Hivi kweli kuna haja ya kuamsha mizimu iliyolala ili ipate kutusaidia?
Yaani tumeshindwa kujisaidia mpaka tunaomba msaada kwa visivyojiweza! Ama kweli tumesoma lakini hatujaelimika, sisi wenyewe hatujui nini tunataka, hatujui nini tatizo letu, hatujui nini suluhisho la matatizo yetu, hatuthamini uwezo wetu tuliyokuwa nao, hatujiamini kabisa na hatujui nini lengo na kusudio la maendeleo yetu. Na hakuna wa kutusaidia isipokuwa ni sisi wenyewe. Imani ya dini haihusiani na maendeleo, kwani wahindi wanaabudu ng'ombe lakini wamepiga hatua kimaendeleo, wachina wanaabudu miungu yao nao wamepiga hatua, wazungu nao wengi wakristo nao wamepiga hatua, wayahudi nao wana imani zao nao wamepiga hatua, waarabu nao wengi ni waislamu wamepiga hatua, sisi waafrika ndiyo wenye matatizo, ikiwa hatuwezi kupiga hatua katika maendeleo ya uchumi na viwanda basi japokuwa tuweze kujitosheleza kwa chakula kutokana na ardhi kubwa na yenye rutuba tuliyonayo, hata hivyo utasikia baadhi ya nchi za Afrika zina ukame.
Na hivi bado kuna watu wanaofikiria mizimu kwenye karne hii sayansi na teknolojia?