Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

MTOTO KITAA,

Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela". Hoja ya " kwanini kusiwe na ukomo" si ya la Dr Slaa. Waulizwe watunga Katiba Mkutano Mkuu.

Nadhani tusipandikize hoja juu ya hoja, hatutapata majibu fasaha, tutabaki kukisia, kutoa tafsiri mbalimbali kwa maonjo ya kila mmoja. Nilichojibu ni kile ambacho kiko ndani ya mamlaka ya Katibu Mkuu. Hata hivyo, Katiba ya Chadema inatoa fursa, kwa kila mwanachama, kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba kwa utaratibu unaotolewa na Katiba yenyewe.

Kama kuna mtu anafikiria kuna hoja hiyo, hajachelewa awasilishe pendekezo ipitie vikao vya mabadiliko ya Katiba, na Kama vikao vitaridhia, mabadiliko yatafanyika, nadhani ndiyo demokrasia. Demokrasia siyo kile ambacho mtu mmoja mmoja anakifikiria!
Slaa sisi hatujalishwa unga wa ndere. Je kwanini kusiwe na ukomo wa uongoz? Je hii ndio demokrasia mnayopigia kerere kila siku? Slaa kumbuka sisi sio mazombi. Na ujipange uje utoe majibu sahii hapa sisi hatuna zidumu fikra...................
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco.

Umeuliza maswali ya ujenzi lakini bahati mbaya hayana majibu stahiki.
 
Last edited by a moderator:
Mwenye jukumu la kutoa ushahidi wa vinginevyo ni mtuhumiwa!, mimi sio mtuhumu ni ripota tuu!.

Pasco team Edward unajua wakayi mwingine unajichanganya hadi unakosa mwelekeo,sijui ndio influence ya bahasha ya kaki inakufanya upagawe.

Majibu haya iliyotoa hapa ni tofauti kabisa na ulichomjibu ukwelikitugani.

Majibu yako kwa ukwelikitugani umeandika kwamba "The one who allege is the one supposed to prove". Kisha ukaandika "The burden of proof lies with the prosecution".

Sasa kama unasema umefuta tongotongo za sheria UDSM kwa miaka minne,sasa hizi flip-flop zinatoka wapi? Au hata hizo tongotongo ulizotaka kufuta hukufanikiwa kuzifuta!!?
 
Last edited by a moderator:
Mwigamba anadanganywa na maadui wakuu wa chadema waliojipanga kusambaratisha Chadema kwa kila njia. Lakini kwa taarifa yake Chadema inaufahamu mchezo wake siku nyingi.

Alidiriki kujitenga na chama wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani Arusha na kipindi chote cha kampeni aliondoka Arusha. Kazi yote ya kampeni ilifanywa na Lema na Katibu Amani Golugwa.Nilielezwa kwamba alitaka Chadema ishindwe ili apate nafasi ya kumshambulia Lema..!!

Mtu wa aina hii nitasema ni msaliti na hastahili kuwa kiongozi wa Chadema. Angejua anachosema ni cha kweli kwenye hotuba yake ya jana angeushambulia uongozi na kuanika mabaya yote halafu wanachama waamue. Lakini kitendo cha kuusifu uongozi huku ukitoka njema unapigiana simu na maadui wa Chadema ni unafiki usiovumilika!!!!!

mkuu Molemo hizi habari za nilielezwa kama JeiKei hapa hazina nafasi
 
Soma:

6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.
(b) Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya uchaguzi mkuu atashika wadhifa wake hadi kipindi cha uchaguzi mkuu kinachofuata.
(c) Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
(d) Muda wa uongozi unaweza kufupishwa kama mamlaka iliyochagua au kuteua itaamua hivyo.
(e) Ibara hii itahusu pia viongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee wa CHADEMA.

6.3.4 Kukoma kwa Uongozi
(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya Chama.

​
 
Pasco team Edward unajua wakayi mwingine unajichanganya hadi unakosa mwelekeo,sijui ndio influence ya bahasha ya kaki inakufanya upagawe.

Majibu haya iliyotoa hapa ni tofauti kabisa na ulichomjibu ukwelikitugani.

Majibu yako kwa ukwelikitugani umeandika kwamba "The one who allege is the one supposed to prove". Kisha ukaandika "The burden of proof lies with the prosecution".

Sasa kama unasema umefuta tongotongo za sheria UDSM kwa miaka minne,sasa hizi flip-flop zinatoka wapi? Au hata hizo tongotongo ulizotaka kufuta hukufanikiwa kuzifuta!!?
Mkuu Mwita, usichanganye tuhuma na mashitaka!, tuhuma zikielekezwa kwako, wewe mjibu tuhuma ndio unapaswa kuzijibu. Ndio maana nikaridhika na majibu ya Dr. Slaa, jee umeona nikumuuliza Dr. alete ushahidi?., nimesema nasubiri verification ya hayo aliyoyasema!.

Mashitaka ndio mshtaki hutakiwa kuleta ushahidi!. Kwenye issue hii, hakuna mashitaka yoyote zaidi ya tuhuma tuu na majibu ya maneno matupu!, bado nasubiria hizo katiba!, kumbe katiba yenu ni deal hivi!.
Pasco
 
MTOTO KITAA,

Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela". Hoja ya " kwanini kusiwe na ukomo" si ya la Dr Slaa. Waulizwe watunga Katiba Mkutano Mkuu.

Nadhani tusipandikize hoja juu ya hoja, hatutapata majibu fasaha, tutabaki kukisia, kutoa tafsiri mbalimbali kwa maonjo ya kila mmoja. Nilichojibu ni kile ambacho kiko ndani ya mamlaka ya Katibu Mkuu. Hata hivyo, Katiba ya Chadema inatoa fursa, kwa kila mwanachama, kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba kwa utaratibu unaotolewa na Katiba yenyewe.

Kama kuna mtu anafikiria kuna hoja hiyo, hajachelewa awasilishe pendekezo ipitie vikao vya mabadiliko ya Katiba, na Kama vikao vitaridhia, mabadiliko yatafanyika, nadhani ndiyo demokrasia. Demokrasia siyo kile ambacho mtu mmoja mmoja anakifikiria!

Dr. Hoja hizo unajua lengo ni kufanya uchaguzi wa uongozi kwanza kukiwa na agenda ya CCM pili kuondoa kasi ya utendaji wa uongozi uliopo. Jibu kwa Pasco linatosha hawa wengine wanatafuta promo.
 
6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama
utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.
(b) Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya uchaguzi mkuu atashika wadhifa
wake hadi kipindi cha uchaguzi mkuu kinachofuata.
(c) Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena
mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
(d) Muda wa uongozi unaweza kufupishwa kama mamlaka iliyochagua au kuteua
itaamua hivyo.
(e) Ibara hii itahusu pia viongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee wa
CHADEMA.

6.3.4 Kukoma kwa Uongozi
(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya
katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya
Chama.
Mkuu Mkono Luzuba, asante kwa hii!, ila bado nasubiria scanned copies!.
Pasco.
 
Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela".
Mkuu DR. Slaa, kwanza asante kwa kuendelea kuwepo!, Hoja ni kipengele kilichonyofolewa kinyemela na sio kupenyezwa.

Nimeridhika na majibu yako, nasubiria tuu uthibitisho wa scanned copies.
Pasco.
 
Utatumia nguvu nyingi kuzuia haki isipatikane lakini kamwe haitakuwa milele.
 
CHADEMA tangu ianzishwe miaka yote hii Msajili wa vyama vya siasa nchini hakugundua kwamba CHADEMA ina katiba "fake".

Miaka miwili kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2015 baada ya juhudi mbali mbali za CCM za kudai CHADEMA ni chama cha wachagga, chama cha wakristo, chama kinachotaka kuleta fujo nchini na pia kupanga ugaidi (Ushahidi fake wa gaidi mwigulu) kushindikana ndio mnazuka na jingine kwamba katiba ya CHADEMA ni fake!!!!!

Hebu tuondoleeni upuuzi wenu usio na kichwa, miguu wala mkia hapa!!!!!! Watu wengine banaaaa DAH!!!!!!

 
Wanabodi,

Naomba msaada kwa yeyote mwenye Katiba ya Chadema ya 2004 kabla ya kesho, nikiikosa itanibidi kudamkia kwa Msajili ili kuipata kwa lengo la kuikamilisha thread yangu hii.

Natanguliza shukrani.

Pasco.
 
tumia tu akili ya kuzaliwa kaka, kama umekosa mitandaoni nenda makao makuu ya chama nina imani ni watu wema tu watakupatia ukipate hicho unachokitafuta. hapa unaudhihirishia umma kuwa wewe si mtu wa kutafuta taarifa unapenda kutafuniwa.....
 
Pasco hapa kunakitu kimejificha kwa nini ililetwa katiba moja ya mwaka 2006 pekee ambayo ndiyo inalalamikiwa kuchakachuliwa?

Twende mbele turudi nyuma hata kama katiba iko vile ilivyo ni utamaduni gani mtu wa kugombea uongozi milele bila kuwa na ukomo no! no! No! Hapa kunatatizo lakini mda siyo mrefu ukweli huu utabainika tu.
 
I like this kind of argument. My thanks to Dr. as well for his constructive ideas and quick intervention, I knew you would come in before 'things get worst', as some one waited for it.
 
Naomba kukosolewa,ktk Katiba ya Chadema...Sura ya Sita,ibara za tatu,ibara ndogo za pili(a),,na tatu (a) zina ukakasi usiostahili kukaliwa kimya

Naomba kuzinukuu,kisha nifafanue zinavyokinzana..Nanukuu:-

6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.

6.3.3 Kurekebisha tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Chama
(a) Tarehe ya uchaguzi mkuu wa Chama inaweza kurekebishwa kwa kusogezwa mbele kwa muda usiozidi mwaka mmoja toka mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo.

Mwisho wa kuzinukuu

SASA,KAMA SURA YA SITA,IBARA YA TATU,IBARA NDOGO YA PILI (A) IMEWEKA UKOMO WA UONGOZI,WA MIAKA MITANO,,,HALAFU IBARA YA TATU,IBARA NDOGO YA TATU(A) INATOA FURSA KWA CC KUONGEZA MUDA WA UONGOZI,KWA MWAKA MMOJA,,TENA BILA HATA KUELEZA NI MAZINGIRA GANI YATAKAYOLAZIMU UONGEZAJI WA MUDA HUSIKA,,HUU SIO UHUNI HUU??,,,HUKU SIO KUKINZANA KIUFUNDI,KWA VIPENGELE VIWILI VILIVYO WAZI KABISA? Dr.W.Slaa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom