Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Usimuhukumu mtu bila kujua,siku nikiweka Siri ya familia ya Mzee malecrla hapa hata wewe ungekuwa zaidi ya lemutuz.
Lemutus alikuwa na msongo wa mawazo,alijua tu atakufa siku si nyingi
We jamaa Una masiri mengi mengi hebu yamwage hapa
 
Kwanza, ninapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, washikaji na wanaJF walioguswa na kifo cha William Malecella. Mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.

Sasa, twende moja kwa moia kwenye mada, kupitia mada hii, bila kuficha wala kumumunya maneno, William Malecela (Le mutuz) alijulikana na kufahamika zaidi kama mtu wa ovyo kwa sifa hizi (sifa ambazo alikuwa akijivunia nazo hadharani mitandaoni na mitaani);

1. Mpenda sifa popote.
2. Mpenda pombe.
3. Mpenda umalaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)

Le Mutuz japokuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akijaliwa kuwa na watoto, akipambana kwa namna mbalimbali kutafuta kipato, huku akitokea kwenye familia ya mzee Malecela yenye heshima kubwa sana kisiasa na kijamii ndani na nje ya Tanzania, lakini mienendo na tabia za Le mutuz zilikuwa zenye kutia aibu na kinyaa, akiishi kama kijana aliyepevuka juzi, aliyekosa malezi yoyote ya kijamii na kidini.

Japokuwa hayo yalikuwa ni maisha yake binafsi (sio busara sana kuyahukumu) lakini ni vyema kusema ukweli na kuweka angalizo muhimu kwa vijana ambao ndio wamejaa mtandaoni kuwa makini na kukwepa kuiga au kujifunza kupitia maisha binafsi ya Le mutuz ambayo yalijaa anasa na uchafu mwingi.

UKWELI USEMWE KIKAMILIFU.
Haya ungemwambia alipokuwa mzima ukiyasema sasa ni sawa na uzandiki tu.
 
No facts no comments
 
Unaposema fulani alikuwa mfano mbaya kwa jamii kwa kutumia hivyo vigezo vyako hapo, unamaanisha wengine wote tuliopo hapa ndio mfano mzuri?

Tatizo unafiki umechukua sehemu kubwa sana ya maisha yetu, wengi mnaomponda Lemutuz hapa mnajiona nyie ndio malaika, mfano mzuri kwa jamii zenu, kumbe upo uchafu wenu mwingi tu mnaoufanya sirini.

Kosa pekee la Lemutuz ni kuamua kuwa muwazi kwa maisha yake, kitu ambacho nyie wengine kimewashinda, kwanza unapata wapi "mandate" ya kuhukumu "life style" ya mwingine, mnataka wote tufanane?

Kwanza yule hajakulia huku, maisha ya ughaibuni ndio kwa kiasi kikubwa yalimfanya awe vile, factors kama hii ulitakiwa uiweke kwenye "consideration" kama una upeo, bahati mbaya hamna, tokeni nje ya hilo box mlilojifungia.

"Ukweli usemwe" ... Nonsense!.
Kukulia nje sio sababu labda useme maisha ya watoto wa viongozi waliowengi wana maadili mabovu ni wachache sana walionyooka, ndio haohao kama wa Simba Chawene
 
Namjua Lemutuz wakati anaishi New York ingawaje hatukuwa karibu sana, very nice guy, mambo ya familia hatujui na sote tuna matatizo yetu, alipenda kula shangwe zake tuu, pombe au mademu 90% humu tunahusika na haikufanyi uwe mtu wa ovyo, na idea ya mfano mbovu kwa vijana sijui maana yake nini, mnashindwa kuwafundisha vijana wenu leo mnamsingizia Lemutuz, wapuuzi sana nyie na watoto wenu wote
 
Marehemu alipenda kusifiwa kama yeye ni mtu wa kuponda starehe kwa kiwango cha SGR, kwa hiyo tukionya jamii isiige maisha ya namna hiyo tutakuwa tumekosea?
Na ninaamini ni lifestyle yake ndio imemtanguliza mbele ya haki, na sio huyo tu bali ni watoto wengi wa viongozi, wengi wana tabia mbaya na afya mbovu.
 
Back
Top Bottom