wanajeshi sio vichaa mpaka wawapige raia umejiuliza hili? kutakua na jambo raia wamewakosea tumia akili kidogo pia tambua jeshi ni jeshi raia ni raia
Na wewe pia tumia akili kabla ya kutetea jambo. Fuatilia kwanza chanzo cha tatizo kati ya mwanajeshi (kanal) na huyo raia ni nani alieanza kumchapa mwenzake makofi. Kwanza alivaa kiraia, hivyo dogo hakufahamu kama marehem ni mwanajeshi. Lakini pia sidhani kama wewe mtu mzima na familia yako unaweza kukubali, au kuruhusu mtu usiemfahamu akupige makofi barabarani mbele ya watu, huku aliekupiga akiwa yeye ndio mwenye makosa ya kupaki gari hovyo kwa sababu tu ya cheo chake.
Usifikiri pia raia ni mjinga, kwamba atoke huko alipotoka aache watu wote aliokutana nao barabara kilometa kibao, eti akamvamie tu mjeda bila sababu. Ukweli ni kwamba ni lazima kuna sababu ambayo imepelekea raia apate hasira na kuamua na yeye kujihami kwa silaha kama njia ya kulipiza kisasi kwa kile alichofanyiwa ambapo bahati mbaya kisasi hicho kikasababisha mauaji.
Nina imani ingekuwa raia ndio kamuanza mwanajeshi alaf mwanajeshi kampiga raia hadi kifo, hilo swala lingeisha kimya kimya na wala mtuhumiwa wa mauaji ya raia asingekamatwa kama alivyokamatwa raia. Hata mzazi wako aliekuzaa kuna umri fulani ukifikisha hawezi kukupiga hovyo barabarani. Kama kuna kosa umefanya ni lazima baba yako au mama yakoi atakwita myamalizie ndani. Sembuse mtu mliekumbana tu barabarani akupige makofi na wewe pengine una mke au mume na watoto nyumbani.
Kama hayajakukuta, au hayajamkuta ndugu yako, usipende kukimbilia kuwa defend wanajeshi kwa sababu ya magwanda yao. Kumbuka hao ni binadam kama ulivyo wewe na mimi. Hivyo wanaweza pia kukosea kama wakoseavyo binadamu wengine. Kuna video iliwahi kurushwa mitandaoni (kama uliwahi kuiona) askari trafiki alikuwa anamsimamisha mwanajeshi, ila yule mwanajeshi hakusimama badala yake akawa anaendelea kwenda mdogo mdogo huku akimpushi yule trafiki aliesimama mbele yake na gari lake.
Baada ya video kuvuja na watu kupiga kelele mitandaoni, ndo tukasikia kwamba yule askari amekamatwa kwa kosa la kumzuia yule trafiki kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria. Na hapo bado kuna matukio mengi tu ya jeshi kupiga raia kwa visingizio mbali mbali, alaf ukifatilia kwa kina sometimes unagundua kwamba sababu ni raia mmoja kutembea na demu wa mjeshi nk.
Nikija kwenye point ya kupiga watu. Kwanza kisheria dunia nzima hauwezi kumhukumu mtu kwa kosa la mungine. Ndo maana wewe leo ukimpiga mtu alaf ukakimbia askari hawawezi kuja wakamkamata kaka yako au mzazi wako kwa sababu ya kosa lako. Watachofanya ni kukutafuta wewe mwenyewe kwa kosa ulilofanya mwenyewe.
Sasa inashangaza jamaa wa bajaji (alieuwa) aishi zake msumi huko, aje zake Kawe kufuatilia mambo yake, akumbane na mwanajeshi, yatokee ya kutokea alaf jamaa akimbie zake kuelekea kwao Msumi, then jeshi lifike na kuanza kuwapiga raia hovyo, tena mbaya zaidi wengi wao hawakuwepo eneo la tukio na wengine hawakufahamu kilichotokea.
Jeshi linalopiga raia zaidi ya mia moja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja, ni sawa sawa na Hamas au Jeshi la Israel ambapo matatizo yao yamesababisha maelfu ya raia wa Israel na Palestina wengi wao ni wanawake na watoto kuuwawa bila sababu yoyote.
Wangetumia upelelezi wao kujua jamaa anaishi wapi, wamkamate na kumfikisha katika vyombo vya sheria, maana sheria zipo kwa ajili ya kutoa hukumu kwa kesi kama hizi.