Tuambizane: Madalali (stock brokers) wa Soko la Hisa Dar (DSE) ambao wanafaa na wasiofaa

Mkuu umejibu vyema,changamoto basi ni watu kukosa uelewa na elimu. Hakuna anaezaliwa anajua kitu duniani,vyote tunajifunza. Basi hata na mambo yanayohusu hisa tunaweza kujifunza kama tulivyojifunza mambo mengine.
Kama mwanafunzi wa darasa la kwanza anafahamu kwamba kuokota kiwembe barabarani kunaweza kusababisha maambukizi ya VVU, basi hakuna sababu kwanini mwanafunzi wa chuo kikuu hajui chochote kuhusu DSE. Elimu ya hisa itolewe kwa wingi, watu wakipata ufahamu tutasaidia kupunguza hayo matatizo wanayokutana nayo brokers. Sisi wenye ufahamu tujitahidi kusambaza elimu kwa wengine kadri tutakavyoweza, DSE pia wasambaze elimu kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii etc. Tusaidie umma uelimike kuhusu masuala ya uwekezaji. Shukrani
 
Ndugu yangu;
Kwanza sijasema kwamba Ubaguliwe.Ila katika soko la hisa nguvu ya mtaji wako Ndio kila kitu.Ili wewe uweze kuuza hisa zako ni lazima kuwa na mnunuzi.Sasa imagine wewe unataka kununua Hisa za Milioni 1 halafu kuna mimi nataka kununua hisa za Milioni 500..Hivi unafikiri Broker Priority yake aweke kwenye kutafuta hisa kwa ajili yako au kwa ajili ya huyo wa 500?

Obviously Broker ataumiza kichwa kwa ajili ya huyu wa Milioni 500.Tena kwa Taarifa yako kuna wakati Broker inabidi sasa asisubiri tu mpaka mtu aweke Hisa sokoni bali anaenda Tafuta DON mmoja ambaye ana UKWASI labda wa BILIONI TANO ambazo zimefungiwa kwenye STOCK fulani anamshauri adiversify kidgo.So yule Kibopa anatoa HISA zake kidogo za milioni 500 zinawekwa sokoni Tajiri mpya anaingiza Mpunga sokoni na Yule wa Zamani anapokea Cash an akiamu Sehemu ya Hio Pesa anamwambia Broker amtafutie TENA HISA za Kampuni nyingine kadhaa.

SO ukiwa na mtaji mdogo kwenye SOKO la hisa usitaki kuhurumiwa.SOKO halinaga HURUMA Demand and SUPPLY ndio inafanya kazi na sio huruma na AIBU.

AS a mater of fact subirini SIKU soko letu la HISA likicrash ndo mtaelewa kwa sasa Hamtaelewa.Mnakumbuka ISSUE ya DESI ilivyokuwa?Basi mkiingia kwenye SOKO la HISA kama DESI msishangae siku mkaingia kwenye APP ys DSEE mkajikuta na LUNDO ya HISA zisizokuwa na Thamani.

SOKO la HISA ni PLAY GROUND YA MATAJIRI NA RISK TAKERS na sio watu ambao wamezoe kucheza kokoro la mchina,kubet au kucheza UPATU.
 
Broker wako ni mzuri sana sema sasa watu kama wewe mmekuwa wengi.Watu ambao mkishaweka Sell Order mnataka muone Pesa kwenye Account na mkiweka Buy Order mnataka muone Hisa kwenye Holdings zako.

Hamna Subira,Hamna Uzoefu,Hamna Patience na mbaya zaidi mnapenda sana kupost Mitandaoni.

Unataka Sasa Brokers waanzishe Call centre kama ya VODA au TIGO kwa ajili ya kupokea simu yako na kukwambia kwamba Muamala wako unafanyiwa kazi?Anyway Endelea kujifunza ukishaanza kuwekeza Bilioni Moja hutakuwa hata na muda wa kupiga simu kwa Broker badala yake Broker atakuwa ankupigia simu na kukukumbusha amba uuze au ununue kulingana na hali ya soko
 
Kwamba wewe ushauri wako unautoa vijiweni na kwenye Magroup ya whatsapp kisha unaenda DSE app unaweka BUY order ya HISa 10 za NMB hisa 10 za Voda,Hisa 10 za CRDB hisa 10 za Tatepa kisha unasema nimefanya Diversification na leverage.Then baada ya kama Mwezi unasikia hisa za Mwalimu Benk unauza za Voda unanunua za mwalimu?Anyways wewe kama unafikiri Broker haweza kukushauri basi elewa tu kwamba unamiss Fursa ya Muhimu sana.Ushauri wangu kwako ni Huu.Ukwasi wako ukifika sehemu nzuri basi Jitahidi Uende ukatembelee ofisi ya Broker wako ili upate touch ya watu ambao wanasimamia Pesa zako.

Kwanza fahamu kwamba Broker kuna wakati anakuwa na Access ya kufahamu Uelekeo wa SOKO kabla hata Public haijafahamu na ukiwa na ukaribu naye na ukawa na UKWASI unaoeleweka Basi ujue Fursa zitakufuata.
 
Mkuu ,una uhakika nikipiga simu huwa namuuliza nini broker?Ni hivi, mimi nikiweka order ya kununua hisa huwa nakaa kusubiri notification kwamba hisa zimeshanunuliwa. Sijawahi kupiga simu kuulizia kuhusu kama order niliyoweka hisa zimenunuliwa au lah. Mimi hadi nampigia simu broker ni changamoto kubwa na hawa brokers wanaofanya kazi hapo kwao ni binadamu. Sometimes kuna vitu wanasahau vya muhimu lazima upige simu uulizie ndo wanasema sorry tulisahau wanarekebisha. Sasa wasipokupokelea simu inaweza ikawa kuna jambo wamesahau linakwamisha mambo yako. Swali langu ni, " kwanini simu yangu haipokelewi,kwanini meseji hazijibiwi",tena sio mara moja wala mara mbili.
 
Yah elimu ni muhimu. Ukitumia muda mwingi kuelimisha jamii au wateja malalamiko yanapungua.
Hata mbuyu ulianza kama mchicha....

Kuna msemo wa watu wa huko duniani.

Anasema "ukinipa saa limoja kukata mbuyu kwa shoka, basi nitatumia dakika 45 kunoa shoka na dakika 15 kukata mbuyu"...

Pia tambua ukiona fursa inatangazwa sana fahamu wewe ndio fursa....
Kaa kitaalamu na hizi PR....
 
Mkuu, una uhakika mimi nikiweka order nataka nione hela kwenye account? Are you sure? Plus unasema sina uzoefu are you sure mi nimeanza kuwekeza lini kwenye soko la hisa la DSE? Sina patience, mkuu unajua mwenendo wangu wa uuzaji na ununuaji hisa hadi useme sina patience? Mpaka nimelileta hili suala hapa jukwaani, it is too much. Imevuka viwango vya ubinadamu. Just because you have more money than me,haikupi wewe haki ya kunidharau na kunidowngrade wakati hata sura yangu huifahamu
 
Mkuu ushaw
Mkuu ushawahi kunikuta kwenye kijiwe kipi? Ushawahi kunikuta kwenye group lipi la whatsapp ? Maisha yangu ya uwekezaji unayajua? Okay tuishie hapa, you have more money than me,nimekubali ,sitajibu ujumbe wako mwingine coz naona wewe ni aina ya watu ambao mnawadharau hata wale msiowajua kwa sababu accounts zenu zina billlions. Hata sisi tutafika mlipo nyie. Good luck
 
Sasa mkuu wote tutaweza kuwa na bilioni kweli? Kama wanakua hawajali wateja wa buku buku si waweke limit tu.

Ukishakubali hela ya mteja mhudumie ila sio kusema hela yake ndogo. Inawezekana ana tatzo la msingi linahitaji suluhisho.
Halafu tambua ili mtu kujiamini kuweka hela nyingi inabidi again trust...

Honestly mimi sikuwahi patiwa elimu ya hisa. Niliaambiwa nianze ila nilisita nikaanza na UTT ila baadae nikajiuliza kama UTT wanawekeza kwenye hisa why mimi nisiwekeze? Nikaanza kutest mdogo mdogo mpaka nikajiamini na kuanza kuweka hela nyingi. Sasa kama broker wangu angenikatia tamaa nisingeweka hela....

Ambacho nadhani tonatofautiana ni malengo. Mfano mimi sina hata wazo la kuuza na sijui hata kuuza mwaka wa tatu huu. Wengine wao ni ma trader, anaingia na kutoka na hawa ndio wanachangamsha soko. Sisi wazee wa kuhold tuna sunya tu. Ila ndio tabia ya soko inameza wote trader na investor....

Sasa hivi tuna wazee wa kubet kabsa kwenye hisa hajui hata kuna makato ya asilimia 2.34 akiuza wala akinunua yeye hasomi akiona imepanda anauza ikishuka anauza. Mtu anataka hisa zimpe hela ya kula tu....

Going forward DSE waongeze kiwango cha kiwango cha hisa kinachoweza kubadili bei ya soko, now ni hisa 100 nadhani wangeweka hisa 500 mpaka 1000 ili bei ibadilike....
 
Unaweza ukawa sahihi haya mambo ya hisa ni ya kisomi sana mimi siyajui lakini kuna wimbi kubwa sana la content creators kushawishi watu kuwekeza.

Wanasema unaweza kuanza kidogo na ukichelewa utapoteza faida. Wanatengeneza hofu.

Inaweza ikawa ni madalali wamefanya njama au makampuni yenyewe au wawekezaji wakubwa ila mkuu sioni kama wawekezaji wadogo wana cha kulaumiwa hapa.
 
Mkuu umejibu vyema. Shukrani. Hata mimi sio mtu wa kuuza hisa ,nahold kwa muda mrefu kadri nitakavyoweza. Lakini uwekezaji wa DSE umebadili maisha yangu kwa sababu ulinifanya nibadili mtazamo wangu kuhusu pesa,huko kubadili mtazamo kulinisaidia hadi kipato changu kikakua. Uwekezaji ulinifanya nikawa mtu mwingine kabisa,kuna mabadiliko kwenye maisha yalitokea. Kama ningesubiri niwe na mamilioni basi ile transformation ya maisha niliyoipata hadi leo nisingekuwa nimeipata. Nikitazama mbali ,naona nilichelewa kuanza.
 
Relax;
Do not take offence.All in all Usisahau kwamba SOKO la Hisa sio Get RICH QUICK SCHEME.Unajua kinachoendelea kwenye SOKO la HISA kwa sasa?Kama Hujua Pitia Stock nyingi zinazouzwa ni za Taasisi gani?Taasisi za Kifedha,Banks na Mutual Funds etc.Hakuna Hisa za Biashara naUzalishaji ambazo ziko Busy sokoni.Hisa ambazo ziko Busy sokoni ni za Taasisi za Kifedha.

Unaelewa effect yake katika Uchumi?
 
Tuelimishe mkuu hata kwa juu juu....
 
Hizi elimu tumechelewa kuzipata sana. Ila ndio hivyo kuna wakati sahii kwa kila jambo. Muhimu tuendelee kujifunza kila uchao na kuchukua tahadhari....
 
Hii kitu hata stock exchange kubwa za duniani ipo inaitwa speculation na haiepukiki hata leo hii makampuni kama apple yapo overvalued kwa sababu kama hizi.

Ki msingi hoja ya mtoa mada yahusu huduma mbovu za brokers, kwa upande wangu naona wanashindwa ku catch up na matumizi ya technology ndo maana huduma zao mbovu. Regardless mtu ananunua hisa za elfu hamsini au milioni hamsini order yake inatakiwa iwe executed kwa wakati na akihitaji customer service apewe kwa wakati FullStop.
 
Tuelimishe mkuu hata kwa juu juu....
Well
Elimu yangu ni Simple.Kwenye Hisa kama mtaji wako ni mdogo nunua HISa kwa ajili ya kuhudhuria AGM yaani vhisa vichache halafu unavisahau ikifika wakati wa AGM unaenda unafanya Networking ili ufahamiane na watu hasa hizi face to face AGM zinazofanyika UKUMBINI.

Kama lengo lako ni kutengeneza Portfolio nzuri Anza na UNITS kama za UTT au Similar Mutual Funds Wekeza kule kidogo kidogo mpaka ufikishe kiwango kizuri cha Fedha kisha sasa ndo uanze kuwekeza kwenye STOCKS.

Ukitaka kuingia kwenye STOCKS hakikisha unafahamu namna ya kusoma Taarifa za Fedha,namna ya kufuatilia hali ya uchumi na namna ya kufanya manunuzi ya HISa.Usifanye Impulse Buying or Selling.

Mwisho Brokers wote wanafanya kazi sawa.Wanasimamiwa na sheria zinazofanana na wanawajibishwa na mamlaka ya usimamizi wa mitaji CMSA.Kama Broker ana violations fulani basi sehemu sahihi ya kufikisha Taarifa ni CMSA ili wao wamsimamie na kumuwajibisha.

Mwisho ila sio kwa Umuhimu.Kabla haujaanza kukimbizana na Hisa Hakikisha Una cashflow ya kueleweka maana hisa sio kwa ajili ya akiba akiba huwa inakaa Benki.

Vile vile kama unamiliki hisi zenye thamani ya kueleweka hakikisha unazipeleka Benki,Unachukulia Mkopo na Hizo zako ziwe Dhamana.Hiyo inakusaidia sana kufaidikia hasa hisa zinapopanda na kushuka Bei.

Kwa mfano kama Una Hisa zenye Thamani ya Milioni 100,unaenda Benki unachukua mkopo wa Milioni 50 unaweka kwenye Biashara zako nyingine unawapa Share Certificates kama Dhamana yako.

Cha muhimu katika Hizi biashara za Hisa ni kuwa na Proper Planning kwani kufilisika na kutajirika ni mara moja.

Ni muhimu Pia ukafuatila INDICES za soko la HISA huwa zinakupa Picha ya Hali ya SOKO na uelekeo wa soko.Fuatilia hasa DSE Index ambazo zinatangazwa mara kwa mara
 
Speculation ni tofauti na impulse Buying.Kinachoendela katika Stock market ya Tanzania nia Impulse Buying ambayo ina create demand ambayo hata Speculators wenye hawaelewi elewi.Speculators huwa wanafanya Data analysis na kutengeneza Basis kwamba kutokana na A,B & C kuna uwezekana Hisa za Kampuni X zikapanda Bei kwa kipindi cha Mwezi mmoja ujao.So wakishaweka Dat Vizuri wananua Hisa kisha zikifika ile Bei wanayotaka wanauza.Hawakai nazo.Sasa impulse Buyers wanavurugaga SOKO kiasi kwamba wnafanya watu wa cash out Mapema hali ambayo inapelekea soko lina Slump. Ndio maana huwa kuna neno wanatumia wanasema Sophisticated Investors ambao wanaangalia aspects nying kabisa za soko.

All in All nakubaliana na ww kwamba Brokers ni watoa huduma na wanaowajibu wa kutoa huduma bora.
 
Mkuu uko njema kwenye maswala ya hisa,Sasa unatushauri nin sisi wenye vimitaji vya 100m tunaotaka kuwekeza kwenye hisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…