and 100 others
JF-Expert Member
- Feb 3, 2023
- 3,707
- 12,367
Amebadilika sana, nadhani alipo step down kuna jambo alijifunza na pia alipokoswa kuuawa, baada ya pale nilikuwa simuoni yule Trump ninayemfahamu... Amebadilika sana for good lakini... Nahisi atafanya makubwa...Trump kaja kwa style nyingine. Aliahidi ataondoa vita. Nadhani ndio kaanza mchakato.
Wamarekani gani hao wanaokereka?
Mimi najua wamarekani wanaoichukia Iran,ni wale wamarekani weusi wa Liwale na Nzega.
makobaz yamepaniki mazee dah ...hehe.. yaani yanakesha mitandaoni yakitunga habari za uongoo...eti mwamba trump aongee na lizee la ugaidi ayatola never...irani atulie asubiri dozi yake inaandaliwa freshiii
Nadhani ni harakati za US kuumaliza mgogoro wa Middle East! Iran ni key player wa vita vya Gaza,ndiye muungaji mkono wa vikundi vya Hamas na Hezibollah.
Huenda kuna makubaliano fulani kati ya US na Iran ambayo yatafanya Iran isiendelee kuunga mkono vita vya Gaza.
Pumbavu Wa pray for Israel mko wapi?
Wanaaibika kwa kuwa Hawana akili,
Asije akaharibu mambo zaidi maana hatabiriki
View attachment 3153357
Amebadilika sana, nadhani alipo step down kuna jambo alijifunza na pia alipokoswa kuuawa, baada ya pale nilikuwa simuoni yule Trump ninayemfahamu... Amebadilika sana for good lakini... Nahisi atafanya makubwa...
Kwanini Israel walianzisha kitu ambacho kiko juu ya uwezo wao?Kwa Sasa hatuhitaji vita Tena. Tunahitaji amani. Hata Mimi kwa Sasa naiona vita ya Israel na Hamas haina maana Tena. Tulete amani middle east maisha yaendelee.
Ko hii ni vita ya kidiniNiliwambia wakristo humu Trump.lazima atabadilika Iran ni moto wa kuotea mbali.
Kauli kama hiyo ya lisipotokea hili au lile mniite mbwa mimi huwa nawaona watamkaji kama watumia ugoro!!!!Kwann tukuite mbwa?wewe umetoa maoni yako sasa tena unataka uitwe mbwa? Hii kauli Huwa inatoka kwenye midomo ya wapumbavu na wajinga
mkuu why nzega? Mbona hakuna wamarekani huku?Wamarekani gani hao wanaokereka?
Mimi najua wamarekani wanaoichukia Iran,ni wale wamarekani weusi wa Liwale na Nzega.
Iran haina chaguo jingine lolote zaidi ya kujisogeza karibu na Dunia. Sera zake za kumiliki makundi ya kigaidi yanayoyasumbua mataifa jirani ya kiarabu, yameifanya Iran kutengwa na kuwa adui wa mataifa karibia yote ya kiarabu na Dunia. Maisha ya wananchi wa Iran yanazidi kuwa duni kila leo ukilinganisha na mataifa yote ya kiarabu yenye utajiri wa mafuta na hivyo kuifanya serikali ta Iran kuchukiwa na hata na wananchi wake. Mapato ya mafuta karibia yote yanaishia kwenye programu za kivita badala ya ustawi wa wananchi wake. Hali hii kwa ujumla imeichosha Iran, ndiyo sababu ya Rais mpya kutamka kuwa sera yake itakuwa ni kurudisha mahusiano na Dunia.Kweli kabisa. Ili middle East itulie, Iran ndio muhusika mkuu. USA na Iran wakikubaliana, Amani itarudi Middle East na Dunia itakuwa salama.
Hivi wewe jamaa huwa huchoki KUONGEA UONGO!??Iran haina chaguo jingine lolote zaidi ya kujisogeza karibu na Dunia. Sera zake za kumiliki makundi ya kigaidi yanayoyasumbua mataifa jirani ya kiarabu, yameifanya Iran kutengwa na kuwa adui wa mataifa karibia yote ya kiarabu na Dunia. Maisha ya wananchi wa Iran yanazidi kuwa duni kila leo ukilinganisha na mataifa yote ya kiarabu yenye utajiri wa mafuta na hivyo kuifanya serikali ta Iran kuchukiwa na hata na wananchi wake. Mapato ya mafuta karibia yote yanaishia kwenye programu za kivita badala ya ustawi wa wananchi wake. Hali hii kwa ujumla imeichosha Iran, ndiyo sababu ya Rais mpya kutamka kuwa sera yake itakuwa ni kurudisha mahusiano na Dunia.
Vikwazo dhidi ya nchi yoyote Duniani ni kuifanya nchi hiyo itepete kisha irudi kwenye mstari. Iran imekwishatepeta, na imetamka kuwa ipo tayari kuachana na programu za utengenezaji silaha za nyuklia, kama kufanya hivyo kutakuwa na maslahi kwa wananchi wa Iran.
Hii ni nafasi nzuri kwa pande zote, kwa Iran, na Dunia. Iran kwa kuwa ina hofu ya kushambuliwa, kuwepo na mkataba wa kiusalama kati ya Iran na Israel na mataifa ya kiarabu, ambapo hakuna nchi itaruhusiwa kuishambulia Iran; Iran ifute mradi wake wa nyuklia na iyafute makundi yake ya kigaidi, na isifadhili makundi yoyote ya wanaharakati yanayozipinga serikali za nchi za kiarabu.
Iran ikiondolewa vikwazo, mapato yake ya mafuta yakaenda kwenye maendeleo ya watu, muda si mrefu inaweza kufikia maendeleo ya ustawi wa watu kama ilivyo Saudia au UAE.
Baada ya hapo vikwazo na kila mbinu vitumike kuitepetesha zaidi North Korea, huko wananchi wanaishi kama wapo jehanamu kutokana na utawala dhalimu wa Kiduku.