Kuna watu wako neutral aisee , hawazuzuliwi na sisiem hata kwa maneno au vitendo ambavyo mwenye akili anajua vinafanywa kama hadaa wapate kura, lkn pia wanaangalia Upinzani kama watu wanaostahili kupewa nchi na wala si Mamluki .
Fikiria leo wanabadili Wimbo wa Taifa, halafu wanaona haina madhara . Ni kweli kuuimba au kutoimba haubadulishi hali ya barabara zetu , au mfumo wa elimu lkn huo ndio nembo ya NCHI
Ipo siku watabadili bendera kuwa ina shida, watabadili taratibu za nchi, watabadili tamaduni na utaifa. Na kweli WATABADILI
Je Ujasiri huu unatoka wapi?
Waliona weakness ya Katiba na Sheria za Nchi. Na ZIPO NYINGI
Wanapata Ujasiri kusema kashtaki ,maana wajua hakuna kifungu kinawatia hatiani.
Lkn ukwelu HAWAFAI
Kutokomaa kisiasa kuliko pitiliza nadhani wataomba msamaha maisha yaende hakuna MKAMILIFU chini ya Jua ila WAMETELEZA
Lkn ukisiakia wanasema liwalo na liwe. Basi wenye akili watajua. Je UJASIRI HUU UNATOKA WAPI?
NANI YUPO NYUMA YAO?
Wengine sijui wamesingizia kuwa safari hii hakuna kumsubiri Mungu wananchi WATAINGIZWA BARABARANI. Ok sawa
Vyombo vyetu vya Usalama angalieni NDANI na NJE huenda seemu kinatokea Kiburi.
Tujenge vyama kama Simba na Yanga
Ushabiki Mzuri wa Vicheko mnakwaruzana uwanjani hata kurushiana mikojo lkn mnacheka mnapeana zawadi kwa kumfunga mwenzako.
Ova.