Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Siyo kaushamba,hawa ni washamba kabisa, nakumbuka miaka ya nyuma pale Mwenge kwenye magorofa waliyokuwa wanakaa hawa washamba walikuwa wanaweka mapazia ya viroba. Hawa walitakiwa wakae porini tu kwenye makambi yao.
😁😁😁 wewe wakikudaka wanakata hivyo vidole gumba vilivyo-type
 
Sio Rahisi Kama unavofikiria waulize wataalam wa Maswala ya kiusalama watakuambia Kama Ni Rahisi kiasi hicho Askari ambao tayari walishazoea kupokea mishahara alafu Leo hii uwafukuze waingie street njaa ya Mwezi mmoja tu utaanza kusikia Matukio ambayo jamii ilikuwa imepumzika nayo.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
I think nimekupata kwa namna fulani. Ila basi wajaribu kuwafundisha nidhamu na upendo wa dhati kwa raia.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
Rais anayesifiwa kwa utendaji wa watu wa chini basi abebe lawama za uzembe wa watu wa chini pia
 
Kumbe kuna kichapo kilitembezwa kawe na hamsemi?
Watu wa dar, kina Maghayo ni wasiri sana
 
Nidhamu iatawekwa na kufuatwa.....
Kama itaachwa hivyo kwamba amemuua mwanajeshi na hajafanywa chochote...Kesho itakuwa wewe
Tatizo tunaloongelea hapa, sio kutaka kuachwa kwa aliefanya tukio. Tatizo ni ile aliefanya tukio ni mungine, na wanaopigwa na hao sojaz ni wengine ambao hawakuwepo na wengine hawakufahamu hata kilichokuwa kimetokea.

Lakini pia sheria zipo na mahakama pia zipo, hivyo wangeiachia polisi na mahakama wafanye kazi yao, na kama polisi wangeshindwa kumkakata basi hapo ndo wangeingia mtaani kumtafuta wenyewe na kisha kumfikisha katika vyombo vya sheria.

Lakin kumbuka kwamba siku hiyo kijana hakukusudia kuuwa mtu. Bali ni ajali iliyosababishwa na marehem mwenyew kwa kuziba njia ambayo ipo kwa ajili ya watu wote wenye vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu kupita.

Mjeda alipoombwa kistarab apaki gari lake pemben ili jamaa apite na bajaj yake, ndo hapo mjeda alipoanza kumshambulia jamaa kwa maneno na kisha kumpa makofi kadhaa yaliosababisha hasira kwa kijana (hata wewe kupigwa mbele ya watu na mtu ambae ndio mwenye kosa, usingeweza kuvumilia), hivyo dogo akapandwa hasira na kuamua ku revenge kwa kutumia kisu cha mkunjo kilichosababisha umauti wa soja.

Kama soja angepaki gari yake mahali sahihi au kuamua kupaki pembeni kistaarab kama dogo alivyomuomba, yote hayo yasingetokea.

Hivyo binafsi sifurahishwi na uonevu au mauaji ya aina yoyote ile. Msimamo ni kwamba jeshi halikutakiwa kupiga watu hovyo kwa kosa la mtu mungine.
 
Back
Top Bottom