Treni yaleta ‘kilio’ usafiri wa mabasi Dar - Moshi

Treni yaleta ‘kilio’ usafiri wa mabasi Dar - Moshi

Yaani treni inaenda Moshi mara 3 kwa week, trip moja inabeba watu 150 kwa hiyo hadi mwezi uishe itakuwa imebebeba abiria kama 2000 tu ndiyo imeua biashara ya mabasi msimu wa Christmas?

Get outta here.
Hili la treni kubeba abiria 150 kwa trip moja umelitoa wapi mkuu? Nadhani umeshindwa hata kufikirisha ubongo wako. Treni ina mabehewa mangapi na kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria wangapi?

Hii uloyoleta ni uzandiki tu na haukubaliki kwa maendeleo ya taifa.
 
Besta Mlagila,

Sasa naona wafanyabiasha wa mabasi wameanza kukubali majibu ya train. Huko bank marejesho yataanza kusua sua,wapigadebe tafuteni shughuli ya kufanya, hotel zilizoko barabarani huko Korogwe sasa vyakula vitakuwa vipororo.na bado SGR ikifika Morogoro kilio kitaongezeka kwa wamiliki wa mabasi
hivi kwani wauzaji wa vyakula pale korogwe hawalipagi kodi mkuu
 
Labda mimi ndio sielewi hapa
Usafiri bado sana huko hata kama wataweka train tatu naona bado mabasi yatapata wasafiri tu
Train moja tu tena safari moja wanalalamika
Hapa nilipo watu ni 60m na usafiri wa train upo wa chini ya ardhi na upo wa juu na ni nyingi sana
Lakini pia mabasi yapo ya nje ya mji na yote yanajaa full
Katika usafiri bado sana na wasafiri ni wengi bado


Sent from my iPhone using Tapatalk
Nenda China kuna train kila route na mabasi yapo yanajaa
 
Nakubaliana na wewe kabisa.Hizo treni ni hatua ya maendeleo lakini haziwezi kuuwa biashara ya mabasi kwa sababu kila usafiri una sifa na kasoro zake na abiria wana sababu tofauti za kusafiri.Wengine ni wafanyabiashara wanapenda walale kwenye treni asubuhi wafike waendako na wengine ni wagonjwa au wanafunzi wanataka asubuhi mapema wawe wa mwanzo kufika sehemu husika sio saa mbili linapofika treni hata kuoga bado.
Tukiendelea na sababu za kusafiri,wengine ni watalii wanapenda wasafiri na kufaidi mandhari ya mazingira wanamopita ili kujifunza hili na lile.Kwa upande wangu huku niliko usafiri wa treni una nguvu sana na treni zimeunganishwa na miji yote ya nchi lakini pia mabasi ni mengi sana.Vituo vingi vya treni vinapendeza na vimepangiliwa kuliko hata uwanja wetu wa JK uliopo Dar es salaam.Treni zinaingia na kuondoka takriba kila baada ya robo saa sio usiku usiku au jioni jioni .Zaidi ni njia za mabasi hakuna kupishana mpaka unafika unakokwenda.Sehemu zinapokutana barabara iwe ni ya treni au mabasi basi moja inapita juu na nyengine chini yake.Katika hali kama hiyo mabasi yanjaa na matreni pia.

Kweli kabisa Mkuu
Tunahitaji mipangilio mizuri na utaratibu mzuri
Tatizo viongozi wanapokuja nchi zilizoendelea wao wanalala tu na kula bata na kununua suits tu
Wanayaona yote haya na wengi wamesoma Ulaya na kuona miundombinu yao ila hawana mikakati kabisa ya kuiga


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
huo ni mzuka tu! mikoa ya Njombe,Mbeya na morogoro ni watumiaji wakubwa wa Treni ya Tazara tena ukiwa ndani ya Makuba Express ni nzuri kuliko Hiyo ya Moshi-Dar au Reli ya kati.Pia Tazara ina utulivu kwa kua Reli yake ni standard kuliko hiyo ya Moshi Dar lakini miaka yote hii Imeshindwa kuyapiku mabasi sababu kuu ni kama mbili au tatu hivi kama ifuatavy.
1. usafiri wa treni Tanzania unasafari chache sana kwa wiki nje na matarajio ya abiria hususani wafanyabiashara ambao wanatamani kutembea twenty four hours yaani atoke NjOMBE/MBAYA aende DSM afanye shughuli zake siku ya pili arudi nje ya usafiri wa mabasi hakuna huo mfumo kwenye Treni sababu ni uduni wa hudumu na uwekezaji.
2. usafiri wa treni Tanzania Unagharama pengine tofauti na nchi nyingine.Ikifika Disemba ndio usiseme kwa abiria anayeshukia makambako analipa zaidi ya 30000 wakati kwenye basi nako amabapo anondoka asubuhi na kufika jioni nauli 30000 au chini tofauti na treni amabpo atatoka IJUMAA saa tisa na dakika 55 dasm na kuingia makambako Jumamosi alfajiri.
3. usafiri wa treni Tanzania bado hauja wa uhakika ndio na hauna mbadala kama kwenye mabasi.

Hivyo MAONI yangu usafiri wa mabasi hauwezi athiriwa na usafiri wa treni ni watu mia nne ndio wamerudi na treni Juzi tujiulize ni watu wangapi wanasafiri kwa siku toka Arusha,Kilimanjaro,Tanga kuja DSM.
Kurejea kwa usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam na Moshi baada ya kupita miaka 25, kumetingisha usafiri wa mabasi kwenda mikoa ya kaskazini kutokana na idadi ya abiria kudaiwa kupungua.

Kwa kawaida kila mwishoni mwa mwaka huwa kuna mahitaji makubwa ya usafiri wa abiria wa kuelekea mikoa ya kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro kutokana na watu wengi wenye asili ya huko kwenda kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya wakitokea sehemu mbalimbali nchini.

Wakati wadau wa usafiri wa mabasi na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) wakikiri abiria kupungua tangu treni ilipoanza kutoa huduma Ijumaa iliyopita, uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) umeongeza safari za treni kutoka mbili kwa wiki hadi tatu kutokana na wingi wa abiria.

Treni hiyo ilianza kutoa huduma Ijumaa iliyopita ikiwa na mabehewa nane (saba ya abiria) kwa kuondoka Dar es Salaam saa 10 jioni na kuwasili Moshi, Jumamosi iliyopita saa 5 asubuhi na iliondoka siku hiyohiyo mjini Moshi saa 10 jioni kurejea Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu hali ya usafiri wa mabasi kwenda mikoa ya kaskazini kwa sasa katibu wa Taboa, Enea Mrutu alisema “usafiri wa treni umetukata koo kwa kweli abiria hakuna kama siyo mwezi Desemba? Yaani nyakati kama hizi unakuta mabasi ya kwenda Arusha na Kilimanjaro mchana? Ajabu miaka iliyopita huwezi kukuta jambo hili.”

Awali, TRC ilieleza kuwa treni itakuwa inatoka Dar es Salaam Ijumaa na Jumanne na Moshi-Dar es Salaam kila Jumatano na Jumamosi. Ratiba hiyo ilidumu kwa simu mbili tu kwani kuanzia Jumatatu wiki hii, safari zimeongezwa hadi tatu kwa wiki.

Siku ya kwanza treni hiyo iliondoka Dar es Salaam ikiwa na abiria 263 wakati 24 walipandia njiani. Ilitoka Moshi kwenda Dar es Salaam ikiwa na abiria 241.

Idadi hiyo ya abiria wa treni kwa safari moja ni takribani mabasi sita ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 35 hadi 58. Treni hiyo ambayo imeongezwa mabehewa ya abiria kutoka saba hadi nane kuanzia Jumatatu iliyopita, ina madaraja matatu.

Behewa la daraja la tatu lina uwezo wa kupakia abiria 80 waliokaa, daraja la pili kukaa abiria 60 na daraja la pili kulala abiria 36 huku nauli ikiwa Sh16,500 (daraja la tatu), Sh 23,500 (daraja la pili kukaa) na Sh39,100 daraja la pili kulala. “Hali ya usafiri wa mabasi imekuwa ngumu, treni imetupunguzia abiria, ukweli ndio huo.

Mwaka jana mwezi Desemba mchana huwezi kukuta basi la kwenda Moshi au Arusha, ila sasa yapo,” alisema Mohammed Papaa, wakala wa mabasi kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo. “Kulikuwa na tabia ya kupandisha nauli za mabasi Desemba, lakini sasa abiria hawaonekani wamekimbilia kwenye treni unapandishaje?” alieleza Papaa.

Wakala mwingine kituoni hapo, Mathias Mrema alitahadharisha hali hiyo ikiendelea, huenda baadhi ya matajiri wakabadilisha biashara na kuhamia katika shughuli nyingine kwa kuwa hawatapenda kuona wakipata hasara. “Sasa hivi abiria unawaona kuanzia saa moja asubuhi tu, baada ya hapa hakuna kitu,” alisema.

Aisha Miraj, mjasiriamali katika kituo cha Ubungo alisema tangu kuanza kwa treni hiyo abiria, wamepungua. “Biashara zetu haziendi vizuri kwa kuwa abiria wamepungua,” alisema Miraj.

Mjumbe wa Taboa, Mustapha Mwalongo alisema licha ya abiria kupungua, uwepo wa usafiri wa treni umewapa unafuu kwa kuwa miaka iliyopita kipindi kama hiki walikuwa wakitafuta mabasi kwa ajili ya kupunguza abiria. “Maendeleo yoyote hayakosi changamoto.

Haya ni maendeleo kwa serikali, lakini ni changamoto kwa wadau wa usafiri wa mabasi kwa sababu abiria wamepungua,” alieleza. Mmoja wa abiria aliyekuwa akielekea Arusha, Said Ally alisema, “Treni imesaidia kupunguza changamoto ya usafiri hapa Ubungo hasa kipindi cha mwisho wa mwaka.

Sasa hivi unachagua usafiri na treni au basi.” Abiria wa treni, Tongeni Mzava alisema, “leo (jana) nipo Dar es Salaam kufanya biashara zangu naondoka jioni na usiku nitalala kwenye treni na kufika Moshi asubuhi na kuendelea na biashara zangu.

Katika treni uko huru zaidi, unakwenda maliwatoni, chakula unapata kwa wakati, unalala na kuamka muda unaopenda, ni usafiri mzuri.” Maysara Mfinanga alisema, “huwa nasafiri kwa wasiwasi na basi, kwanza mwendo kasi lakini kwenye treni una uhakika utafika.

Kwenye treni unaweza kulala, kukaa kama mimi hakuna shida kabisa.” Naye Flora Akwilapo alisema, “siku za nyuma nilikuwa nasafiri na mabasi ila ilikuwa usumbufu unakaa saa nane kwenye basi mgongo unauma ila katika treni hali ni nzuri zaidi.” Akizungumza na Mwananchi, mkuu wa kitengo cha habari na uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alisema wamelazimika kuongeza safari tatu kutoka mbili kutokana na wingi wa abiria.

“Kutokana na mahitaji ya abiria kuanzia Jumatatu ijayo tumeongeza safari, itakuwa inaondoka Dar es Salaam Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na kuondoka Moshi kuja Dar es Salaam kila Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.” “Mahitaji ya abiria yamekuwa makubwa kwa hiyo tumeongeza siku za kusafiri,” alisema na kueleza pia wameongeza mabehewa ya abiria kutoka saba hadi nane.

Hata hivyo, jana asubuhi zilienea taarifa mitandaoni zikidai kuwa treni hiyo imejaa hadi Desemba 27, kitu ambacho kimekanushwa na Mbarouk. Alisema, “Sisi huwa tunakatisha tiketi siku tatu kabla ya safari, hivyo kusema kuwa nafasi zimejaa hadi Desemba 27 ni uongo si taarifa za kweli na wasafiri wapuuze habari hizo. Ila ninachoweza kukuthibitishia ni kuwa abiria wanaongezeka kwa kasi kila siku ya safari.”
 
mimi ni mfuasi wa chama pinzani lakin katika sala la treni namuunga mkono raisi kwa asilimia zote
treni hii imegusa maisha ya watu wa hali ya chini i wish ingekuwa inafanya safari kila siku ya wiki
 
huo ni mzuka tu! mikoa ya Njombe,Mbeya na morogoro ni watumiaji wakubwa wa Treni ya Tazara tena ukiwa ndani ya Makuba Express ni nzuri kuliko Hiyo ya Moshi-Dar au Reli ya kati.Pia Tazara ina utulivu kwa kua Reli yake ni standard kuliko hiyo ya Moshi Dar lakini miaka yote hii Imeshindwa kuyapiku mabasi sababu kuu ni kama mbili au tatu hivi kama ifuatavy.
1. usafiri wa treni Tanzania unasafari chache sana kwa wiki nje na matarajio ya abiria hususani wafanyabiashara ambao wanatamani kutembea twenty four hours yaani atoke NjOMBE/MBAYA aende DSM afanye shughuli zake siku ya pili arudi nje ya usafiri wa mabasi hakuna huo mfumo kwenye Treni sababu ni uduni wa hudumu na uwekezaji.
2. usafiri wa treni Tanzania Unagharama pengine tofauti na nchi nyingine.Ikifika Disemba ndio usiseme kwa abiria anayeshukia makambako analipa zaidi ya 30000 wakati kwenye basi nako amabapo anondoka asubuhi na kufika jioni nauli 30000 au chini tofauti na treni amabpo atatoka IJUMAA saa tisa na dakika 55 dasm na kuingia makambako Jumamosi alfajiri.
3. usafiri wa treni Tanzania bado hauja wa uhakika ndio na hauna mbadala kama kwenye mabasi.

Hivyo MAONI yangu usafiri wa mabasi hauwezi athiriwa na usafiri wa treni ni watu mia nne ndio wamerudi na treni Juzi tujiulize ni watu wangapi wanasafiri kwa siku toka Arusha,Kilimanjaro,Tanga kuja DSM.


Uchambuzi mzuri lakini ukisema treni haitaathiri usafiri wa mabasi sio sawa. Itaathiri ila sio kwa kiwango kikubwa. Kumbuka hata iwe abiria 10 au 20, tayari wameshaanza kugawana tofauti na awali hao wote walikua wanalazimika kutumia usafiri wa mabasi.

Nnaowahurumia zaidi ni wale wenye mabasi ya Dar Moro pindi reli ya SGR ikikamilika, kwanza itakua na mwendo na ya kisasa.

Kingine usumbufu wa maaskari wa usalama barabarani unafanya mabasi yatembee mwendo mdogo sana na kusababisha abiria kuchelewa zaidi.

Wengi wanaona bora wapoteze muda wa usiku kwenye treni ili siku inayofuata waendelee na kazi zao, ikumbukwe ajali za treni zipo lakini zinatokea mara chache sana.

Ule uhuru wa kuamua kulala na kupatikana kwa huduma muhimu kama chakula na vyoo napo kunaleta hamasa kwa wasafiri.

Usafiri wa treni kwa namba moja ama nyingine unaathiri wamiliki wa mabasi.

Nnachojiuliza baada ya kipindi cha krismas watapunguza idadi ya safari na mabehewa?
 
Acha mabasi yafe kabisa,maana walikuwa wajinga na wapuuzi mwisho wa mwaka wanaongeza nauli kitoto toto kabisa,acha walie kilio cha Paka mwizi
 
Tumetoka mbali Dar-Moshi 1974 mnaondoka dar saa tatu asubuhi mnafika moshi kesho yake saa 3 asubuhi.
Sasa mnaondoka jioni mnafika asubuhi
Screenshot_2019-12-13-12-35-23-1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NIKOOO MOSHII HALI N TETE WAPENDWA MABASI YANAENDA DAR KWA SABABU TU YANATAKIWA KWENDA

MABASI HATA NUSU AYAJAI BEI N ZAKUTUPA KURUDI DAR HADI 18000 LWENDA MPAKA 22000 WACHA TUNYOOOKE MUDA WA KUINGIA KANNAN YA MAGUFULI NDIOO HUU

MLIFIKIRI YULE DOGO ALIUZA MALORI 300+ ALIKUWA FALA NA MABASI AKAISHIA KUUZA KABISA ATAKI SHIDA
 
Kiukweli mlikuwa wanyanyasaji sana kwa abiria wa kanda hiyo... yani kipindi hiki mlikuwa mnaringa kupita maelezo... MUOSHA HUOSHWA...dawa ya moto ni maji 😂😂😂
 
Back
Top Bottom