Awamu imeandikwa wapi kwenye katiba?
Kwanza kabisa, tumalize mzozo wa Samia anaruhusiwa kugombea urais mara ngapi. Kwa kunukuu vifungu vya katiba.
Hii ibara ya 40 (4) ndiyo inamhusu Samia, rais aliyekuwa makamu wa rais awali na kuupata urais baada ya rais wa awali kufariki.
Nanukuu katiba
Ibara ya 40.
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili , lakini kama akishika kiti cha urais Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Mwisho wa kunukuu katiba.
Samia Machi mwaka huu atakuwa kashika urais kwa miaka mitatu. Hivyo hataruhusiwa kugombea urais mara mbili.
Hilo tumemaliza, kwa kifungu cha katiba.
Kwenye miaka ya uchaguzi.
Alivyouawa Karume April 7 1972, Aboud Jumbe Mwinyi alikuja kuchukua urais.
Urais wa Zanzibar ni miaka mitano.
Uchaguzi uliofuata ulikuwa mwaka gani? 1975 au 1977? Ulikuwa mwaka 1975. Hatukusema Aboud Jumbe aendelee kwa miaka mitano kutoka 1972 mpaka 1977.
Kwa nini? Kwa sababu urais ni taasisi, si mtu.
Huu mfumo wa mgombea mwenza katika katiba ya Tanzania tumeutoa Marekani.
Marekani rais anakaa madarakani kwa miaka minne.
Rais Kennedy alichaguliwa mwaka 1960, kipindi chake kilikuwa kinaisha mwaka 1964. Kennedy aliuawa mwaka 1963. Makamu wake Johnson akachukua urais mwaka 1963. Kwa nini Johnson hakupewa urais miaka minne 1963 mpaka 1967, na uchaguzi wa mwaka 1964 ukabaki pale pale?
Kwa sababu urais ni taasisi, si mtu.
Vivyo hivyo, Samia atarudi kwenye uchaguzi mwaka 2025, kwa mara ya mwisho. Akikubaliwa na kudumu kwenye kiti atakuwa rais mpaka 2030. Na huo utakuwa mwisho wa urais wake kwa katiba ya sasa.