Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Naona kuna baadhi ya waungwana humu jamvini wanashangilia taarifa hizi mbaya kwa ndugu zetu walio kwenye hiyo mitihani ya kuhitaji dawa hizo.......

Ki ukweli kibinadamu linapokuja jambo linalogusa afya au mustakabali mzima wa binadamu mwenzako ni vyema ukatunguliza utu kwanza...kwani mitihani chini ya jua sio ya mmoja.......

Maisha ni safari ndefu na hakuna ajuaye ya kesho.....na hujafa hujaumbika......

Si vyema kuleta kebehi, dharau ,vijembe na lugha za kuudhi kwa binadamu wenzako walio kwenye mitihani kwani hakuna mwenye kinga ya mitihani hapa chini ya jua.......

Tusijione wakamilifu na watakatifu kwa binadamu wenzetu kwa kuwa tu kwa wakati huu hujapata mitihani.....

Chini ya jua hakuna aliye salama.......
 
Hii kitu sio ya kushangilia, wakati tunasema ni bora ili Serikali ijitegemea ila tuelewe sio Tanzania peke yake inayotegemea hiyo misaada, zipo Nchi zilizoathiiriwa sana na zinauhitaji mkubwa sana wa hizo dawa, so tutarajie vifo vingi vya watoto wachanga, watoto njiti na watu wenye maambukizi ya ukimwi maana imekuwa ghafla. Naamini hakuna Nchi ilitarajia hili
Chalamila aliposema wajawazito wakazalishwe, sijui kama ni neno sahihi, na waume zao kuna watu walishangilia kwa maana kwamba tuishi kwa kuchangia tusipende vya bure. Trump kaja na style ya chalamila, mapovu yanatutoka! Tujitafakari wenzetu wamewezaje hadi sisi kuwategemea wao ndiyo maisha yetu yasonge mbele?
 
Nasema n ww Trump MUNGU ni mkali.samehe Africa n watu Wake.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
God bless Donald Trump.

Tumezoea kuwa tegemezi kwa zaidi ya miaka 60 tokea tupate uhuru.

TANGANYIKA yetu iko mbioni kurudi!

GOD BLESS TANGANYIKA
 
si jambo la kufurahia lakini
Utegemezi umedumaza maendeleo ya bara hili lenye kila aina ya raslimali.
Sasa umefika muda wa kuzikabilii changamoto zetu kupitia raslimali tulizonazo.
Well said.
Bara la Afrika linaenda kupoteza zaidi ya nusu ya watu
Hilo haliwezekani, tunakubalina hapo. Kwani sio kweli nusu ya watu wa Afrika wake wana magonjwa hayo uliyoorodhesha chini.
wake kwa malaria, ukimwi, pepopunda, kifaduro, surua, kifua kikuu nk.

Itoshe.

Haya magonjwa yote yaliletwa na hao hao? Manake tumefundishwa hapa JF kwamba kila kitu wanaleta wazungu, teknolojia, simu, arvs, panadol, bunduki, V8, yani kila kitu kuna ukweli ngani hapo? Na wapo wajinga na wapuuzi wengine wanasema hata kuongea tumefundishwa na Wazungu.

Mawe

Itoshe, watakaokuja pata hasara ni makampuni yao wenyewe wanaotengeneza na kuuza hayo madawa.

Pause for a Min

Deepshit AI, iliyotengenezwa kwa chini ya US$50 milioni, imeenda kuondoa US$600 bilions kutoka kwenye masoko. Wanahangaika huko sasa kuwatengenezea nadharia kwamba AI zao ni bora.


Again think for a min, mathalani tumeacha kununua V8 tano tu tukawekeza kwenye kikombe cha babu na kufanikiwa kama Deepshit. Unafikiri yale makampuni makubwa yanayotengeneza haya madawa watakubali US$600 billion zipotee tu?

My point is, inawezekana kabisa tunazo dawa za mitishamba ambazo zinaweza fanya maajabu kama hizo ARV tena kwa hali ya juu kwa kuwekeza fedha kidogo sana,(kama deepshit) ni Uamuzi tu.

Tufanye nini?

Tunaweza kujiondoa huko WHO, na hilo litatupunguzia Bureaucracy, na vizingiti vyengine<>tukiwa tayari kurudi, tunawaambia wabadilishe hizo Standards ambazo kwa Uhakika, na kwa mda mrefu zinatufinya na tafiti zetu na madawa yetu kwa vigezo vya "Standards" tumshukuru Trump kwa kutuamsha, tena, hata yeye amewaomba waamke kuhusu DSeek

Hata hivyo, hili suala, pamoja na shamrashamra zake, zitakuja kuwatokea puani si mda mrefu Na vile wanavyokomoana, it is not sustainable<> kwa mfano, hawa watengenezaji wa madawa wanaeza sema wapandishe bei za madawa mengine ili kufidia hasara wanayopata kwa kutonunuliwa ARVs na madawa mengine huko, in the end itawagusa Wananchi wenyewe. Katika ahadi zake, amesema anaenda kupunguza makali, na hata bei za Bidhaa, Prescriptions drugs Included. Narudia, hiyo action is not sustainable.Trump na chama chake wataanguka, uchaguzi mdogo 2027 wasipoangalia.

Hii plan yake siyo sustainable na anajua, walakin let us not be complacent.

Amkeni.
 
Kweli kabisa,acha awanyooshe mbwa hawa. Si tulisema huyu mtu hafai kabisa
kwani amekosea wapi?...yeye anajali maslahi ya nchi yake,..kama viongozi wenu nao wanajali maslahi ya nchi zenu tatizo liko wapi?...si mnalipa kodi?...kodi zenu zitawanunulia ARV...so tulieni...
 
Kuna boya ana mikosi yan kyuma ya 5 kapata ukimwi wadudu hawajaanza kuzaliana ARV stoop
Habibu kundemba UMETUPONZAA
 
Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
 
Back
Top Bottom