Tuheshimu Katiba. Uchaguzi Mkuu ufanyike 2026


Sasa kwa nini sa 100agombee tena wakati muda wao umeisha sa100 atakaa pembeni ccm tutapate mtu mwingine
 

mkuu umesoma katiba ya nchi au unaongea sauti unazozisikia kichwani kwako?

Rais akifariki na ikawa kifo kimetokea ndani ya miaka 3+ kabla ya miaka yake 5 basi mrithi anaapishwa na anahudumu hiyo miaka 3+ iliyobaki kwa kuhesabika amehudumu muhula mzima. Baada ya hapo anaruhusiwa kugombea muhula mmoja kukamilisha awamu yake aliyoianza baada ya kumrithi marehemu

Iwapo rais amefariki na kubakiza muda chini ya miaka mitatu yaani -3 basi anayerithi kijiti anaruhusiwa kugombea mara mbili kwa sababu katiba inasema anamalizia muda mchache uliosalia ili aanze awamu yake uchaguzi unaofuata na atagombea mihula miwili.

Mlipokuwa mnamalizana na Mwendazake mlipaswa kuzingatia muda uliowekwa Kikatiba....
 
Hizo AWAMU zipo kwenye katiba? au ni vitu tu vya kujitungia, yaani hilo neno AWAMU limeandikwa kwenye katiba kuwa AWAMU ya kwanza itakuwa hivi na hivi na yapili .......
Mambo ya awamu ni miongozo ya ccm, ambayo hayawahusu WaTz wote. Katiba inaongelea kipindi cha miaka mitano, bila ya kujali aliyechaguliwa yu hai ama mbadala wake unamalizia hicho kipindi
 
Mkuu;

Tafadhali kwanza, Kasome Katiba ya JMT ya mwaka 77, sura ya 2, sehemu yake ya 1, ibara ya 37 kufungu kidogo cha 5:

Ambacho kinazungumzia kumalizia awamu inayoendelea, kwa hapa Rais Samia anamalizia kipindi cha pili cha awamu ya 5! Kwa hapa sio awamu ya 6!

Pili, Kasome sura hiyo hiyo ya 2, ibara ya 40 kifungu kidogo cha 4 ambacho kina rejea ibara ya 37/5; Hapo, kinazungumzia ukomo wa awamu ya urais kwa Rais aliyepatikana kwa mujibu wa ibara ya 37/5:

Kwa hapa Rais Samia atachaguliwa kwa awamu moja tu maana mpaka mwaka wa 2025 atakuwa amehudumu kwa zaidi ya miaka 3 ya kipindi cha pili cha awamu Mwendazake!

Mkuu usipotoshe watu!
 
Huwezi kujificha, kosa la maudhui yanakuhusu. Kama hujui mabadiliko ya sheria ya mtandao hili unalo hata uwe Mbinguni tutakufikia ueleze maudhui Yako. Mwenzio aliyetumia ghost account humu Leo yuko Keko. Hauko salama udhaiavyo.
Usitishe watu
 
Samia aligombea Uwenza ili hatimaye aje kuwa Makamu wa Rais si Rais. Samia hamalizii Awamu ya Jiwe mbona hamuelewi? Kwa nini ni AWAMU YA SITA? JPM alitawala awamu ya ngapi?

Mbona kwenye kupiga kura kulikuwa na picha ya magufuri na samia ukiweka tiki kwa magufuri sawa ukiweka tiki kwa samia sawa saaa kwa nini asimalizie muda wa magufiuri halafu astaafu
 
Hoja yako siipingi...unataka kusema hata wabunge na madiwani ukomo wao uwe 2026 au kutakuwa na chaguzi 2 ktk kipindi Cha mwaka 1..Endelea kusoma vizuri uelewe.!
 
Samia aligombea Uwenza ili hatimaye aje kuwa Makamu wa Rais si Rais. Samia hamalizii Awamu ya Jiwe mbona hamuelewi? Kwa nini ni AWAMU YA SITA? JPM alitawala awamu ya ngapi?
Wewe katiba huijui na hujui kwamba rais akifariki makamu wa rais anashika kiti cha rais?

Hiyo katiba unayoitajataja umeisoma?

Unaelewa mtu akiwa mgombea mwenza anakuwa makamu wa rais na makamu wa rais anakuwa rais wakati wowote rais akifariki?
 
Awamu ni maneno ya kisiasa unaweza kutunga vyovyote, unaweza hata kusema awamu ya tano na nusu, si jambo la kisheria wala kikatiba.

Katiba haina neno awamu.
👍🤝👏🙏
 
Alishasema kuwa Katiba sio Msaafu, so Acha kuamini upumbavu
 
Wewe katiba huijui na hujui kwamba rais akifariki makamu wa rais anashika kiti cha rais?

Hiyo katiba unayoitajataja umeisoma?

Unaeleea mtu akiwa mgombea mwenza anakuwa makamubwa rais na makamu wa rais anakuwa rais wakati wowote rais akifariki?
Hahahaha wakajipange upya kwa kweli
 
Hahahaha wakajipange upya kwa kweli
Mtu anatajataja katiba katiba, katiba katiba.

Hajaweka hata ibara moja anayoisema tuichambue.

Anakwambia katiba inabakwa.

Unamuuliza, inabakwa vipi, ibara gani?

Anakimbia hata hajibu.

Hata yeye mwenyewe hajui ibara gani anaiongelea, anakurupuka tu kwa hisia, inaonekana hata kuisoma hiyo katiba hajaisoma.
 
Soma tena vizuri katiba kwa kuangazia ibara ya 40 kifungu kidogo cha 4.
Uchaguzi mkuu ni 2025 kwa mujibu wa kifungu hicho. Pia, Rais Dr Samia akigombea 2025 na kushinda, hataruhusiwa tena kikatiba kugombea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…