Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
- Thread starter
-
- #141
Mkuu Revo, hapo iko very clear kuwa uongozi wa Chadema ni kila miaka mitano mitano, ila sikitokea sababu zozote za kufanya uchaguzi usifanyike basi extention ni mwaka mmoja tuu, ukipita bila uchaguzi, viongozi wote waliopo wanakosa uhalali!.Naomba kukosolewa,ktk Katiba ya Chadema...Sura ya Sita,ibara za tatu,ibara ndogo za pili(a),,na tatu (a) zina ukakasi usiostahili kukaliwa kimya
Naomba kuzinukuu,kisha nifafanue zinavyokinzana..Nanukuu:-
6.3.2 Muda wa Uongozi
(a) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa uchaguzi mkuu wa Chama utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka mitano.
6.3.3 Kurekebisha tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Chama
(a) Tarehe ya uchaguzi mkuu wa Chama inaweza kurekebishwa kwa kusogezwa mbele kwa muda usiozidi mwaka mmoja toka mwisho wa uhalali wa uongozi uliopo.
Mwisho wa kuzinukuu
SASA,KAMA SURA YA SITA,IBARA YA TATU,IBARA NDOGO YA PILI (A) IMEWEKA UKOMO WA UONGOZI,WA MIAKA MITANO,,,HALAFU IBARA YA TATU,IBARA NDOGO YA TATU(A) INATOA FURSA KWA CC KUONGEZA MUDA WA UONGOZI,KWA MWAKA MMOJA,,TENA BILA HATA KUELEZA NI MAZINGIRA GANI YATAKAYOLAZIMU UONGEZAJI WA MUDA HUSIKA,,HUU SIO UHUNI HUU??,,,HUKU SIO KUKINZANA KIUFUNDI,KWA VIPENGELE VIWILI VILIVYO WAZI KABISA? Dr.W.Slaa
1. Katiba ilichakachuliwa au haikuchakachuliwa?
2. Unapouliza ni kwanini isemwe kipindi hiki, wewe ulitaka isemwe kipindi gani?
Aliyetoa tuhuma hizi sio mimi, ni kiongozi mwandamizi wa Chadema, mimi nimetoa tuu angalizo kama ni kweli, what might hapenkwa Chadema!. Kwa sasa ni kweli huu ni upuuzi usio na kichwa wa miguu, ila utakuwa umenisaidia sana kama utanipatia hiyo katiba ya 2004!.CHADEMA tangu ianzishwe miaka yote hii Msajili wa vyama vya siasa nchini hakugundua kwamba CHADEMA ina katiba "fake".
Hebu tuondoleeni upuuzi wenu usio na kichwa, miguu wala mkia hapa!!!!!! Watu wengine banaaaa DAH!!!!!!
Mkuu Revo, hapo iko very clear kuwa uongozi wa Chadema ni kila miaka mitano mitano, ila sikitokea sababu zozote za kufanya uchaguzi usifanyike basi extention ni mwaka mmoja tuu, ukipita bila uchaguzi, viongozi wote waliopo wanakosa uhalali!.
Haja yangu is still valid mpaka katiba ya 2004 itakapopatikana kuimaliza hii kitu!.
Pasco.
Mkuu Samson Moses, katiba za vyama ni mali za vyama, hata ikitamka kiongozi ni kipindi chote cha uhai mpake afe, msajili atairidhia!.Suala si wakati pekee,kama kweli katiba hiyo ni fake kama ambavyo aliyetuhumu alivyotuma kwenye JF basi nchi hii ina vacuum ya uongozi uliotukuka,ikiwa ofisi ya msajili inaendeshwa bila kufuata taratibu na sheria hakuna haja ya kuwa na ofisi hiyo tena.
Samson Mwigamba ameonyesha ni jinsi gani alivyo muoga na kutumia njia mbadala ya kutumia mitandao ya kijamii ilihali alikuwepo ndani ya kikao,huu ni unafiki uliokithiri.Kama kweli alikuwa na nia nzuri na chama kikao kile ndicho kilikuwa muafaka wa kuweka mambo yote bayana,kuliko kusifu na chini ya kapeti unaponda.
Ikithibitika katiba ni fake,wajumbe na viongozi waliogushi sheria iwaone kuliko kujaribu kupotosha umma kuwa chama kifutwe,chama hiki ni cha Watanzania na si mali ya mtu,unaposema unakifuta kwa makosa ya wachache ina maana unawanyima haki Watanzania zaidi ya milioni nane haki yao ya kupenda.
Mwigamba,nakuomba kaka yangu,funguka kama kweli wewe ni mwanaharakati uliyedhamiria kuikomboa nchi yetu kwa kusema ukweli,nani yupo nyuma ya pazia aliyesababisha wewe kubali kufanywa kipaza sauti zaidi kuliko uhalisia wenyewe kwa kutumia hidden image kuwakilisha usichokiamini kwa kusema mbali na ulichokitenda kwa wakati mmoja.
Tuhuma rasmi haziwezi kutolewa JF,Zinatolewa kwenye vikao halali vya Chama.
Mkuu Sixa, hoja ipi imebadilika?, hivi kuna hoja ya lugha?!.Hoja imebadilika saa ngapi? Kma hoja ni kuipata katiba ya 2004 nenda manhartan pale ama kwa msajili wa vyama utuletee scanned copies ubandike haapa. Sijui unmtuma nani Pasco. BTW maelezo ya @Dr W Slaa yanaonyesha katiba iliyopitishwa na wanachama imeandikwa kwa kiswahili, na ndio yenye minutes, hiyo ya kiingereza haijapitishwa na wanachama wala haina miniti so technically haitambuliki kisheria. In short hoja yako imejibiwa, usichotaka ni kuamini ukweli wa aliyoyajibu Dr Slaa. Otherwise umenifungua macho pia
Laiti ungelijua!.Pasco yupo Kilowasa lowasa stukeni.
Hii post atakuwa ameandika Slaa mwenyewe sio Josephine Mushumbusi.
Post za Slaa utazijua tu jinsi zinavyojenga hoja.
Mkuu Rose Mayemba, niliamini Chadema ni chama cha kisasa chenye wapenzi lukuki humu, nikitaraji by now, wangeishanimwagia hizo scanned copy!. Nikikosa kabisa, ndipo kesho nabisha hodi kwa Msajili.tumia tu akili ya kuzaliwa kaka, kama umekosa mitandaoni nenda makao makuu ya chama nina imani ni watu wema tu watakupatia ukipate hicho unachokitafuta. hapa unaudhihirishia umma kuwa wewe si mtu wa kutafuta taarifa unapenda kutafuniwa.....
MTOTO KITAA,
Nadhani umechanganya hoja. Hoja hapa ni kuwa " Katiba ni feki" kwa kuwa kuna " kipengele kimepenyezwa kinyemela". Hoja ya " kwanini kusiwe na ukomo" si ya la Dr Slaa. Waulizwe watunga Katiba Mkutano Mkuu.
Nadhani tusipandikize hoja juu ya hoja, hatutapata majibu fasaha, tutabaki kukisia, kutoa tafsiri mbalimbali kwa maonjo ya kila mmoja. Nilichojibu ni kile ambacho kiko ndani ya mamlaka ya Katibu Mkuu. Hata hivyo, Katiba ya Chadema inatoa fursa, kwa kila mwanachama, kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba kwa utaratibu unaotolewa na Katiba yenyewe.
Kama kuna mtu anafikiria kuna hoja hiyo, hajachelewa awasilishe pendekezo ipitie vikao vya mabadiliko ya Katiba, na Kama vikao vitaridhia, mabadiliko yatafanyika, nadhani ndiyo demokrasia. Demokrasia siyo kile ambacho mtu mmoja mmoja anakifikiria!
PASCO kauliza swali la msingi sana lakini nashangaaa mnazunguka mbuyu
LETENI HIYO KATIBA YA 2004 TUIONE, TUICHAMBUE KISHA TUTAJUA KAMA HIZI TUHUMA NI ZA UKWELI AU LA
kwanza leteni hiyo katiba