hahaha fantasia bwana"" ..nadhani wajua kuwa MJ alibadilisha muonekano wa ngozi yake " baada ya kuugua ugonjwa wa vitiligo "" ...!?
Michael Jackson (29 Agosti 1958 – 25 Juni 2009) alikuwa mwanamuziki na mburudishaji wa Kimarekani ambaye ametumia zaidi ya miaka arobaini katika jicho la umma, kwanza akiwa kama nyota mtoto akiwa na kundi zima la
The Jackson 5, kishaa badaaye kama msanii wa kujitegemea. Kuanzia katikati mwa miaka ya 1980 imekuwa wazi kwamba mwonekano wa Jackson ulikuwa unabadilika bila kificho. Ngozi ya mwili wake imeanza kupauka, pua na umbo la sura yake imebadilika, na kapoteza uzito.
Ile hali ya mpauko wa ngozi awali ulisababishwa na
vitiligo na
lupus (ugonjwa wa ngozi ambao tiba yake ni tata) — ambao Jackson alijaribu kuutibia kunako mwaka wa 1986—na matumizi yake ya vipodozi mbalimbali ili kuficha madoa yake ya mwilini.
[1]Baadhi ya madaktari wa upasuaji wamekisia ya kwamba pia alifanya "rhinoplasty" (upasuaji wa pua), kuinua paji la uso, upasuaji na usawazishaji wa kidevu, na kabadilisha vilevile midomo yake.
[2] Hayo yote ya karibu yanakadiliwa kufanywa na mwimbaji huyo kunako miaka ya 1990, amepitia karibia michakato kumi ya kubadili umbo lake.
[1]
Jackson na baadhi ya ndugu zake walisema ya kwamba walikuwa wakinyanyasika sana kimwili na kihisia na baba yao, na mwaka wa 2003, alikubali kwamba alikuwa akimchapa viboko sana Jackson wakati yu mtoto.
[3]Jackson hapendi kabisa kulizungumzia hili, lakini pindi tu anapolisema, anakuwa na huzuni sana na kusema ya kwamba angetapika kabla ya kukutana na baba'ke. Madaktari wanasema alikuwa na matatizo ya maumivu ya mwili.
Deepak Chopra, daktari na rafiki wa karibu Jackson kwa karibia miaka 20, amesema: "Kilichokuwa shurutisho kwake ni hali ya kufanya upasuaji uliokuwa a hali ya kujibalisha mwenyewe, hali ambayo dhahiri ni kutojiheshimu au kujikubali wewe kama wewe."
[4]
Wakati fulani katika miaka ya 1990, ilionekana ya kwamba Jackson amekuwa tegemezi kubwa la madawa mbalimbali, hasa dawa za kuua maumivu na na vipoozeo vikalivikali, na afya yake ikaanza kuyumba waziwazi. Ameenda kujiswafi kunako mwaka wa 1993 kwa msaada wa
Elizabeth Taylorna
Elton John,
[5] lakini ulevi wa dawa ulibaki palepale.
Amefariki kwa mshtuko wa moyo kunako tar.
25 Juni 2009.