Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
- Thread starter
- #41
Mkuu umejibu vyema,changamoto basi ni watu kukosa uelewa na elimu. Hakuna anaezaliwa anajua kitu duniani,vyote tunajifunza. Basi hata na mambo yanayohusu hisa tunaweza kujifunza kama tulivyojifunza mambo mengine.Kuna mabroker wana magroup ya whatsapp kule wawekezaji wanauliza maswali na kujibiana. Unless iwe shida ya broker mfano muda wa kupokea malipo umepitiliza, order hazijawa reflected n.k...
Nmejionea mengi kwenye hayo magroup, mtu kanunua hisa anatala kuuza anaulizwa broker wako nani anasema sijui mimi huwa nanunua tu🤔 kuna watu wanapiga kampeni ya kupandisha hisa eti tuipandishe week hii tuuze... serious....
Kurudi kwenye point yako.
Ili kuanza kununua hisa inabidi kupata ABc ya kile unaenda kufanya. Sasa kwa kuwa sasa hv kujiunga na soko ni rahisi watu wanajiunga kiholela then ndio wanatafuta elimu. Kwa siku unakuta broker anapokea wateja wapya 500. Je wanawekeza nini? Kumbuka ili broker aboreshe huduma inahitaji apate commission za kutosha. Can you imagine unahudumia watu mia 5 na commision hawaleti hata milioni kwa mwezi. Wataweza kuupgrade huduma kweli au ndio watajibana pale pale kwa uwezo wao....
Pia tujitahidi kujua staff wawili watatu wa broker hii huwa inasaidia sana kutatua ishu ambazo customer care wanakua busy sana...
All in all tuwekeze na tutafute elimu hata chatgpt
Kama mwanafunzi wa darasa la kwanza anafahamu kwamba kuokota kiwembe barabarani kunaweza kusababisha maambukizi ya VVU, basi hakuna sababu kwanini mwanafunzi wa chuo kikuu hajui chochote kuhusu DSE. Elimu ya hisa itolewe kwa wingi, watu wakipata ufahamu tutasaidia kupunguza hayo matatizo wanayokutana nayo brokers. Sisi wenye ufahamu tujitahidi kusambaza elimu kwa wengine kadri tutakavyoweza, DSE pia wasambaze elimu kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii etc. Tusaidie umma uelimike kuhusu masuala ya uwekezaji. Shukrani