Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Paskali, mwanzoni nilidhani na wewe huwajui "Wasiojulikana" na Wasiojulikana. Lakini nimeacha imani hiyo. Unawajua wote wa aina mbili na ndo maana unakimbilia kukosoa thread yangu badala ya kujikita na maswali niliyouliza.
Mkuu Baija, nchi inaongozwa kama familia, hata wewe ukiwa nyumbani, kama mtoto wa kiume unaejitambua, siku mama yenu amesafiri kwenda kijijini kwao kusalimia, huku nyuma baba akaingiza mgeni, na ukamuona. Kumbe yule mgeni aliacha chumbani kwa baba nguo yake fulani, uvunguni mwa kitanda, bila baba kujua, ama kwa kusahau kwa bahati mbaya ama kwa makusudi ili mwenye nyumba aone na ajue kuwa hayuko peke yake.

Mama aliporudi, kukaibuka ugomvi mkubwa kati ya baba na mama kuhusu hiyo nguo imetoka wapi, imeingiaje uvunguni mwa kitanda, imeachwa na nani, na katika shughuli gani?.

Baba kamwambia mama hamjui mwenye nguo hiyo wala hajui chochote kuhusu nguo hiyo imeingiaje,labda watoto au msichana wa kazi alijichanganya.

Kwa vile wewe uliona picha nzima, jee utamweleza mama ukweli wa ulichoona?.

Hiyo ndio essence ya wasiojulikana hawa
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Kama baba amesema hajui nguo imefikaje, who are you kusema imefikaje?.

Kama yule aliyemshikia Nape bastola naye hajulikani mpaka leo bado anatafutwa na polisi wetu na hajapatikana, what are the chances kuwabaini wasiojulikana wa Lissu?.

Wana familia bora, wanamwamini baba mwenye nyumba, hata kama wewe ulimuona mgeni wa baba, lakini hukumshuhudia wakati akiivua hiyo nguo na kuiacha uvunguni mwa kitanda chumbani kwa baba, hivyo kama baba kasema hajui, then it might be true, ni kweli kabisa baba hajui, na hiyo nguo iliachwa siku nyingi nyuma na mgeni mwingine ambaye hata wewe hukumuona.

Hivyo nilitoa angalizo hili
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Kwenye hili la kuwabaini wasiojulikana wa Tundu Lissu, serikali yetu bado haijashindwa, nilisema humu, kwa vile tupo watu wenye uwezo kuisaidia serikali yetu iweze kuwabaini, nikauliza jee tujitolee tuu kuisaidia serikali yetu kuwabaini na kuwataja watakaotusaidia kuwabaini wasiojulikana hawa au tuisubiri, serikali iseme imeshindwa ndipo isaidiwe?.

WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums

P .
 
Mama Sabrina, yes nimeoa, tena ni ndoa ya Katoliki, ili pia mimi nadumisha mila nzuri za asili yetu, miongoni mwa mila nzuri za kabila langu, ni pamoja na kutokuwa na idadi ya mwisho ya wanawake, wala sipangi uzazi, hivyo kama vipi sema tuu.
P.
Ha ha ha, ili mradi tu awe cheupe dawa asisahau hili mhimu sana!
 
Nimesikiliza mahojiano ya Tundu Lissu kwenye kipindi cha Hard Talk cha BBC TV, akizungumzia mhusika wa Shambulio lake, nikaona hizi ramli zibaendelea.

Nitatoa ushauri kwa Kamanda Simon Siro, hata kama hakuna nia ya kufanya uchunguzi angalau wajifanyishe tuu kuwa they are doing something, wajifanyishe wamewatia ndani walinzi wote waliokuwa zamu siku ya tukio, wajifanyishe wamemkamata aliyezifungua zile CCTV za aneo la tukio na HDD ya recording imepatikana, waendelee kusisitizia bado wanamsubiria dereva wa Lissu ambaye ni shahidi muhimu na kusubiria maelezo ya Lissu ili angalau jumuiya ya kimataifa ijiridhishe kuwa at least we are doing something kutapunguza hizi ramli.
P
 
Hayaweza kufanyika hayo unayotaka
 
NAAMINI YASHAFANYIKA NA MGONJWA SAIKOLOGIA ANASUBIRIWA AJE AKAMILISHE USHAHIDI
 
Na walivyo bogus wanaweza kujifanyisha hivyo na wakibanwa wanasema "sii ndivyo ameshauri Pasco wa JF?"
 
Nani mwenye nguvu za kimamla hata afanye hayo unayo sema yafanyike?....... Alafu unahimiza tusihukumu!!!!
 

Kwa hiyo watu wanyamaze tu, wasiseme lolote kwa sbb Mungu mwenyewe ndiye atahukumu?

Na mwathirika wa tukio akiulizwa ilikuwaje, ajibu........ Aaah, bwana usiniulize kwa sbb mambo haya karma (nature) itayaamua??

Nionavyo mimi ni hivi:

Tuache watu wazungumze, watoe hisia zao maana kupitia hisia hizo ndipo tunapoweza kupata majibu ya kila jambo, kila hoja!!

Na kwa taarifa yako tu ni kuwa, whether watu wazungumze kwa kutoa maoni, hisia ama watoe hukumu zao za kweli ama uongo, kamwe haiwezi kumzuia mtoa hukumu ya haki kutoa hukumu yake kwa kila tendo jema ama baya la kila MTU!!
 

Hadi sasa hakuna aliyehukumiwa kwa jaribio la kutoa uhai wa Tundu Lissu. Wapo waliohisiwa kuhusika
Wapo waliotuhumiwa kuhusika na jaribio hilo la mauaji. Tuhuma ndio hupelelezwa ili kupata muhusika atakayehukumiwa. Mtuhumiwa anapaswa kujitahidi kujisafisha/kukanusha tuhuma na sio kuongeza uzito wa tuhuma dhidi yake.
 

Siku karma ikifanya kazi , Mtemi atakuwa ameshapoteza wengi
 
Najisikia kichefu chefu kwa andiko lako. Unajifanya kipofu hali ya kuwa unaona. Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Aqulline. Polisi wamesha conclude Mbowe anahusika mbona hukuandika kuhusu hilo. Polisi wamesahaconlude Tundu alipigwa risasi na wasio julikana, hali ya kuwa akili ya kawaida haikubali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta ndimu ulambe, embe bichi, mbilimbi au ukwaju utulize kichefuchefu chako, ni kawaida ikiwa changa, baadae kitatulia.

Kichefuchefu chako kikitulia take time kutembelea mitaa hii, ila kama ni changa sana, bora tulia kwanza, maana hautasikia kichefuchefu tuu, unaweza kutapika kabisa.

Kuhusu kifo cha Akwiline.
Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel! - JamiiForums

Kuhusu wasiojulikana
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums

P
 
Hiyo bakora ikija si ajabu ikawa sote ameshatukolimba , utajuaje kama karma imempiga bakora??
It's true, bakora za karma ni kama ufalme wa Mungu, kwa maana hamjui siku wala saa, na bakora zikitembea hakuna taarifa kuwa ndio bakora, ni majanga ya kawaida ya ugonjwa au ajali etc, the bottom line ni lazima upigike, madaraka, mamlaka au pesa, can't do a thing.

P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…