DOKEZO Treni ya SGR ya Dar - Dodoma imesimama Morogoro kwa Saa Mbili, kisha imezima tena kabla ya kufika Dodoma

DOKEZO Treni ya SGR ya Dar - Dodoma imesimama Morogoro kwa Saa Mbili, kisha imezima tena kabla ya kufika Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
TUNASHUKA, TUNAPANDISHWA KWENYE MABASI
Abiria wote baada ya kuambiwa tushuke, tumeambiwa kuna mabasi ambayo yanakuja kutuchukua hapa tulipo kutupeleka Dodoma Mjini kwa kuwa inaonekana kuna kama Kilometa zaidi ya 20 kabla ya kufika Dodoma.
January ngumu hii, hayo mabasi yametoka wapi? sio kwamba ni baishara ya mtu kweli? NI abood au Shabiby?
 
Naweza kutoa hela kwa kitu kinachoshibisha, mule bites bei ghali halafu ukila tumboni upepo mtupu
Sasa kwani vitumbua unashiba kweli...
Wee kula wali ndondo nyumbani ukiingi kwenye treni dar to dodoma mdomo mkavu tuu hapana bwana u agonga ghahawa kidogo
 
Huyu mkurugenzi wa Mkuu kama angekuwepo mwenda zake hichi kibarua angekuwa ameshakinawa zamani! Ila sijui anamchukuliaje Mama? Maana kila siku changamoto haziishi kwenye SGR! Hii ni tafsiri kamili kwamba jamaa kazi imeshamshida kilichobaki ni kuendelea kuliabisha taifa tuu. Majirani zetu Kenya Wana SGR la Hovyo lkn hawana changamoto za kijinga kama Sisi! Laiti mwenda zake angekuwepo huyu Kadogosa angemla bila kunawa!
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ni matatizo ya kiufundi hata wao hawajatarajia mbona siku nyingine wanaenda sawa jitahidi kuwa mvumilivu kama mnaona tren halina uhakika pandeni mabasi mbona miaka iliyopita mlikuwa mnapanda mabasi
Mkuu hiyo train ni Used siyo mpya ukiona vifaa used vinakuja Nchini uko vinapotoka vinakua vimeshapitwa na muda, ni sawa ununue Nokia Lumia used.
 
Back
Top Bottom