Umeongea ukweli na ikitokea wawekezaji wakubwa wakaamua kuuza hisa zao tutakimbiana..!!Hapana Mimi sio Broker Msumbufu.Ila Niko kwneye Game ya Share Tangu kipindi Shares zinauzwa Manually.Kipindi kili kwanza ukienda kwa Broker na Kamilioni Unataka kununua Hisa anakupiga Darasa wee mpaka mnaamua kwenda kutumia Hio Milioni Pale Serena Happy Hour Kunywa BEER ili upate Connection za Kutengeneza PESA ya Maana.
kiwango kizuri chakuwekeza kwenye stock ni kiasi gani labda tupe elimuWell
Elimu yangu ni Simple.Kwenye Hisa kama mtaji wako ni mdogo nunua HISa kwa ajili ya kuhudhuria AGM yaani vhisa vichache halafu unavisahau ikifika wakati wa AGM unaenda unafanya Networking ili ufahamiane na watu hasa hizi face to face AGM zinazofanyika UKUMBINI.
Kama lengo lako ni kutengeneza Portfolio nzuri Anza na UNITS kama za UTT au Similar Mutual Funds Wekeza kule kidogo kidogo mpaka ufikishe kiwango kizuri cha Fedha kisha sasa ndo uanze kuwekeza kwenye STOCKS.
Ukitaka kuingia kwenye STOCKS hakikisha unafahamu namna ya kusoma Taarifa za Fedha,namna ya kufuatilia hali ya uchumi na namna ya kufanya manunuzi ya HISa.Usifanye Impulse Buying or Selling.
Mwisho Brokers wote wanafanya kazi sawa.Wanasimamiwa na sheria zinazofanana na wanawajibishwa na mamlaka ya usimamizi wa mitaji CMSA.Kama Broker ana violations fulani basi sehemu sahihi ya kufikisha Taarifa ni CMSA ili wao wamsimamie na kumuwajibisha.
Mwisho ila sio kwa Umuhimu.Kabla haujaanza kukimbizana na Hisa Hakikisha Una cashflow ya kueleweka maana hisa sio kwa ajili ya akiba akiba huwa inakaa Benki.
Vile vile kama unamiliki hisi zenye thamani ya kueleweka hakikisha unazipeleka Benki,Unachukulia Mkopo na Hizo zako ziwe Dhamana.Hiyo inakusaidia sana kufaidikia hasa hisa zinapopanda na kushuka Bei.
Kwa mfano kama Una Hisa zenye Thamani ya Milioni 100,unaenda Benki unachukua mkopo wa Milioni 50 unaweka kwenye Biashara zako nyingine unawapa Share Certificates kama Dhamana yako.
Cha muhimu katika Hizi biashara za Hisa ni kuwa na Proper Planning kwani kufilisika na kutajirika ni mara moja.
Ni muhimu Pia ukafuatila INDICES za soko la HISA huwa zinakupa Picha ya Hali ya SOKO na uelekeo wa soko.Fuatilia hasa DSE Index ambazo zinatangazwa mara kwa mara
We jamaa unazingua ati vimtaji vya 100m 😂Mkuu uko njema kwenye maswala ya hisa,Sasa unatushauri nin sisi wenye vimitaji vya 100m tunaotaka kuwekeza kwenye hisa
Sasa we unaona hiyo 100m ninyingi kwenye soko la HISA,siunaona mdau anakwambia watu m500We jamaa unazingua ati vimtaji vya 100m 😂
Unadhani mtaji wa 100m kwa Tanzania DSE unakuweka kwenye percentile gani definitely kwenye top 10% in my opinionSasa we unaona hiyo 100m ninyingi kwenye soko la HISA,siunaona mdau anakwambia watu m500
Sasa mkuu kwenye m100 hapo kwa hisa za crdb siunaona utapata hisa chache tuUnadhani mtaji wa 100m kwa Tanzania DSE unakuweka kwenye percentile gani definitely kwenye top 10% in my opinion
Kiwango kinategemea na Ukwasi wako.Kiwankiwango kizuri chakuwekeza kwenye stock ni kiasi gani labda tupe elimu
Wengi Mnaingia kwa mihemko katika Uwekezaji huu Bongo. Hamna Elimu sahihi juu ya Hisa, Liquidity, Volatility Na Markets Nature.Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kutokana na kuenea kwa elimu ya fedha, kwa sasa Watanzania wengi wamehamasika kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Cha kusikitisha ni kuwa wawekezaji wanakwama kwa stockbrokers ambao ndio wanahusika kumnunulia au kumuuzia hisa mwekezaji. Kwa sasa mitandaoni kuna malalamiko mbalimbali kuhusu madalali hao kuwa na huduma mbovu, kutojibu malalamiko ya wateja n.k.
Kwenye soko la hisa, muda ni zaidi ya mali. Dalali akikuchelewesha hata siku moja tu tayari ni hasara kubwa kwa sababu bei ya hisa inabadilika kila siku, na kwa soko la hisa la Dar es Salaam bei ya hisa ni kama inapaa kadri siku zinavyozidi kwenda.
Hivyo basi, tupeane uzoefu: dalali gani ana huduma nzuri na yupi ana huduma mbaya. Ili wawekezaji wanaosumbuka na madalali wabaya wawahame, kwa sababu inakera sana.
Mi naanza na dalali wangu msumbufu anaitwa Orbit Securities Co Ltd. Simu hawapokei, meseji hawajibu; yaani ni kama vile mimi ninawalazimisha wanihudumie, tena wanihudumie bure.
Mwanzo hawakuwa hivi, lakini kwa sasa huu usumbufu umenifika kooni, lazima nihame.
Karibuni tusaidiane.
Unasema ni mzoefu wa hisa hadi nje na hujaanza leo alafu unataka broker aanze kutoa elimu kwa hawa wanunuaji wa laki laki?Mkuu,kama watu wanapiga simu kuulizia vitu vya ajabu,maana yake hao watu hawana elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu soko la hisa linafanyaje kazi na kipi wapige simu kwa broker kuulizia na kipi wasipige. Kwanini hao watu wasipewe elimu ya kutosha ili simu zisizo na umuhimu zipungue huko kwa brokers?
Kwanini suluhisho la matatizo liwe kuwaambia watu wasiwekeze? Watu wapewe elimu ya uwekezaji tena elimu sahihi. Mimi nakumbuka wakati naanza kuwekeza kuna swali nilikuwa najiuliza,nikamtafuta mtu ana shahada ya masuala ya kifedha na anafanya kazi taasisi kubwa tu hapa nchini ili anisaidie kupata majibu .Cha kushangaza akanijibu hajui chochote kuhusu hisa licha ya kwamba yeye anafanya kazi kwenye ile taasisi. Yaani ni maajabu. Nchi nyingine watoto wa sekondari wanafahamu kuhusu hisa,watoto wa sekondari.
Wenye mitaji midogo wafanye nini?Relax;
Do not take offence.All in all Usisahau kwamba SOKO la Hisa sio Get RICH QUICK SCHEME.Unajua kinachoendelea kwenye SOKO la HISA kwa sasa?Kama Hujua Pitia Stock nyingi zinazouzwa ni za Taasisi gani?Taasisi za Kifedha,Banks na Mutual Funds etc.Hakuna Hisa za Biashara naUzalishaji ambazo ziko Busy sokoni.Hisa ambazo ziko Busy sokoni ni za Taasisi za Kifedha.
Unaelewa effect yake katika Uchumi?
Wakuze Mitaji yao kwanzaWenye mitaji midogo wafanye nini?
Asee tofauti na nmb ,crdb ,tbl,tcc na dse ni kampuni gani nzurii ya kuwekeza yenye gawio nielezee na Nico kidogoWakuze Mitaji yao kwanza
Sema wachangiaji wachache sana ila yote kwa yote vijana tuwekeze hata kidogo tulichonacho tusikatishane tamaaMada nzur