Tuchanane: Mambo ambayo akifanya mtu aibu unaona wewe!

Tuchanane: Mambo ambayo akifanya mtu aibu unaona wewe!

Tobito

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,308
Reaction score
4,165
Binadam alivyo leo kitabia na mwenendo ni zao la mambo 3.
1. Jenetiki alizorithi
2. Mazingira aliyokulia
3. Mazingira aliyomo.
Tunakutana ukubwan, si vibaya tuambizane mambo yanayotia kinyaa kwenye jamii.(general bad manners).
Haijalishi kwa makusudi au bahati mbaya.
1. Kuongea na simu sauti ya juu mambo yako ya faragha.
2. Kupenga kamasi bila leso.
3. Kula unatoa milio ya kutafuna.
4. Kutamka sehem za siri mbele ya watoto.
5. Kuongelea staili za ngono za mwenza.
6. Kumtukana uliyemtongoza akakataa.
7. Kupeleka sheria mpya kwenye mji wa mtu.
8. Kusalimia kwa kurejea dini za wahusika na si imani yako.
9. Kurukia folen sehem za huduma.
10. Kuongea kilugha na mko na asiyekijua.
11. Kumhusisha mwanao kwenye harakati za mapenzi yako.
12. .....Endelea
 
Mtu anakunywa chai,sasa anapovuta inasikika sauti hadi aibu huwa naona mimi ,

Kupaka bleach kwenye ndevu,hii kwangu ni No

Kunywa uji ulio kwenye kikombe kisha kwakuwa unaisha kutia kidole cha shahada kuukombelezea
Hiyo ya breach za ndevu kuna waumini flan ni ibada ili majini yakutii kuleta riziki au ulinzi.
 
Back
Top Bottom