Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Umemjibu vizuri san mkuu.

Huyo jamaa anatakiwa ajaribu kujiweka katika nafasi ya wale waliopigwa bila sababu, kabla ya kukimbilia ku comment.
 
SIdhani kama wanaweza wakakemewa hadharani...

Ila kuna situations ambazo kichapo kinasaidia kuleta heshima.
Kinasaidia kuleta heshima kwa kupiga watu wasiohusika wala kuwepo katika tukio mkuu?
 
Bado hujasema
 
we kenge mkaiheshimu jeshi, kaa mbali na wanajeshi. Mmezidi kuwawajuaji, hata hapa umeandika utumbo we hujui majukumu ya jeshi. Mnapimana nguvu na wanajeshi. Mbona wapumbavu hivyo? Au ulifikiri jeshi km hicho chama chenu ambapo mmezoea malamishi na uwongo? Mi naona hao wanajeshi wa Kawe ni wastaarabu sana, ingekuwa makambi mengine leo hii kusingelikuwa na kijana wa kiume hapo kawe. Mnamwua mwanajeshi? Kweli halafu unakuja kuandika humu bila hata haya? Nyie ni vile vitoto vya single mothers, Pumbav kabisa
 
Mwanajeshi anayepiga mwananchi huyo sio mwanajeshi, ni mgambo kama mgambo wengine tu. Ni vizuri wakabainika hao wachache wakachukuliwa hatua ndani ya jeshi ili wasiendelee kulichafua jeshi letu tukufu.

Na nyinyi raia wekeni utii kwa askari wenu. Kumfanyia baya askari ni kulishushia heshima jeshi. Kama kuna uonevu jeshi lina mamlaka zake, ukiripoti jambo linafanyiwa kazi.
 
Tutawanyoosha hao viherehere alafu majeruhi tutwapeleka hospitali za jeshi mbona kazi mtakuwa nayo, kikubwa ni heshima kabla hujauponza
Gen. Mkunda alisema anataka jeshi ambalo wananchi watalikimbilia na sio kulikimbia.

"Mike" combat ni vazi la kuazima ukishalijua hili umeshinda.
 
Pa1 mkuu, ifike mahala kila mmoja wetu apaze sauti yake.

Maana leo kwa wana Kawe hatujui kesho itakuwa kwa kina nani.
nyie wapumbavu hamjui hata maana ya jeshi, Monduli pale duka bovu walivunjaga mpaka vinyumba vya wamasai baada ya kumpiga mwanajeshi na sime. Huko tena wameua? Vijana wa Dsm ni washamba sana na wapumbavu. Lazima aliyeua apatikane na bado mtapigwa sana mpaka mshike adabu. Heshimu wanajeshi hivyo visiasa vyenu uchwara kafanyieni huko vijiweni kwenu.
 
Inategemea.
Mfano mtu atoke Kinondoni aelekee zake Magomeni. Kufika pale mapipa itokee ajali kati ya gari yake na ya mwanajeshi.

Bila kujali ni nani aliesababisha ajali, itokee vurugu kati ya mwanajeshi na raia aliegongana nae. Katika purukushani purukushani yule raia azidiwe na mwanajeshi, so raia nae ili kujihami ili asije kuumizwa zaidi, achukuwe jiwe au kitu kilichopo karibu (nafikiri unafahamu mtu anapokuwa na hasira ya kujihami, huwa achagui silaha ya kutumia ili kujinusuru na kipigo) hivyo raia achukue jiwe, chuma au chochote kilichopo karibu amtwange nacho soja kichwani au popote.

Soja aanguke na kuzima hapo hapo. Raia nae kwa kutambua kuwa ameuwa japo sio kwa kukusudia (kumbuka raia alitumia hiyo silaha kwa lengo la kujiokoa au kujinusuru na kipigo cha mwanajeshi ambacho pengine na yeye kingesababisha kifo chake). So kama unavyojua mtu ukishaua hata kwa bahati mbaya, hauwezi kukaa kusubiri ukamatwe, hivyo raia aamue kukimbia kuelekea kwao Kinondoni kuangalia namna gani anaweza kupanga mpango wa kutoroka.

Jeshi lipate taarifa kwamba kuna mwenzao kauwawa Magomeni mapipa, jeshi lije pale mapipa na kuanza kupiga kila raia watakaekutana nae njiani, pengine na wewe ukiwa mpita njia kuelekea kariakoo ukumbane na kipigo kutoka kwa jeshi hilo kwa kigezo kuwa kuna mwenzao ameuwawa katika eneo hilo la mapipa.

Sasa hiyo kwako wewe unaona ni sawa kweli?
Kwamba muuaji awe mungine tena mmoja, alafu wapigwe wengine wasiojua wala kuhusika tena mamia?

Mambo mengine tuwe tunafikiria kabla ya kusapoti.

Ndio tunalipenda jeshi letu, tunaliheshimu na kulithamini. Lakin linapofanya unyama au uonevu dhidi ya raia ni lazima tuongee na kukemea hata kama hatusikilizwi
 
Kwahiyo leo hii ukipata tetesi kuwa Zuchu alitembea na mumeo, wewe hasira zako zote utazimalizia kwa kila msanii wa kike utakaekutana nae njiani, si ndio.... ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…