Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kutokana na kuenea kwa elimu ya fedha, kwa sasa Watanzania wengi wamehamasika kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Cha kusikitisha ni kuwa wawekezaji wanakwama kwa stockbrokers ambao ndio wanahusika kumnunulia au kumuuzia hisa mwekezaji. Kwa sasa mitandaoni kuna malalamiko mbalimbali kuhusu madalali hao kuwa na huduma mbovu, kutojibu malalamiko ya wateja n.k.
Kwenye soko la hisa, muda ni zaidi ya mali. Dalali akikuchelewesha hata siku moja tu tayari ni hasara kubwa kwa sababu bei ya hisa inabadilika kila siku, na kwa soko la hisa la Dar es Salaam bei ya hisa ni kama inapaa kadri siku zinavyozidi kwenda.
Hivyo basi, tupeane uzoefu: dalali gani ana huduma nzuri na yupi ana huduma mbaya. Ili wawekezaji wanaosumbuka na madalali wabaya wawahame, kwa sababu inakera sana.
Mi naanza na dalali wangu msumbufu anaitwa Orbit Securities Co Ltd. Simu hawapokei, meseji hawajibu; yaani ni kama vile mimi ninawalazimisha wanihudumie, tena wanihudumie bure.
Mwanzo hawakuwa hivi, lakini kwa sasa huu usumbufu umenifika kooni, lazima nihame.
Karibuni tusaidiane.
Maoni ya Mdau;

Issue sio Broker issue ni Unauza Hisa Kiasi Gani?Hivi kweli Mtu una Portfolio ya 50k unataka Broker akutazame seriously?mnafikiri soko la hisa ni UPATU(Ponzi scheme) au kibubu?
Kama unataka Dalali ukachukulie serious kwanza uwe mwekezaji serious Sio umenunua Vihisa Vya Milioni 20 hata mwezi haujaisha ushaanza kutaka Kuviuza upate hela ya BIA.Kama tabia yako ni hio nenda UTT huko wao hawana Brokers wala nini.
Ujumbe wangu haulengi kuwavunja moyo wawekezaji ila ni kuwaambia tu kwamba Soko la hisa ni Play Ground ya watu wenye Ukwasi na ambao wana BUY na KUHOLD na sio kila siku kuuza na kununua mnafanya SOKO linakuwa na FUJO.Hisa zinapanda Bei bila uhalisia kwa sababu ya watu ambao hawana utulivu.Wakisikia za CRDB zinapanda wanakimbizana nazo mara wakisikia sijui za nani zimeshukua wanaanza kuuza kama nyumbu.
Matokeo yake mnafanya SOKO linakuwa Volatile kiasi kwamba Biashara ya Hisa inakuwa kama ya maandazi.
Kingine Zingatieni.Kwenye mfumo wa HISA wa DSE unapoweka BUY or Sell Order sio kwamba inafanyika in real time.Yale ni kama maelekezo kwa Broker wako,Na huwa hauko mwenyewe unayefanya Buy or Sell Order.Na ili Upate Hela lazima kuwe na Order match ya Buy na Sell sio ufikiri kwamba Ukiwa Bar ukataka kulipa Bill basi unaweza tumia hisa zako za laki moja kulipa Bili.
Stock Market is not for Broke People.Stock Market is for the Rich.Watu ambao wako katika level ya Financial Freedom na Pesa zao zinawafanyia kazi.
All in all Brokers wote wako vizuri na wanafanya kazi zao vizuri.Cha muhimu hakikisha Unatembelea ofisi ya Broker waka angalau mara moja hasa ukianza kuwekeza Pesa nyingi ili ufahamu aina ya watu ambao wanasimamia Pesa zako na pia ili wakushauri vyema ni wakati gani wa kununua,kuuza aua hata kufanya Private Sell.