESIMAMA TENA KABLA YA KUFIKA DODOMA

Ilipofika Saa tano na dakika 40 flani hivi Treni ikawashwa tukaendelea na safari, muda wa saa saba na nusu Mchana kabla ya kufika Dodoma, mzigo umezima tena, hatujajua hapa ni wapi ila ndio tunasikilizia kujua nini kinaendelea.

Abiria wote tumeambiwa tushuke kwenye Treni, hatujui nini kinachoendelea.

Imagine niliamka saa tisa ili niwahi Treni ya Saa kumi na mbili na saa tatu na nusu niwe nimefika, mpaka sasa saa saba na nusu mchana hatujafika Dodoma, si bora ningepanda basi nijue moja.

TUNASHUKA, TUNAPANDISHWA KWENYE MABASI
Abiria wote baada ya kuambiwa tushuke, tumeambiwa kuna mabasi ambayo yanakuja kutuchukua hapa tulipo kutupeleka Dodoma Mjini kwa kuwa inaonekana kuna kama Kilometa zaidi ya 20 kabla ya kufika Dodoma.
Hizo ni changamoto ndogo ndogo zitaisha tu.
 
Jana pia ile iliyoondoka saa 11:15 jioni, ilisimama Kilosa kuanzia 12: 45 jioni tukaondoka saa 3:00 usiku, DSM tumeingia 5:00 usiku!

Nadhani kuna shida za kiufundi, lakini pia dhihaka za Wabongo kwa founder! Akiwemo Kaflag, JPM alitumia muda mwingi kufikiria maendeleo ya TZ halafu mna mtweza! Acheni dhihaka, la mambo yake/ miradi itakuwa na kisirani!!!
 
Back
Top Bottom