True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Shusha vitu nzeheee.
 
...67
Ghafla lilitimka vumbi zito sana kusini mwa kilinge kile cha wale watu, wote waligeka kutazama kule, wengine niliona wakisogea pembeni ili kuachia njia ya kupita hicho kitu kinachokuja.
Lilionekana lijifisi kubwa kuliko wote waliokuwa pale, alifika na kuuzunguka moto ule kwa mbwembwe na madoido, kisha akasimama ambapo sasa vumbi lilitulia,
Sikuamini alipoonekana jimama lililoshiba na kujazia mwili (kibonge) likishuka hali limevaa kama wale wachawi wengine wa kike kufunika nyuchi na matiti pekee huku wanaume wakiwa wamefunika nyuchi pekee na kubaki vifua wazi.
Alikuwa amebeba mtoto wa umri kati ya miaka 3 na 4.
Wale wengine walipiga kelele za shangwe na wengine wanaume kupiga mbinja kwa furaha.
Masufuria mengi na makubwa yenye masizi meusi kwa nje yalijitokeza ghafla pale karibu na moto.
Wakati huu nilikuwa natetemeka kwa uwoga na baridi kali la usiku lakini nilijikaza mpaka mwisho.
Twidegeleke lolo bhadugu bhane (sasa tusikilizane ndugu zangu).
Nisauti aliyoitoa yunge na watu wote walikaa kimya.
 
Yunge ni motoo....bhebe nyanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…