Treni ya Umeme yatumia dakika 114 Dar hadi Morogoro, Wananchi 600 wasafiri

Leo bibi tozo alitoa offer kwa abiria mkuu.
 
Dar - Moro kwa siku ni route ngapi?
 
Nani amekabidhiwa ulinzi wa vyooni, maana huko ndiko treni itaanza kuharibikia
 
Walete vichwa vipya na vya kisasa vya treni , huo muda wa safari masaa mawili Dar-Moro ni mrefu sana, Dar-Moro inapaswa iwe saa moja tu kwa usafiri wa SGR, Dar-Dom iwe 3 hours na Dar - Mwanza 6 hours , otherwise bado tutapanda mabasi na treni itaendeshwa kwa hasara na kufa!!

Huo muda wa leo wa safari tofauti ni ndogo na usafiri wa mabasi, binafsi sijaona maajabu ya SGR
 
Picha Tafadhali
 
Kwa bus Dar Moro ni masaa 4,
Kwa treni ni mawili,

Bado huo muda ni mdogo ? Tuache nongea wakuu
 
Tusubiri waseme wanaendesha kwa hasara.
Mkuu 'Mad',

Mie hupenda sana watu wa aina yako. Wanatoa ufafanuzi papo kwa papo bila ya mizunguko.
Huko serikalini tungekuwa na watu wenye kufanya hivi, nchi yetu isingekuwa na matatizo mengi tuliyo nayo sasa.

Hapa JF, mfano wako ni nadra sana.
Nikupe Hongera za Dhati kabisa.
Sasa ni hivi:
Kule Bandarini Dar es Salaam, unadhani hapakuwepo na watu wenye vichwa timamu kama hiki chako?

Unafikiri U-DART hakuna wanaojua udadavuzi kama wako?

Nashukuru umehitimisha kwa kuweka huo mstari wa mwisho nilio unyanyua na kuubandika hapo juu.

Hili ni kama tamaduni ndani ya nchi hii.

Nionyeshe mahali popote ambapo imekuwa ni tofauti: kwenye Ndege; kwenye kilimo chetu; kwenye ufugaji wa kuku; kwenye viwanda vyetu, Feri Kigamboni, n.k., n.k..

Ninachoweza kukubashilia kuhusu hii SGR; haitakuwa tofauti sana na ile reli ya mjerumani/Mwingereza, au ile ya mchina.
Tutawatafuta wawekezaji toka nje, kama wale wa India wakati ule, lakini haitafua dafu.

Sitaki kuwa wakala wa shetani kwa nchi yangu. Kwa hiyo nasema hivi..., uozo wote huu tutauacha nyuma hapo tutakapofanikiwa kuwapata viongozi wanao jali maslahi ya nchi hii, siyo hawa akina Samia.
 
Vision ya Magufuli kweli tunahitaji rais mwingine mwenye vision ya Hali ya juu kuhusu Nchi.
Samia si alikuwa hapo pembezoni mwake muda wote, imekuwaje tukaishia huku tulipo sasa chini ya msaidizi wake?

Siwezi kamwe kubeza "Dira" aliyokuwa nayo Magufuli juu ya taifa hili (bila ya kufikiria hayo mengineyo ambayo hayakuwa mazuri).

Sasa tuna mwenye dira ambayo ni kinyume kabisa na huyo aliyekuwa akimsaidia kutimiza dira ya mwanzo.
 
Dah inauma mzee, sana sio kidogo. Ngoja tusiwajudge mapema tusubiri mwakani mwezi wa 6.
 
Dah inauma mzee, sana sio kidogo. Ngoja tusiwajudge mapema tusubiri mwakani mwezi wa 6.
Bila 'overhaul' ya chanzo cha uozo tulio nao kila mahali, ni garantii, hiyo SGR haitakuwa tofauti na sehemu zingine.

EEeeHEeeee!,"mwakani mwezi wa sita". Hata sijui kama hiyo treni itakuwa imekwisha fika Dodoma!

Kama ni kwa kipande hicho hicho cha Dar - Moro; matatizo yao yatakuwa ni idadi ya wasafiri. Hakuna idadi ya wasafiri kujaza treni nne kwa siku hapo; na hata mbili nina mashaka sana.
Kwa hiyo hesabu zako zitasomeka tofauti kidogo.

Usisahau wenye mabasi bado wapo.
 
Hakuna cha kuwapongeza, tuliwaajili wafanye hayo. chawa mkubwa we πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
Pili, masaa mawili km 192 km ni muda mwingi sana. Ulaya ni 300km/hr. Ilibidi iwe less tha an hour. Bado waliiba hela wakaleta mikweche.,
Ndonaposhangaa moro hapo tu masaa 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…