Tuheshimu Katiba. Uchaguzi Mkuu ufanyike 2026

Kwa mujibu wa katiba yetu na sheria za uchaguzi, Samia atagombea urais mwaka 2025, huo ndio utakuwa uchaguzi wake wa mwisho kugombea urais kwa mujibu wa katiba hii, kugombea tena 2030 kwa katiba hii hawezi, labda abadilishe katiba.

Hata hili jambo lililowekwa wazi kwenye katiba hulijui?
RAIS SAMIA anaongoza awamu ya NGAPI? Kuna awamu ya miaka minne then mitano? Hivi lojiki yangu inaeleweka? Ya 2026?
 
Hivi Magufuli angefariki desemba mwaka huu naye Samia akaapishwa kuwa Rais mpaka Oktoba mwakani angekuwa Rais wa Awamu ya ngapi?
 
Wajumbe, aliyekuwa Rais wa JMT Dk. John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17/3/2021 hapo Mzena kisha Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo chake saa 5:57 usiku "akiwa ziarani Tanga".

Baada ya hapo aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitawazwa kuwa Rais wa JMT. Katiba yetu inaelekeza kuwa Rais atakuwa madarakani kwa miaka 5 (si minne wala sita) na kama atataka kugombea tena kwa awamu ya pili na ya mwisho basi ataomba ridhaa kwa chama chake.

Katiba imeweka bayana kuwa Rais ataacha Urais kwa (1) kufariki
(2) Kuumwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake na (3) kwa kujiuzulu. Katiba haisemi kwamba Rais akipatwa na hayo matatu let's say ndani ya miaka minne basi atakayemrithi atamalizia awamu yake (marehemu).

Naamini hii ndiyo maana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umetambuliwa kama Awamu ya Sita na si ya Tano. Kama ni hivyo basi, tutakuwa hatujamtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan endapo tutafanya uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani Jumapili ya mwisho maana haitokidhi matakwa ya Katiba ya miaka mitano madarakani.

Kwa hiyo tuheshimu Katiba na haki ya Samia tufanye uchaguzi mwezi machi 2026 siku aliyoapishwa. Ova!
🤔💭 📝
 
Mkuu umevamia fani. Waachie waliolipa ada na kukaa darasani wakaisoma constitutional law
Nimecheka sana. Umemaliza. Eti Rais wa dharura anataka kutungiwa sheria afanane na Rais wa kuchaguliwa kwa ballot box. Haiwezekani.
 
RAIS SAMIA anaongoza awamu ya NGAPI? Kuna awamu ya miaka minne then mitano? Hivi lojiki yangu inaeleweka? Ya 2026?
Haieleweki mkuuu.

Katiba inaeleza wazi, ikitokea raisi amefariki akiwa madarakani, makamu wake ataapishwa kua raisi na kumalizia siku zilizo baki b4 uchaguzi mkuu, so hata kama imebaki miezi 3
 
Wajumbe, aliyekuwa Rais wa JMT Dk. John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17/3/2021 hapo Mzena kisha Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo chake saa 5:57 usiku "akiwa ziarani Tanga".

Baada ya hapo aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitawazwa kuwa Rais wa JMT. Katiba yetu inaelekeza kuwa Rais atakuwa madarakani kwa miaka 5 (si minne wala sita) na kama atataka kugombea tena kwa awamu ya pili na ya mwisho basi ataomba ridhaa kwa chama chake.

Katiba imeweka bayana kuwa Rais ataacha Urais kwa (1) kufariki
(2) Kuumwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake na (3) kwa kujiuzulu. Katiba haisemi kwamba Rais akipatwa na hayo matatu let's say ndani ya miaka minne basi atakayemrithi atamalizia awamu yake (marehemu).

Naamini hii ndiyo maana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umetambuliwa kama Awamu ya Sita na si ya Tano. Kama ni hivyo basi, tutakuwa hatujamtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan endapo tutafanya uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani Jumapili ya mwisho maana haitokidhi matakwa ya Katiba ya miaka mitano madarakani.

Kwa hiyo tuheshimu Katiba na haki ya Samia tufanye uchaguzi mwezi machi 2026 siku aliyoapishwa. Ova!
Hujui Katiba inasemaje; kaa chini usipige kelele uache sheria ifuate mkondo wake
 
RAIS SAMIA anaongoza awamu ya NGAPI? Kuna awamu ya miaka minne then mitano? Hivi lojiki yangu inaeleweka? Ya 2026?
Awamu imeandikwa wapi kwenye katiba?

Kwanza kabisa, tumalize mzozo wa Samia anaruhusiwa kugombea urais mara ngapi. Kwa kunukuu vifungu vya katiba.

Hii ibara ya 40 (4) ndiyo inamhusu Samia, rais aliyekuwa makamu wa rais awali na kuupata urais baada ya rais wa awali kufariki.

Nanukuu katiba

Ibara ya 40.

(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili , lakini kama akishika kiti cha urais Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.

Mwisho wa kunukuu katiba.

Samia Machi mwaka huu atakuwa kashika urais kwa miaka mitatu. Hivyo hataruhusiwa kugombea urais mara mbili.

Hilo tumemaliza, kwa kifungu cha katiba.

Kwenye miaka ya uchaguzi.

Alivyouawa Karume April 7 1972, Aboud Jumbe Mwinyi alikuja kuchukua urais.

Urais wa Zanzibar ni miaka mitano.

Uchaguzi uliofuata ulikuwa mwaka gani? 1975 au 1977? Ulikuwa mwaka 1975. Hatukusema Aboud Jumbe aendelee kwa miaka mitano kutoka 1972 mpaka 1977.

Kwa nini? Kwa sababu urais ni taasisi, si mtu.

Huu mfumo wa mgombea mwenza katika katiba ya Tanzania tumeutoa Marekani.

Marekani rais anakaa madarakani kwa miaka minne.

Rais Kennedy alichaguliwa mwaka 1960, kipindi chake kilikuwa kinaisha mwaka 1964. Kennedy aliuawa mwaka 1963. Makamu wake Johnson akachukua urais mwaka 1963. Kwa nini Johnson hakupewa urais miaka minne 1963 mpaka 1967, na uchaguzi wa mwaka 1964 ukabaki pale pale?

Kwa sababu urais ni taasisi, si mtu.

Vivyo hivyo, Samia atarudi kwenye uchaguzi mwaka 2025, kwa mara ya mwisho. Akikubaliwa na kudumu kwenye kiti atakuwa rais mpaka 2030. Na huo utakuwa mwisho wa urais wake kwa katiba ya sasa.
 
Wajumbe, aliyekuwa Rais wa JMT Dk. John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17/3/2021 hapo Mzena kisha Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo chake saa 5:57 usiku "akiwa ziarani Tanga".

Baada ya hapo aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitawazwa kuwa Rais wa JMT. Katiba yetu inaelekeza kuwa Rais atakuwa madarakani kwa miaka 5 (si minne wala sita) na kama atataka kugombea tena kwa awamu ya pili na ya mwisho basi ataomba ridhaa kwa chama chake.

Katiba imeweka bayana kuwa Rais ataacha Urais kwa (1) kufariki
(2) Kuumwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake na (3) kwa kujiuzulu. Katiba haisemi kwamba Rais akipatwa na hayo matatu let's say ndani ya miaka minne basi atakayemrithi atamalizia awamu yake (marehemu).

Naamini hii ndiyo maana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umetambuliwa kama Awamu ya Sita na si ya Tano. Kama ni hivyo basi, tutakuwa hatujamtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan endapo tutafanya uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani Jumapili ya mwisho maana haitokidhi matakwa ya Katiba ya miaka mitano madarakani.

Kwa hiyo tuheshimu Katiba na haki ya Samia tufanye uchaguzi mwezi machi 2026 siku aliyoapishwa. Ova!
Uchawa ukizidi utajiona wewe pekee ndiye mwenye busara nchini, hili ndilo tunashuhudia.
 
RAIS SAMIA anaongoza awamu ya NGAPI? Kuna awamu ya miaka minne then mitano? Hivi lojiki yangu inaeleweka? Ya m

Wajumbe, aliyekuwa Rais wa JMT Dk. John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17/3/2021 hapo Mzena kisha Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo chake saa 5:57 usiku "akiwa ziarani Tanga".

Baada ya hapo aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitawazwa kuwa Rais wa JMT. Katiba yetu inaelekeza kuwa Rais atakuwa madarakani kwa miaka 5 (si minne wala sita) na kama atataka kugombea tena kwa awamu ya pili na ya mwisho basi ataomba ridhaa kwa chama chake.

Katiba imeweka bayana kuwa Rais ataacha Urais kwa (1) kufariki
(2) Kuumwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake na (3) kwa kujiuzulu. Katiba haisemi kwamba Rais akipatwa na hayo matatu let's say ndani ya miaka minne basi atakayemrithi atamalizia awamu yake (marehemu).

Naamini hii ndiyo maana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umetambuliwa kama Awamu ya Sita na si ya Tano. Kama ni hivyo basi, tutakuwa hatujamtendea haki Rais Samia Suluhu Hassan endapo tutafanya uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani Jumapili ya mwisho maana haitokidhi matakwa ya Katiba ya miaka mitano madarakani.

Kwa hiyo tuheshimu Katiba na haki ya Samia tufanye uchaguzi mwezi machi 2026 siku aliyoapishwa. Ova!
Kwa kukusaidia soma Katiba Sura ya Pili Ibara ya 40 Ibara ndogo ya 4 kuhusu Rais akiondoka madarakani kwa sababu zilizoelezwa katika Ibara ya 37 Ibara ndogo ya 5. Hizo bangi zako za awamu achana nazo. Hakuna maelezo yoyote kuhusu awamu yameelezwa katika Katiba.
 
Urais wa Samia na Magufuli unaenda pamoja. Samia alikuwa ni backup wa Magufuli. Ndiyo maana alikuwa mgombea mwenza na kapigiwa kura kwenye uchaguzi wa rais kuwa makamu wa rais, ndiyo maana watu wanaosema Samia kawa rais bila kuchaguliwa hawana hoja.

Hivyo, kipindi ambacho Samia alichaguliwa kuwa makamu wa rais,na backup wa rais Magufuli atakayechukua urais Magufuli akifariki, kilianza 2020 na kinaisha 2025.

Hii dhana yako ni ndoto tu, uchaguzi utafanyika 2025.

Urais si mtu, urais ni taasisi.
Makamu wa rais hapigiwi kura na anaweza kuteuliwa siku yoyote, kumbuka makamu wa rais alipofariki nchi haikuingia kwenye uchaguzi bali aliteuliwa mwingine kushika nafasi yake.
Achana na upindishaji wa katiba unaofanywa na CCM.
 
Makamu wa Rais si lazima apigiwe kura, kwa sababu akifa Rais na Makamu wa Rais kuwa Rais, hatuhitaji uchaguzi mwingine kumpata Makamu wa Rais mwingine (kama ilivyokuwa kwa Philip Mpango), lakini, ukisema Makamu wa Rais hapigiwi kura unakosea.

Kwani Samia alipata kuwa Makamu wa Rais vipi? Unataka kusema Samia hakupigiwa kura kama mgombea mwenza wa Magufuli ili kuwa Makamu wa Rais?

Kifo cha Magufuli kimeanika ujinga mkubwa sana wa Watanzania wengi.

Watanzania wengi walikuwa wanafikiri kwamba, kwenye uchaguzi wa rais, wanampigia kura rais tu, huyu Makamu wa Rais ni kama mapambo tu.

Mara paap, Magufuli kafa. Ndiyo watu wakastuka, alaaa, kumbe tumempigia kura huyu Makamu wa Rais Samia aje kuwa rais siku yoyote Magufuli akifa?

Watu walifikiri kwenye uchaguzi wa Rais wanampigia Magufuli tu. Kwenye uchaguzi wa Rais unampigia kura Rais na Makamu wake, ndiyo maana anayekuwa Makamu wa Rais anaitwa "running mate", wale ni a packaged deal unawapigia kura wote pamoja, mmoja unampigia awe Rais, na mwingine awe Makamu wa Rais.

Unakubali kuwa akifa Rais, huyu Makamu wa Rais anakuwa Rais.

Na hapo ndipo mantiki ya uongozi wa Samia kuisha 2025 inapokuja. Samia alichaguliwa 2020, hakuchaguliwa 2021. Hakuna uchaguzi uliofanyika 2021, utataka vipi uchaguzi ufanyike 2026?

Hivyo, mandate ya kuchaguliwa kwake, ile power ya miaka mitano aliyopewa na watu, ina expire 2025, si 2026.

Watu wengi hawajasoma katiba, halafu ukiwaelezea katiba inavyosema, wanasema katiba inachosema ni kuvunja katiba.
 
Kwa kukusaidia soma Katiba Sura ya Pili Ibara ya 40 Ibara ndogo ya 4 kuhusu Rais akiondoka madarakani kwa sababu zilizoelezwa katika Ibara ya 37 Ibara ndogo ya 5. Hizo bangi zako za awamu achana nazo. Hakuna maelezo yoyote kuhusu awamu yameelezwa katika Katiba.
Post namba 33 nimemuwekea vifungu hivyo ajifunze katiba na abishe kwa kuweka vifungu vya katiba, si kwa kubwabwaja tu.
 
Kwa logic ya mtoa maada, nchi inaweza kwenda miaka hata 100 bila uchaguzi wa rais.

Siombei mtu afe, natoa mfano tu.

Magufuli kafa 2021, Samia Makamu wake achukue urais kwa miaka mitano mpaka 2026. Akae miaka mitano ya urais baada ya kifo cha Magufuli.

Bahati mbaya mwanzo hapo 2026 kabla miaka mitano haijafika, Samia naye kafa. Makamu wake Mpango anachukua nchi 2026 mpaka 2031 (bila uchaguzi). Anapewa miaka mitano yake.

2031 kabla Mpango hajafikisha miaka mitano ya urais wake, bahati mbaya sana Mpango naye kafa. Alikuwa kamchagua Makamu wake Makonda. Makonda anachukua urais mpaka 2036, bila uchaguzi.

2036 Makonda naye kapigwa na radi kafariki. Alikuwa kamchagua Makamu wake Sabaya. Sabaya anachukua urais mpaka 2041. Bila uchaguzi.

Nchi inaweza kuendelea hivyo hata miaka 100 bila uchaguzi.

Watu wenye werevu walishaona hilo ndiyo maana wakaweka miaka ya uchaguzi iwe fixed.
 
IMG_8869.jpg
 
Mkuu kwa nini twende mzobe mzobe kubaka Katiba?
Unapoweka madai ya "kubaka katiba", weka kifungu cha katiba na eleza kinabakwa vipi.

Nimekuonesha mfano wa kujenga hoja na kuitetea kwa vifungu vya katiba kwenye post namba 33 hapo juu. Nimenukuu ibara ya 40 (4) kukupa somo kwamba Samia anaruhusiwa kugombea urais mara moja tu.

Umeelewa na kukubali somo hilo la katiba?

Wewe unaitaja sana katiba lakini huweki nukuu za ibara za katiba tuzichambue.

Unaposema kubakwa katiba, unaongelea ibara gani, imebakwa vipi?
 
Back
Top Bottom