Iran haina chaguo jingine lolote zaidi ya kujisogeza karibu na Dunia. Sera zake za kumiliki makundi ya kigaidi yanayoyasumbua mataifa jirani ya kiarabu, yameifanya Iran kutengwa na kuwa adui wa mataifa karibia yote ya kiarabu na Dunia. Maisha ya wananchi wa Iran yanazidi kuwa duni kila leo ukilinganisha na mataifa yote ya kiarabu yenye utajiri wa mafuta na hivyo kuifanya serikali ta Iran kuchukiwa na hata na wananchi wake. Mapato ya mafuta karibia yote yanaishia kwenye programu za kivita badala ya ustawi wa wananchi wake. Hali hii kwa ujumla imeichosha Iran, ndiyo sababu ya Rais mpya kutamka kuwa sera yake itakuwa ni kurudisha mahusiano na Dunia.
Vikwazo dhidi ya nchi yoyote Duniani ni kuifanya nchi hiyo itepete kisha irudi kwenye mstari. Iran imekwishatepeta, na imetamka kuwa ipo tayari kuachana na programu za utengenezaji silaha za nyuklia, kama kufanya hivyo kutakuwa na maslahi kwa wananchi wa Iran.
Hii ni nafasi nzuri kwa pande zote, kwa Iran, na Dunia. Iran kwa kuwa ina hofu ya kushambuliwa, kuwepo na mkataba wa kiusalama kati ya Iran na Israel na mataifa ya kiarabu, ambapo hakuna nchi itaruhusiwa kuishambulia Iran; Iran ifute mradi wake wa nyuklia na iyafute makundi yake ya kigaidi, na isifadhili makundi yoyote ya wanaharakati yanayozipinga serikali za nchi za kiarabu.
Iran ikiondolewa vikwazo, mapato yake ya mafuta yakaenda kwenye maendeleo ya watu, muda si mrefu inaweza kufikia maendeleo ya ustawi wa watu kama ilivyo Saudia au UAE.
Baada ya hapo vikwazo na kila mbinu vitumike kuitepetesha zaidi North Korea, huko wananchi wanaishi kama wapo jehanamu kutokana na utawala dhalimu wa Kiduku.