Dr. Willibrod Slaa
Public Figure
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,524
Slaa sisi hatujalishwa unga wa ndere. Je kwanini kusiwe na ukomo wa uongoz? Je hii ndio demokrasia mnayopigia kerere kila siku? Slaa kumbuka sisi sio mazombi. Na ujipange uje utoe majibu sahii hapa sisi hatuna zidumu fikra...................
Mwenye jukumu la kutoa ushahidi wa vinginevyo ni mtuhumiwa!, mimi sio mtuhumu ni ripota tuu!.
Mwigamba anadanganywa na maadui wakuu wa chadema waliojipanga kusambaratisha Chadema kwa kila njia. Lakini kwa taarifa yake Chadema inaufahamu mchezo wake siku nyingi.
Alidiriki kujitenga na chama wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani Arusha na kipindi chote cha kampeni aliondoka Arusha. Kazi yote ya kampeni ilifanywa na Lema na Katibu Amani Golugwa.Nilielezwa kwamba alitaka Chadema ishindwe ili apate nafasi ya kumshambulia Lema..!!
Mtu wa aina hii nitasema ni msaliti na hastahili kuwa kiongozi wa Chadema. Angejua anachosema ni cha kweli kwenye hotuba yake ya jana angeushambulia uongozi na kuanika mabaya yote halafu wanachama waamue. Lakini kitendo cha kuusifu uongozi huku ukitoka njema unapigiana simu na maadui wa Chadema ni unafiki usiovumilika!!!!!
Mkuu RITZ, nimejibiwa vizuri kabisa na Dr. Slaa, ninachosubiri ni uthibitisho tuu wa ukweli huo.
Mkuu Mwita, usichanganye tuhuma na mashitaka!, tuhuma zikielekezwa kwako, wewe mjibu tuhuma ndio unapaswa kuzijibu. Ndio maana nikaridhika na majibu ya Dr. Slaa, jee umeona nikumuuliza Dr. alete ushahidi?., nimesema nasubiri verification ya hayo aliyoyasema!.Pasco team Edward unajua wakayi mwingine unajichanganya hadi unakosa mwelekeo,sijui ndio influence ya bahasha ya kaki inakufanya upagawe.
Majibu haya iliyotoa hapa ni tofauti kabisa na ulichomjibu ukwelikitugani.
Majibu yako kwa ukwelikitugani umeandika kwamba "The one who allege is the one supposed to prove". Kisha ukaandika "The burden of proof lies with the prosecution".
Sasa kama unasema umefuta tongotongo za sheria UDSM kwa miaka minne,sasa hizi flip-flop zinatoka wapi? Au hata hizo tongotongo ulizotaka kufuta hukufanikiwa kuzifuta!!?
MTOTO KITAA,
Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela". Hoja ya " kwanini kusiwe na ukomo" si ya la Dr Slaa. Waulizwe watunga Katiba Mkutano Mkuu.
Nadhani tusipandikize hoja juu ya hoja, hatutapata majibu fasaha, tutabaki kukisia, kutoa tafsiri mbalimbali kwa maonjo ya kila mmoja. Nilichojibu ni kile ambacho kiko ndani ya mamlaka ya Katibu Mkuu. Hata hivyo, Katiba ya Chadema inatoa fursa, kwa kila mwanachama, kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba kwa utaratibu unaotolewa na Katiba yenyewe.
Kama kuna mtu anafikiria kuna hoja hiyo, hajachelewa awasilishe pendekezo ipitie vikao vya mabadiliko ya Katiba, na Kama vikao vitaridhia, mabadiliko yatafanyika, nadhani ndiyo demokrasia. Demokrasia siyo kile ambacho mtu mmoja mmoja anakifikiria!
Mkuu Mkono Luzuba, asante kwa hii!, ila bado nasubiria scanned copies!.6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama
utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.
(b) Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya uchaguzi mkuu atashika wadhifa
wake hadi kipindi cha uchaguzi mkuu kinachofuata.
(c) Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena
mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
(d) Muda wa uongozi unaweza kufupishwa kama mamlaka iliyochagua au kuteua
itaamua hivyo.
(e) Ibara hii itahusu pia viongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee wa
CHADEMA.
6.3.4 Kukoma kwa Uongozi
(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya
katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya
Chama.
Mkuu DR. Slaa, kwanza asante kwa kuendelea kuwepo!, Hoja ni kipengele kilichonyofolewa kinyemela na sio kupenyezwa.Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela".
Asante.katiba ya chadema 2006