Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Pasco umeibuja fitna iliyokuwa imetulia tuliiiiiii

Umefanya jambo ambalo CCM na entire CC wameshindwa kulifanya.....

I hope by saa 5 asubuhi utapata simu toka kwa Kinana.

Nakuhakikishia hiyo katiba unayoitaka na hizo so called minutes za SLAAA kwenda kwa msajili wa vyama zote zitapatikana leo leo (dont ask me how lakini uwezo, nia na sababu zipo)

Ahhhhh hivi kweli wana chadema zaidi ya 400 humu ndani mmeshindwa kuleta hiyo katiba kwa kuogopa member mmoja tuu bwana PASCO?

Nasema hivi kuna umuhimu hiyo department ya dark arts ya CCM apewe PASCO

salaaaleeee
Itabidi kwanza nipewe uanachama wa CCM ndipo hayo mengine yafuate.
Ila pia kuna aina mbali mbali za ujenzi, nyingine ni kwa kutikisa kwa nguvu ili kupima uimara, ikitikisika, unabidi kubomoa ili kujenga upya imara zaidi!.

Kama tunataka Chadema imara, ni lazima tuipitishe kwenye tanuru la moto, ikipita sala, inageuka chuma cha pua!.

Mimi sina chama, ila pia inawezekana kwa kuisakama Chadema, ndio naiimarisha zaidi kuliko wapenzi wa Chadema ambao kazi yao ni kuiimbia nyimbo za sifa na mapambio.

Pasco.
 
Mkuu Pasco kama ulichokiandika kwenye paragraph ya kwanza hapo chini ni kweli basi hakuna haja ya kuwa na sheria za vyama vya siasa pamoja na ofisi ya msajili, na kama umepotosha umma basi miaka yako minne pale UDSM ulikwenda poteza muda. Binafsi naamini ( japo sijaisoma sheria za vyama vya siasa) kunakuwa na minimum standards za muundo wa vyama vya siasa, na hivyo kutoa muongozo wa vitu gani vya msingi viingie kwenye katiba.

Mkuu Samson Moses, katiba za vyama ni mali za vyama, hata ikitamka kiongozi ni kipindi chote cha uhai mpake afe, msajili atairidhia!.

Hoja yangu ni kuwa ku na katiba ya Chadema ya 2004 inadaiwa iliweka bayana muda wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Hii ndio katiba halali, kisha chama kina haki ya kuibadili wakati wowote ila mabadiliko haya yaliza yapitie process ya kichama na kuwasilishwa kwa msajili, ukishawasilisha katiba mpya, ile ya zamani inabatilishwa automatically.

Hoja ya Mwigamba ni kuwa katika kupitisha katiba mpya ya Chadema ya 2006, kuna kipengele cha ukomo, kilinyofolewa kinyemela, hivyo katiba iliyopelekwa haina kipengele hicho!.

Kitendo cha kufanya mabadiliko ya katiba, bila kukizungumzia kipengele fulani, au kukifuta rasmi na badala yake kukichomoa kinyemela, ndiko kunakopelekea, katiba hiyo kuwa fake!.

Bado naisubiria katiba ya Chadema ya 2004 ili kulithibitisha hili!.

Pasco.
 
Pasco hapa kunakitu kimejificha kwa nini ililetwa katiba moja ya mwaka 2006 pekee ambayo ndiyo inalalamikiwa kuchakachuliwa?

Twende mbele turudi nyuma hata kama katiba iko vile ilivyo ni utamaduni gani mtu wa kugombea uongozi milele bila kuwa na ukomo no! no! No! Hapa kunatatizo lakini mda siyo mrefu ukweli huu utabainika tu.

Wewe una akili finyu sana.
 
Tatizo la wewe Pasco ni moja, kuleta hoja bila kuzifanyia tafiti. Mimi nashangaa wanaosumbuka na Freeman Mbowe, baada ya kuangaika na Dr Slaa akaonekana kuwa ni kisiki sasa naona mnaamia kwa Mbowe. Kwa kumbukumbu zangu, Freeman Mbowe alikwisha tamka mara kadhaa kuwa hatagombea tena nafasi hiyo. Pili, hivi ni kweli kwa akili za kawaida kabisa, Mbowe anaweza akachomoa hicho kipengele na wajumbe wote wa mkutano mkuu wakamuangalia na kumchekea? Kwanini tusiwe wa kweli kuwa, kama hicho kipengele akipo basi wakulaumiwa ni wajumbe walipitisha hiyo katiba na sio Mbowe.

Zaidi sana, mimi nazichukulia tuhuma hizi ni upepo ulioanza tangu katikati ya mwezi huu, kuanzia kwenye ruzuku, pesa za uswisi na sasa hili la katiba. Hii ni mipango mkakati wa watu wasioitakia mema CHADEMA kujifanya wanaipenda sana CHADEMA kiasi cha kuwa wasemaji wa chama hiki.

CHADEMA ni mpango wa MUNGU, akuna wa kuwa kinyume chake.
...Naam! Biblia takatifu inasema watakuja kwa njia moja Yeye Yehova atawatawanya kwa njia saba. yametokea, yanatokea na yataendelea kutokea. tutulie tu. Hawataweza hata wapange kwa kulishana viapo kwa masangoma.
 
Kinyume cha uongo ni ukweli, huyo kiongozi aliyesimamishwa uongozi ndani ya chadema kwa kutuhumiwa kusema uwongo ni lazima tuthibitishe uwongo wake kwa kutumia ukweli.

Hoja ya Pasco ina mshiko ama mantiki kubwa sana. Tunataka maandiko ya hiyo katiba ya 2004 ili kujua mbichi na mbivu.

Welldone Pasco.
 
Mkuu Pasco kama ulichokiandika kwenye paragraph ya kwanza hapo chini ni kweli basi hakuna haja ya kuwa na sheria ya vyama vya siasa pamoja na ofisi ya msajili, na kama umepotosha umma basi miaka yako minne pale UDSM ulikwenda poteza muda. Binafsi naamini ( japo sijaisoma sheria ya vyama vya siasa) kunakuwa na minimum standard za muundo wa vyama vya siasa, na hiyo kutoa muongozo wa vitu gani viingie kwenye katiba.
Investa, no first and hard rules za katiba, sheria ni majina tuu yasiwe ya zamani, chama kisiwe na kikabila, cha kidini, na lazima kiwe na wanachama bara na pwani.

Hakuna hitaji lolote la kisheria kuhusu uchaguzi wa ndani wa chama zaidi ya hitaji la kila chama lazima kiwe na bodi ya wadhamini!. Chama kikiamua uchaguzi wake wa ndani ni kila baada ya miaka 10 ni sawa tuu!, au rais wa chama ni life president, its ok!, kwa vile Tanzania tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka 5, then vyama vyote vimejikuja vime subscribe miaka mitano mitano kwenye katiba zao!.

Pasco.
 
Duh Asante sana kwa kutujuza Kumbe chama kqmq familia maana baba hana mrithi wq kuwa baba katika familia khaa
 
Kama ndio hivyo mkuu basi tunahaja sasa ya kuweka minimum standards za hizi katiba ziweje! Guideline lazima iwekwe, kwa sababu lengo la kuleta vyama vingi na nchi kuridhia ni katika jitihada za kutanua wigo wa demokrasia. Kwa msingi huohuo inabidi jitihada zifanyike kuwe na minimum standards kuhusiana katiba yenye kukidhi vigezo gani inatakiwa.
Sambamba na hilo, ukaguzi wa ndani ya vyama inatakiwa pia uwekewe utaratibu wenye kueleweka. Yote haya yanapoint weakness kwenye hii ofisi ya msajili pamoja na sheria za vyama vingi.
Umefika wakati sasa hii ofisi ianze kufanya kazi yake badala ya kutisha tisha kufuta vyama vya siasa wakati watendaji wenyewe hawako proactive kwenye oversight supervision. Wanasubiri mpaka Mwigamba na Zitto kabwe waibue mambo ndo waanze kupata coverage ya malumbano na vitisho kwenye vyombo vya habari! Aibu yenu ofisi ya msajili.

Investa, no first and hard rules za katiba, sheria ni majina tuu yasiwe ya zamani, chama kisiwe na kikabila, cha kidini, na lazima kiwe na wanachama bara na pwani.

Hakuna hitaji lolote la kisheria kuhusu uchaguzi wa ndani wa chama zaidi ya hitaji la kila chama lazima kiwe na bodi ya wadhamini!. Chama kikiamua uchaguzi wake wa ndani ni kila baada ya miaka 10 ni sawa tuu!, au rais wa chama ni life president, its ok!, kwa vile Tanzania tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka 5, then vyama vyote vimejikuja vime subscribe miaka mitano mitano kwenye katiba zao!.

Pasco.
 
Hapo Arusha kama kawaida, kuna mpango wa kumpata cheo cha aliyefukuzwa mshikaji kutoka kule maeneo. Subiri muone, kule kule atatoka mtu wa kule kule na kuendeleza utartibu ule ule wa Kikanda na chama chao. Kama kawaida ya chama chetu.
 
Wazungu wanasema uwezo wa kufikiri wa sisi waafrika ni mdogo, hivi ni nani anayetakiwa kuthibitisha ukweli wa Mwigamba? Yeye atuletee hiyo katiba anayodai imechakachuliwa tuone hicho kipengele, au nyie mnao mwunga mkono mlete ushahidi. Anaye tuhumu ana wajibu wa kuthibitisha tuhuma dhidi ya mtuhumiwa, tusiwe kama kasuku tujipe muda wa kufikiri japo kidogo. By the way, huwezi fanya alicho kifanya huyu jamaa halafu bado ukaendelea kuwa kiongozi, haiwezekani. Arusha panatamaniwa sana na CCM, labda hii ndiyo mikakati yao ya kuirudisha mikononi mwao kwa kuivuruga CDM, panahitaji mwenyekiti wa ukweli siyo hawa wanao watafutia watu vyeo.
 
hata dr slaa amekanusha alete katiba ya 2004
 
Aliyetoa tuhuma hizi sio mimi, ni kiongozi mwandamizi wa Chadema, mimi nimetoa tuu angalizo kama ni kweli, what might hapenkwa Chadema!. Kwa sasa ni kweli huu ni upuuzi usio na kichwa wa miguu, ila utakuwa umenisaidia sana kama utanipatia hiyo katiba ya 2004!.
Pasco.

Sitaki kuamini kuwa wewe na Mwigamba lenu ni moja. Haiishii hapo naona kwa sasa Raia Mwema ana makala za "magaidi" ndani ya CDM.

Kwa heshima zote hoja hizi mfu mnataka kuisaidia CHADEMA au mnataka "KUIMALIZA CHADEMA" kama agenda ya TISS na JK.

Tuna "wajibu" na nchi yetu kwa kila jambo. Hizi "line up" zenu za kuishambulia CHADEMA inaonyesha kukosekana ukomavu kwa sababu kujielekeza kwenye Katiba ya CHADEMA ili mpate sababu za kuifuta mtaishia kujifuta wenyewe.

Kwa sasa kungekuwa na jitihada mbadala za utekelezaji wa sera na siyo Katiba za vyama ambavyo vina uhalali wa Kisheria.

Tuseme kuna kipengele kimonyofolewa na Msajili ana Katiba anayoikubali wewe itakusaidia nini? Itakula kwa Msajili na uchaguzi wa CDM kwa agenda na matakwa ya CCM hamtaambulia kitu.

Nikukumbushe Pasco (Pascal Mayala) kwenye kipindi chako cha KipimaJoto ITV ulipokuwa na JK kwenye "podium" ulimuuliza swali la hela nyingi (20bn??) akakuambia wale waarabu anafanya nao biashara; kipindi kikafia hapo. Nilitegemea kama mwandishi ungekwenda mbali kuwa hiyo biashara ni uuzaji wa mali asili au nchi yenyewe kama inavyojitokeza sasa hivi. ULINYAMAZA, UMENYAMAZA na UNAENDELEZA agenda ya "Boyz to Men" ya JK na EL. Ni sawa kabisa na ni haki yako, ila kumbuka CDM nao wana haki ya kuendesha shughuli zao kisheria na kihalali. Na mimi navutiwa na nimeshawishika kuwa ni MBADALA halali wa siasa za nchi yetu.

Nimewaza sana kuhusu bandiko la Mwigamba makala ya Raia Mwema na bandiko lako; sipati hata chembe ya sababu muhimu ya KITAIFA ya kushadidia bandiko la kuishambulia CHADEMA zaidi ya mateke ya mfa maji. Mimi ni mtu wa Arusha, Mwigamba awe yuko sahihi mbele yako na mbele ya CCM kwangu mimi hayuko sahihi kwa sababu anaendeleza agenda ya adui yangu CCM akiwa ndani ya uongozi wa CHADEMA. Na ni matumaini yangu anyang'anywe uanachama kwa sababu "once mamluki always mamluki" arudi kwa waliomtuma na anao wakubali.

Kwa suala la katiba endeleeni kwa sababu baada ya kushindwa kwenye medani zote mnataka CDM ifutwe. Wewe kama mkristo unajua kuwa "wale walipoambiwa wanyamaze, Yesu akawaambia wakinyamaza hawa mawe yatapiga kelele". Jiandaeni maana kwa sasa MAWE YAKO TAYARI KUPIGA KELELE
 
Kinyume cha uongo ni ukweli, huyo kiongozi aliyesimamishwa uongozi ndani ya chadema kwa kutuhumiwa kusema uwongo ni lazima tuthibitishe uwongo wake kwa kutumia ukweli.

Hoja ya Pasco ina mshiko ama mantiki kubwa sana. Tunataka maandiko ya hiyo katiba ya 2004 ili kujua mbichi na mbivu.

Welldone Pasco.

Haina mshiko analalamika kuwa "source" haifichiki tena. Au mnataka tuanze kuanika ya CCM hapa jamvini kwa kuanzia na Katiba?
 
Mkuu Only 83, kwanza nimekubali udhaifu, uriporter sikusomea!, hivi kuwa ripota hapa jf ni mpaka usemee?!.
Kazi ya kwanza ya mwandishi yoyote ni kuripoti tuu!, hilo la kufanya uchunguzi, linahitaji specialization na uwezo fulani ambao kwa bahati mbaya mimi sina!. Nimeikuta thread humu jf, nimeiripoti tuu kilichoelezwa!.
Hili la uwezo wangu mdogo wa kuchambua mambo, pia nalikubali kama nilivyokubali mimi mwandishi dhaifu mwenye uvivu wa kufikiri!.

Baada ya yote hayo, maadamu Chadema imetuhumiwa kwa katiba feki, Katibu Mkuu amekanusha sio feki, nasubiri basi hizo katiba, tuyamalize!.
Pasco.

Mara nyingi MODS uwa wanakazia watu tuweke thread ambazo ni sahihi na hasa tunaporipoti ishu inayogusa maslahi ya wengi. JF sio kijiwe na wambea na wazandiki, ni Great Thinker Forum, tunataka thread zilizochujwa na kuchujika. Unaposema kuripoti hoja hapa JF ni lazima uwe umesomea, nasema si lazima, ila unapaswa kutumia akili za kawaida kama Great Thinker ili ufanye kitu ambacho ni productive..ulichofanya wewe ni kuleta mipasho nk. Badilika wewe, ebo!!
 
Sitaki kuamini kuwa wewe na Mwigamba lenu ni moja. Haiishii hapo naona kwa sasa Raia Mwema ana makala za "magaidi" ndani ya CDM.

Kwa heshima zote hoja hizi mfu mnataka kuisaidia CHADEMA au mnataka "KUIMALIZA CHADEMA" kama agenda ya TISS na JK.

Tuna "wajibu" na nchi yetu kwa kila jambo. Hizi "line up" zenu za kuishambulia CHADEMA inaonyesha kukosekana ukomavu kwa sababu kujielekeza kwenye Katiba ya CHADEMA ili mpate sababu za kuifuta mtaishia kujifuta wenyewe.

Kwa sasa kungekuwa na jitihada mbadala za utekelezaji wa sera na siyo Katiba za vyama ambavyo vina uhalali wa Kisheria.

Tuseme kuna kipengele kimonyofolewa na Msajili ana Katiba anayoikubali wewe itakusaidia nini? Itakula kwa Msajili na uchaguzi wa CDM kwa agenda na matakwa ya CCM hamtaambulia kitu.

Nikukumbushe Pasco (Pascal Mayala) kwenye kipindi chako cha KipimaJoto ITV ulipokuwa na JK kwenye "podium" ulimuuliza swali la hela nyingi (20bn??) akakuambia wale waarabu anafanya nao biashara; kipindi kikafia hapo. Nilitegemea kama mwandishi ungekwenda mbali kuwa hiyo biashara ni uuzaji wa mali asili au nchi yenyewe kama inavyojitokeza sasa hivi. ULINYAMAZA, UMENYAMAZA na UNAENDELEZA agenda ya "Boyz to Men" ya JK na EL. Ni sawa kabisa na ni haki yako, ila kumbuka CDM nao wana haki ya kuendesha shughuli zao kisheria na kihalali. Na mimi navutiwa na nimeshawishika kuwa ni MBADALA halali wa siasa za nchi yetu.

Nimewaza sana kuhusu bandiko la Mwigamba makala ya Raia Mwema na bandiko lako; sipati hata chembe ya sababu muhimu ya KITAIFA ya kushadidia bandiko la kuishambulia CHADEMA zaidi ya mateke ya mfa maji. Mimi ni mtu wa Arusha, Mwigamba awe yuko sahihi mbele yako na mbele ya CCM kwangu mimi hayuko sahihi kwa sababu anaendeleza agenda ya adui yangu CCM akiwa ndani ya uongozi wa CHADEMA. Na ni matumaini yangu anyang'anywe uanachama kwa sababu "once mamluki always mamluki" arudi kwa waliomtuma na anao wakubali.

Kwa suala la katiba endeleeni kwa sababu baada ya kushindwa kwenye medani zote mnataka CDM ifutwe. Wewe kama mkristo unajua kuwa "wale walipoambiwa wanyamaze, Yesu akawaambia wakinyamaza hawa mawe yatapiga kelele". Jiandaeni maana kwa sasa MAWE YAKO TAYARI KUPIGA KELELE
Mkuu Mimi baba, honestly nimeipenda objectivity yako kwenye post yako. Post yako, ya 175 ndio ya kwanza kuchangiwa humu ki great mind, japo kuna great mind wengine walichangia ila sio sio ki great mind.

Tukio likitokea, simple mind watawazungumzia wafanya tukio, Mwigamba, Pasco, Mbowe, Dr. Slaa etc.
Ordinary mind, watazungumzia event, ya Mwigamba kusimamishwa, kutumia pen name kupost ukweli mchungu!,
Great Mind wataulizia "the motive behind" kama ulivyofanya hapa!.

Kama unamfahamu vizuri Mwigamba, unasoma makala zake, utakubaliana na mimi he is bold na very brave!. Ukumuona shujaa wa vita anaingia chini ya uvungu wa kitanda kumkimbia panya, simple mind atamzungumzia shujaa, ordinary mind atacheka kwa kitendo cha shujaa kuingia uvunguni, great mind ata find out the reasons behind shujaa huyu kuogopa panya!.

Nilipolisoma tuu bandiko lake humu jf na mtu yoyote genuine, atakubaliana na mimi Mwigamba amesema kweli tupu!. Kwa ushujaa alionao, unajiuliza what is his motive behind?!, why aogope panya mpaka kujigeuza maskini kulima!. Ndipo nikaelewa Mwigamba was a "caged bird", ndege tunduni!. Chadema should " let the caged bird sing" na kwa walio ndani ya Chadema, nadhani ni Prof. Mwesiga Beregu na ZZK tuu ndio wenye ujasiri huo!. Mimi sio Chadema na kama unadhani ni CCM pia your wrong!.

Kuna wrong notion kuwa kila anayeishambulia Chadema, haitakii mema!. Nimezisima hoja za Mwigamba they are truth!, isipokuwa hili la uchakachuaji katiba ndilo mimi nimelipick kulitafuti`a ukweli, japo limeisha kanusha kuwa ni uwongo na uzushi, bado nasubiria uthibitisho!.

Ukinisoma baadhi ya mabandiko yangu mengi ni kweli naishambulia sana Chadema, kuwa kama ni kweli, inataka Watanzania tuiaminie tuikabidhi nchi come 2015, its seriously needs to change tangu juzi na jana na leo ndio mwisho, kesho might be too little too late!.

Kutokana na wengi humu kuwa na mapenzi makubwa na Chadema, karibu wote mnachelea kuiambia ukwel;i na kubaki kuiimbia nyimbo za sifa na mapambia as if all is well. Angalau Mzee Mwanakijiji hujitahidi tahidi kiaina, mimi huwa sikopeshi, ndiye niliyeanzisha kuwambia JK ni dhaifu, nikawaambia CCM Wamechokwa, nikawaambia Chadema hawajajipanga. If you dig deep into my threads utagundua the motive behind, ni maslahi ya taifa na sio chuki dhidi ya Chadema!. Kuweza kunisoma in beyween the lines, nako kuna hitaji level fulani ya uelewa, naamini Dr. na wachache humu, wananielewa fikawanajua fika ninaulizia nini na my motive behind iko open!. 2015, nchi haiwezi kukabidhiwa kwa Chadema kwenye kikombe cha chai!, kwa mwendo huu Chadema inaokwenda nao, naiona kabisa jinsi nchi tunavyoikabidhi tena CCM huku sisi tusio na vyama tumejinyamazia tuu!. Nimeamua kujitolea kuwaambia loud and clear, ili ikifika 2015, niwakumbushe nilicho waambia!.

Pasco.
 
Mara nyingi MODS uwa wanakazia watu tuweke thread ambazo ni sahihi na hasa tunaporipoti ishu inayogusa maslahi ya wengi. JF sio kijiwe na wambea na wazandiki, ni Great Thinker Forum, tunataka thread zilizochujwa na kuchujika. Unaposema kuripoti hoja hapa JF ni lazima uwe umesomea, nasema si lazima, ila unapaswa kutumia akili za kawaida kama Great Thinker ili ufanye kitu ambacho ni productive..ulichofanya wewe ni kuleta mipasho nk. Badilika wewe, ebo!!
Mkuu Only83, kuwa great thinker ni uwezo, ikitokea hauna, ni hauna, very unfortunately, mimi sio great thinker, and I can't pretend to be one!.
I believe in truth!, ukweli lazima usemwe no matter what, kama ukweli ukijulikana unaweza kuleta mipasuko, hivyo unaona bora u jenge nyumba yako on a lie, kama kujengea tofali la barafu?. Bado naisubiri katiba ya Chadema ya 2004 ili ukweli uthibitishwe!.
Pasco.
 
Nadhan shutuma za mwigamba zina ukwel ndan yake maana cc km wanachama wa cdm tuliambiwa uchaguz wa matawi mwez wa 3, wa kata mwez 6 na wawilaya mwez wa 10 lkn mpaka sasa hakuna cha uchaguz wala nini zaid ya kuteuana tu bila mpangilio.
 
Back
Top Bottom