Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Ungekuwa unajua kuna siri za nchi hazijadiliwi bungeni , usingesema hivyo. Wewe una USA Propaganda kichwani na unaziamini bila hata kuhoji. Unaruhusiwa kuendelea unavyoamini
Acha kuwa na mawazo mgando, uwazi wa uendeshaji serikali magharibi ni tofauti sana na kwa Wakomunisti. Nchi zote za magharibi bajeti zao za ulinzi kiujumla na taarifa za wazi, sio kama Wachina walioficha hadi takwimu za wagonjwa wa COVID wakaitumbukiza dunia kwenye janga la Pandemic.
 
Na anataka wapunguze silaha za nyuklia ila china wamemwambia aanze yeye maana yeye ndiiye mwenye silaha nyingi zaidi wakati china anataka awe na makombola buku kufikia 2030
 
HUYU KAKAA HUKO TANDAIMBA ANARISHWA PROPAGANDA ZA WACHINA NA WARUSI WALE HAWAJUI VIZURI KWA PROPAGANDA MAREKANI INA PRODUCTS NYINGI SANA ANAZIUZA TENA WEWE UNALIPIA BILA KUJUA INCLUDING GOOGLE
Kada wa CCP amesema anataka bidhaa ngumu tu za manufacturing, hataki mambo malaini ya Google, Android, Microsoft, Cloud computing, WhatsApp, VISA, Mastercard, bank, Movies, Music, Afya, Elimu n.k Wachina wao wanataka kazi za kutoka jasho tu!🤣🤣
 
Mbona hivyo vyote China anavyo. Sasa tofauti iko wapi?
 
Mbona hivyo vyote China anavyo. Sasa tofauti iko wapi?
Unaye hangaika naye ni western influenced kichwani, kwanza anaamini USA wako wazi kila kitu hadi military issues.
1. Ukimuuliza nani alimuua Kennedy na kwanini hajakamatwa?
2. Federal Reserve Bank nani anamiliki?
3. NASA propaganda au utendaji wake uko wazi na akina nani?
Kwanza hata yeye hawezi kuwa wazi kwa issue zake za kifamilia kwa kila mtu kiasi kwamba watu wanajua in and out ya maisha ya familia yake.
Anadhani ujinga ule wa USSR chini mapandikizi bado utatumika tena kuvunja nguvu za Urusi na China ambacho hasa ndio lengo kuhakikisha BRICKS inakufa, ni kwi inaweza ife kwa kuwatumia kama Saudi Arabia ambao wanaweza wahitoe ghafla, lkn Militarily China na Urusi wala NK hatawahadaa asubiri kizazi kingine sio leo
 
Umesema vyema, fantastic analysis
 
Na anataka wapunguze silaha za nyuklia ila china wamemwambia aanze yeye maana yeye ndiiye mwenye silaha nyingi zaidi wakati china anataka awe na makombola buku kufikia 2030
Yote haya kwa ajili ya binadamu? Tunahitaji common enemy kutoka sayari za mbali, tuna kiu sana ya vita sasa kukosekana kwa adui inabidi tujitengenezee uadui baina yetu.
 
Yote haya kwa ajili ya binadamu? Tunahitaji common enemy kutoka sayari za mbali, tuna kiu sana ya vita sasa kukosekana kwa adui inabidi tujitengenezee uadui baina yetu.
Wanakwambia bomu moja tu linatosha ila watu wanayo zaidi ya buku
 
Yeye USA Ni nani mpk anitake nipunguze bajeti ya pesa nilizotafuta kwa jasho langu.
Hawa jamaa USA huwa Wana kawaida hiyo,wakiwazidi wengine hukaa kimya,wakizidiwa hutaka ulinganifu.
Sijisemei kama porojo Nina mifano hai,
Mfano miaka ya 80 USA walipoona wamezidiwa na Urusi kwenye makombora ya masafa marefu wakataka uwepo mkataba wa kupunguza silaha Kali duniani.
Walipoona Urusi imeyumba kiuchumi na kusambaratika kwa USSR wakaanza kuunda Tena silaha Kali,Urusi alipowakumbusha wakamwambia kama anaweza na yeye anaweza kutengeneza,Sasa Urusi na china wamekua na nguvu Leo wanataka wapunguze bajeti za ulinzi.
Kwa kifupi Hawa jamaa ni wajanjawajanja.
 
Pia kiteknolojia na kiuchumi walipoona Japan imeizidi Marekani miaka ya 1980 wakaingia naye mkataba ulioitwa Plaza Accord na baada ya hapo Japan ikapoteana.

 
Tatizo liko kwako. Inaonekana wewe ni mmoja ya vijana wa kitanzania ambao wengi hawataki kusoma vitabu hivyo hawajui kabisa tulikotoka bali wanadandia vi-habari vya hapa na pale kwenye mitandao na kuanzisha ubishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…