TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Walinchosha nilipokuwa sehemu fulani karibu na downtown alafu simu inasoma ROAMIN aisee eti jamaa wanagongea mnara wa Tigo tena Dar es salaam! Aibu sana
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
 
Kwanza sina budi kutoa pongezi zangu kwa shirika hili la simu jinsi lilivyoingia kwenye soko la mawasiliano na huduma zake za maongezi T-PESA na INTERNET YA KASI KUBWA Kwa Bei nafuu, huku wakiwa na kaulimbiu yao ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA, kwa sasa mlipoharibikiwa ni hapa:

1. Kusajili laini zenu kwa fingerprints Dar es salaam mzima, huduma inapatikana Kariakoo na Posta tu.
2. Huduma ya vocha na T-PESA, mawakala hamna, ili update ni lazima upitie AIRTEL MONEY.
3. Ile internet ya 4G mlikuwa mnatupatia, kwa sasa hata ZERO-G haifiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
 
Sina uhakika na taarifa zako kuhusu usajili kwa alama, mimi nimesajili line yangu kwenye office zao za Mbezi beach, na nna uhakika kila kwenye office yao kuna hiyo huduma

Niko mkoani tena Bush na nnapata 4G vizuri tuu japo kuna maeneo yana changamoto, ila si kwa TTCL pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
 
Binafsi nilikua napata vizuri tu, lakini Sasa hivi, internet inapanda na kushuka nipo maeneo ya wilaya ya temeke, temeke yote usajili wa fingerprints hamna ukitaka nilazima uende Posta na kariakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
 
Yaani mwezi wa 5 nilisajili namba yangu ttcl kwa njia ya vidole kwenye Ofisi yao Mkoani, leo natumiwa sms zimebaki siku 5 za kufunga dirisha la usajili kwa alama za vidole. Ikabidi nihakiki tena kama namba imesajiliwa nakuta haijasajiliwa. View attachment 1324338

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa changamoto hiyo,tafadhali tufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.
 
Binafsi nakaribia kukataa tamaa na Hao ttcl, mwanzoni walikuwa poa Sana, ila nimeona juzi Kati wamebadili bei ya vifurushi, na kuvinyima Thamani baadhi ya vifurushi,
Kulikuwa na kifurushi Cha mwezi mzima mtandao yote dakika 470 kwa sh14500, hakipo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.
 
Niliwaona hamna kitu baada ya kuweka tariff za Tpesa sawa na akina MTpesa ilhali wao ni wachanga kwenye hiyo huduma. Halotel wanahangaika hadi wanashusha tariff ili waweze kushindana ila hawa wetu wamebeteka tu.
Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.
 
Mie nilisafiri kutoka ushirombo Hadi Geita zaidi ya km 360 kusajili line ya ttcl hiyo mivoda na Airtel wafunge tu nshatoa pesa zangu
Tunashukuru kwa kutuandikia,Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.
 
Tatizo la ttcl kuna maeneo hakuna network kabisa kama huku kata ya kamhanga, GEITA hakuna signal hata kidogo.
Mi nilinunua line yao lkn nashindwa pindi ninapokua huko kituo change cha kazi. Huwa naitumia hadi ninaporudi GEITA mjini. Hata kuweka pesa cwezi kwa sasa kwa ajii ya ukosefu wa network.

Nawaomba/naomba serikali sikivu itufikirie na cc wa mashambani tutumie ttcl yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunashukuru kwa kutuandikia,Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.
 
Aisee hili shirika letu linahujumiwa si bure, haiwezekani wapeleke gawio kwa JPM huku wakijua kabisa kuwa minara yao haitoshi , vocha hazitoshi mji mzima, wanapitwa hadi na watoto HALOTEL na AIRTEL
Tunashukuru kwa kutuandikia,Hatua za kuboresha huduma zetu zinaendelea kufanyika ili kuwapatia wateja wetu huduma iliyobora.
 
Back
Top Bottom