Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Asubuhi Askari woote kikosini kunakuwa na Master parede!
Waathirika waende wakawatambue Walio Fanya ushamba WA kupiga Walio waajiri....
Ya nimekupata vizuri mkuu. Huu ushauri ni mzuri, japo najua hakuna atakaeufanyia Kazi.
 
Mpaka sasa media zote ziko kimya
Hata zile media za umbeya hawajarusha kitu

Ova
 
Ingia mtaani basi na mdudu, slaa, na mwambulukuku muandamane mpaka jeshini. Mwiteni na lussu awasaidie kisheria za kufoka foka.
Duh kweli wanajeshi wa tz hawana shuguli ya kufanya
Ila wanatakiwa wabadilike vyanzo vyao vingi ya ugomvi ni wanawake na pombe
Sishabiki mjeshi kuuliwa ila kafa kifo cha kizembe sana na huyo jamaa wa bajaji naye mpuz hakutumia busara angeachana naye tu

Ova
 
Ya nimekupata vizuri mkuu. Huu ushauri ni mzuri, japo najua hakuna atakaeufanyia Kazi.
Nakumbuka kuna wakati kunduchi mtongani ilitokeaga wananchi kupigwa,
Sababu hizo hizo za madem na mapombe,naona muda sana kumetulia huko

Ova
 
Siyo kaushamba,hawa ni washamba kabisa, nakumbuka miaka ya nyuma pale Mwenge kwenye magorofa waliyokuwa wanakaa hawa washamba walikuwa wanaweka mapazia ya viroba. Hawa walitakiwa wakae porini tu kwenye makambi yao.
Du!hiyo sasa ni chuki
 
Duh kweli wanajeshi wa tz hawana shuguli ya kufanya
Ila wanatakiwa wabadilike vyanzo vyao vingi ya ugomvi ni wanawake na pombe
Sishabiki mjeshi kuuliwa ila kafa kifo cha kizembe sana na huyo jamaa wa bajaji naye mpuz hakutumia busara angeachana naye tu

Ova
Zamani walikuwa hawaruhusiwi kutoka kambini mpaka kwa kazi na vibali maalum, sifahamu kwanini siku hizi wanachanganyika sehemu za kiraia kiholela.

Lazima kuwe na matukio ya kiajabu ajabu.
 
Kwanza nina imani dogo wa bajaj hakujua kama anaegombana nae ni mwanajeshi.

Pili katika maisha kuna kitu kinaitwa hasira haswa unapopigwa au kudhalilishwa mbele ya watu (kitendo cha mjeshi kumchapa dogo makofi mbele ya watu huku akijua fika kwamba yeye ndio mkosaji) kilimfanya dogo ahisi uonevu na udhalilishaji wa hali ya juu.

Mwisho kabisa dogo alichukua hatua ile kujihami maana huenda aliona angeendelea kupokea kipigo zaidi. Lkn pia naamini dogo hakujua kama kile alichofanya kujihami au kujinasua na kipigo kingesababisha kifo cha msoja.

Ndio maana siku zote tunaambiwa kuwa hasira ni hasara.
 
Zamani walikuwa hawaruhusiwi kutoka kambini mpaka kwa kazi na vibali maalum, sifahamu kwanini siku hizi wanachanganyika sehemu za kiraia kiholela.

Lazima kuwe na matukio ya kiajabu ajabu.
Inasemekana kuwa ile kuwakataza kutoka kambini enzi zile ndio ilikuwa inasababisha matatizo makubwa, na pengine mauaji katika familia zao.

Hivyo ikapendekezwa kwamba jamaa waachwe wajichanganye uraiani ili angalau kujiona kuwa na wao ni sehemu ya watu (raia)
 
Zamani walikuwa hawaruhusiwi kutoka kambini mpaka kwa kazi na vibali maalum, sifahamu kwanini siku hizi wanachanganyika sehemu za kiraia kiholela.

Lazima kuwe na matukio ya kiajabu ajabu.
Wana ushamba fulani,ushamba wa wanawake,wana mihemuko,kujiona wako juu,
Na wakishalewa ndiyo balaaa

RIP SIWETU FUNDIKIRA

ova
 
Kwanza nina imani dogo wa bajaj hakujua kama anaegombana nae ni mwanajeshi.

Pili katika maisha kuna kitu kinaitwa hasira haswa unapopigwa au kudhalilishwa mbele ya watu (kitendo cha mjeshi kumchapa dogo makofi mbele ya watu huku akijua fika kwamba yeye ndio mkosaji) kilimfanya dogo ahisi uonevu na udhalilishaji wa hali ya juu.

Mwisho kabisa dogo alichukua hatua ile kujihami maana huenda aliona angeendelea kupokea kipigo zaidi. Lkn pia naamini dogo hakujua kama kile alichofanya kujihami au kujinasua na kipigo kingesababisha kifo cha msoja.

Ndio maana siku zote tunaambiwa kuwa hasira ni hasara.
Wote hao hawajielewi hyo kanali na huyo jamaa wa bajaji
Mambo mengine ukikutana nayo ni kuachana nayo tu
Ukimya,kujishusha unaokoa mambo
Mengi sana

Ova
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
A Military with no Discipline is literally a bunch of Thugs
 
Wote hao hawajielewi hyo kanali na huyo jamaa wa bajaji
Mambo mengine ukikutana nayo ni kuachana nayo tu
Ukimya,kujishusha unaokoa mambo
Mengi sana

Ova
Kweli mkuu. Sema kanal ndio mkosaji mkuu. Kumpiga mtu mzima makofi sio jambo zuri, na ukizingatia siku hizi kila mtu anatembea na matatizo yake kichwani. So ukizingua na yeye anamalizia mwisho hasara kwenu wote wawili.
 
Back
Top Bottom