Tuambizane: Madalali (stock brokers) wa Soko la Hisa Dar (DSE) ambao wanafaa na wasiofaa

Umeongea ukweli na ikitokea wawekezaji wakubwa wakaamua kuuza hisa zao tutakimbiana..!!

Huu mnyukano wa mabondia wawili unachangiwa na watu wasiolewa vizuri maana ya uwekezaji wanakurupuka kwa kununua hisa hovyo..!!
 
Kiwan kiwango kizuri chakuwekeza kwenye stock ni kiasi gani labda tupe elimu
 
Kiwankiwango kizuri chakuwekeza kwenye stock ni kiasi gani labda tupe elimu
Kiwango kinategemea na Ukwasi wako.

Kama nilivyosema SOKO la Hisa ni soko la Mitaji.Kimsingi Kwenye soko la mitaji unaenda na mtaji wako ambao unataka kuuwekeza.Sasa swala la kujiuliza Je unapoenda SOKO la Hisa na 50,000 Je ni Mtaji?Kimsingi 50,000 kwenda nayo kwenye soko la hisa sio mtaji substancial ingawa bado unaweza fanya manunuzi.

Unaweza wekeza kiwango chochote ila kwa soko la la Dar es Salaama Anza na Milioni 50 kwanza.Lenga ama hisa ambazo ni kongwe na imara sokoni au hisa ambazo bei yake iko chini ila biashara ina performance nzuri.

Unaweza hata changanya changanya.

Milioni 50 haikufanyi uwe mwekezaji mkubwa ila inakufanya uwe na uwezo wa kufikiri vyema katika uwekezaji na kuwa makini.Ila ili ufurahia matunda ya SOKO la HISA kama una Milioni 200 ukazitupia Humo na kuzipanga vizuri usishangae Ndani ya muda mfupi ukavuna Bilioni hasa ukifuma hisa nyepesi kupanda.
 
Wengi Mnaingia kwa mihemko katika Uwekezaji huu Bongo. Hamna Elimu sahihi juu ya Hisa, Liquidity, Volatility Na Markets Nature.

TZ Sock Market Hakuna Liquidity ya kutosha, Mifumo bado ya kizamani, na Volatility Ndogo.
Ndio maana ni ngumu kuuza hisa Hapa bongo cz Market players wachache, mpk usubiri. Pia Movements za Soko huwezi kuziona in Real time data driven technology.

Wakati Ukiwa Hapa hapa Bongo Unaweza kununua Hisa za makampuni ya nje kwa simu tu ktk Masoko ya Ulaya, bila kwenda ofisini utaweza ku comply na vigezo vyote.

Utanunua Hisa katika masoko yenye Volatility na Liquidity Kubwa kiasi kwamba ukitaka kuuza utapata fedha chap au kununua ni mda wowote ule chap unafanya transactions.

Mnauziwa Matumaini ili muingie wengi kununua hisa ili soko like ni vzr lkn bado Technicality na Transparency hkn.
 
Unasema ni mzoefu wa hisa hadi nje na hujaanza leo alafu unataka broker aanze kutoa elimu kwa hawa wanunuaji wa laki laki?

Huyo broker ana wafanyakazi elfu ngapi sasa, kazi anafanya muda gani, order anaweka lini, anauza na kununua lini, unamlipa kiasi gani?
Yani taratibu za kubeti uko ndio mnaleta DSE mwingine anasema anampigia broker saa tano za usiku.

Uliwahi enda ofisi ya broker ukaona ana staff wangapi? Huu mwitikio wa mwaka huu kila siku mamia wanajiunga sasa broker afundisheje.
 
Napendekeza Victoria financial services Ltd. Ni broker poa.
Wanaweza kuwa na changamoto zingine lakini mimi zisifaham.
Lakini hizi ni strengths zao.
1. Mawasiliano mpaka weekend, unaweza kuwapigia simu au kuchat nao WATSAPP
2. Order inakuwa processed instantly iikiwa tu ni masaa ya kazi.
3. Ukisell bada ya 72 hours watakupigia simu.
Sijutii kuwatumia.
Nb: hii sio promo natoa experience yangu.
 
Wenye mitaji midogo wafanye nini?
 
Kitu kizuri kipo hapa.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…