TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tabata kimanga internet ya ttcl inasumbua sana. Njooni mfanye uchunguzi
 
Mtandao wenu hauaminiki kabisa yaani, kuna siku nilijiunga kifurushi cha "toboa night" halafu ghafla mawasiliano yakakata. Kupiga simu huduma kwa wateja najibiwa "utopolo". TTCL huduma kwa wateja bado kuna ubabaishaji mkubwa, mjirekebishe, soko la mawasiliano lina ushindani mkubwa sana.
 
hawa TTCL nilisikia mwanzoni wakisifiwa nikaingia mkenge nikatafuta laini nikanunua..mpaka sasa najuta. Unanunua kifurushi internet iko speed ya konokono..hata ukituma meseji tu ya maneno ya watsap inachukua zaidi ya dakika kuwa sent. Ukiwapigia simu wanajifanya kukuambia eti oooh...labda settings kwenye simu yako hazijakaa sawa...yaani wanakera...Nimeamua niiweke pembeni natumia airtel tu. wajirekebishe sana.
Kwanza hizo vocha zenyewe unaweza kumaliza mji bila kuzipata. Ila nawapongeza kwa kuungana na tigopesa kwenye suala la kununua salio
 
Vocha zinapatikana vizuri tu siku hizi
 
Utopolo???
Ndio nini
 
Tatizo wahudumu wenu hawako romantic yan ukifika mteja ni kavu kavu hadi huduma inaboa sana hasa hao weusi
 


Tunaendelea kukujali kwa kukupa muda wa maongezi kupiga simu kwenda mitandao yote ukiwa na Laini ya TTCL.
RudiNyumbaniKumenoga!




Furahia kifurushi LONGA PACK kinachokupa Dakika za kutosha kupiga mitandao yote kwa gharama nafuu zaidi, kujiunga piga *148*30#.

RudiNyumbaniKumenoga!
 
Tatizo TTCL sijui mnafeli wapi yani

Mnaanzisha Threads halafu tukichangia mnakula kona hamjui sisi ndo wateja wenyewe au tunataka kuwa wateja. Makampuni mengine vifurushi vya internet ni gharama nyie mnaonekana nafuu ila internet yenu inasumbua watu wanalalamika badala ya kutoa maelezo na ufafanuzi mnakimbia.

Halafu weekend ndo imeisha ndo mnaleta tangazo la kifurushi cha weekend😁😁. Sijui hizo Marketing zenu mlisomea Burundi au Korea ya Kaskazini??
 
Upo pande za wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…