2-3 years is good, hiyo miezi 6 una taka ulie kwa kirumi
Miaka 2 hadi 3 kama ni mwanamke ulimkuta ana 22 ina maana utakaa nae hadi 25 ndipo ufanye maamuzi,hii miaka 3 utakuwa unafanya nini au unachunguza nini mzee?
NItakupa mfano, kuna siku nikiwa mitaa ya Mindu, Upanga nimekaa kwenye ghorofa linaitwa Richmond tower namsubiria rafiki yangu ashuke twende sehemu nikaona nipige story na mlinzi. Yule mlinzi alitokea tu kunikubali sana sababu ya mambo tuliyokuwa tunaongea na namna nilivyomchangamsha.
Baada ya kuongea kama dakika 20 hivi akanambia kuna Bluetooth speaker anaiuza nimpe chochote kitu. Nikamwambia niione. Akanipa. Ilikuwa ni spika ya kampuni inaitwa Boze (wanaozijua hizi speaker zina maajabu nadhani kama si sawa na JBL basi zinaipita JBL) kwa wakati ule sikuwa nazijua kabisa. Nikajua ni brand za kichina.
Nikamwambia anauzaje, akanambia nimpe elfu sabini. Mimi nikamwambia hiyo sina labda elfu 40, akanambia labda 60, nikamwambia tufanye 50, akanambia poa tufanye biashara.
Kwa muda ule sikuwa tayari kuilipia ile spika na ilikuwa ni mpya kabisa alipewa zawadi na mtu alikuwa anaishi hapo hapo kwenye apartments za Richmond kipindi anaondoka kurudi kwao.
Alikuwa ananitafuta nikapiga chenga nikijua nitakwenda muda wowote kuichukua hiyo speaker hata hivyo speaker za mchina zipo nyingi naweza pata huko madukani au kuagizia why niwe na pressure ya kununua used tena kwa 50,000.
Siku zikaenda nikapita tena, safari hii hakunikumbusha tukasalimiana ila akaniambi, " speaker yako nimeuza kwa dogo wa kihindi m'moja hapo alinikuta naitumia akaipenda,akaniambia nimuachie. Aliponiuliza bei nikamwambia ajilipue akaropoka laki moja,hata sikutaka kubishana nikamwambia poa. Akaenda kwao akachukua hela akaniletea nikampa speaker."
Mimi akili ikastuka,nikasema ngoja nichunguze why muhindi alipie laki bila utata kwa kitu ambacho mimi nimeleta pozi kukinunua kwa elfu 50?
Niliporudi home jioni,nikaingia mtandaoni uzuri nilipiga picha ile speaker na lebo yake niliipiga picha so serial numbers nilikuwa nazo. Nilipozisearch ikanipeleka straight kwenye website ya Boze ndipo nikajua kuwa nimepuyanga. Ile speaker thamani yake ni zaidi ya laki 7. Ukiweka kwa pesa ya kibongo kutoka dola.
Aisee nilijilaumu sana. Nikajifunza somo muhimu sana kuhusu kuwa na maamuzi yakinifu ila ndani ya muda mfupi mara tu ninapokutana na fursa ya jambo lolote.
Nimekupa story hii ya kisa changu ili upate kujifunza kuhusu maamuzi muhimu ambayo hayataki chenga nyingi. Hiyo kitu hata katika mahusiano ina apply pia. Unapokutana na mwanamke katika maisha yako na amekaa mkao wa kufanya nae mahusiano serious usisubiri miaka 3 ya kuprove wrong.
Miaka mitatu utakuwa unataka mtu awe ni malaika kuishi nae. Ila vigezo muhimu ndani ya miezi sita hadi mwaka ukiweka mikakati ya kijeshi unakuwa na zaidi ya nafasi 1000 za kubaini mtu wa hovyo na wamaana.
Mwanamke ukae nae miaka 3 haujamchumbia ni mnapika, mnapakua na kutandika kitanda day in day out lazima atasoma ishara kuwa humpendi na hauna mipango nae ya baadae na yeye ataanza kuishi na wewe kimashaka huku akiandaa exit strategy kitafuta mahusiano serious nje ya situationship yenu.
Miezi 6 hadi mwaka unakuwa ushajua kuwa huyu ni mke ama sio. Na kama umejua ni mke, haitakugharimu zaidi ya milion 1 na nusu kila kitu katika kumchumbia especially kama wazazi mpo nao mkoa huo huo na utafanya vitu vyako bila mbwembwe za bongo movie.
Mambo yasiwe mengi, weka ndani chunguza miezi yako sita, mwaka amenyooka,mwambie mpenzi nataka nikupandishe cheo,peleka washenga kwao, toa posa,lipa mahari, chukua mali kiuhalali huku mnapanga sherehe ya ndoa. Unakuwa mume na mke halali.
Haya mambo ya kuchunguzana miaka 3 au 5 huyo mwanamke hazeeki? Wewe umri hauendi?ππ