Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Tangu lini hawa wanajeshi wanatulinda? Kazi yao ni kuning'iniza poumbou tu makambini huko. Sisi wananchi inajilinda wenyewe.
Wananing'iniza gololi tu, alaf jioni ndo wanakuja kuvamia maeneo ya wanyonge na kujifanya kina Rambo na Shwaznigga 😂😂😂
 
Mimi Nilikuwa nawapiga saana wanajeshi miaka hiyo huko 24Kj kigoma nimewapiga saana askari wa hicho kikosi aise mpaka ikafikia hatua

Sir meja
Luten kanal na KANAL wa hicho kikosi wakanitafuta nimalize tofauti zangu na askari wao
Kumbe ilikuwa hivyo mkuu, ama kweli uko vizuri.
 
Afisa ameuwawa baada ya kuleta utemi wa kishamba.

Kaziba barabara, dogo akamuomba kistarab tu afisa huyo apaki gari yake vizuri ili dogo apate njia ya kupita na bajaj yake. Ofisa kuona macho ya watu akaona kadharauliwa na kutembeza makofi kwa dogo.

Dogo nae hakupenda unyonge uendelee, ndo akachomoa cha mkunjo na kulenga sehemu husika iliyomuangusha ofisa na kupelekea kupotez maisha.
Mwisho wa Ubaya ni aibu.

Kwa yeyote yule anae zani ana nguvu/nafasi ya kuwaonea wanyonge lazima ajue kua mwisho wa ubaya ni aibu na itampata kweli.

Tanzania kuna Police, Mgambo na Wanajeshi wanatumia nafasi zao vibaya kuumiza raia.

Mbaya zaidi saiv watu wamevurugwa ukizingua wanakiwasha hapo hapo ndo utajua ujui
 
Mwisho wa Ubaya ni aibu.

Kwa yeyote yule anae zani ana nguvu/nafasi ya kuwaonea wanyonge lazima ajue kua mwisho wa ubaya ni aibu na itampata kweli.

Tanzania kuna Police, Mgambo na Wanajeshi wanatumia nafasi zao vibaya kuumiza raia.

Mbaya zaidi saiv watu wamevurugwa ukizingua wanakiwasha hapo hapo ndo utajua ujui
Kweli kbs mkuu, hawa vijana waliotembeza kipigo kwa kina mama na wazee, lazima kuna siku watalipwa na Mungu malipo yalio mabaya zaidi mpaka wajutie ujinga wao.

Time will tell...
 
Kiongozi kauwawa na mtu mmoja, lkn waliopigwa na kujeruhiwa ni zaidi ya watu mia moja, ambao hawakuwa eneo la tukio, na wala hawakuwa wanafahamu kilichotokea.

Wanakumbushwa kuwa walinzi wa maeneo yao, wasiruhusu bijana wahuni wahuni kuwepo mtaani.
 
Wanakumbushwa kuwa walinzi wa maeneo yao, wasiruhusu bijana wahuni wahuni kuwepo mtaani.
Jamaa ni dereva wa bajaj na hapo lilipotokea tatizo ni barabarani ambapo kila mtu kutoka mbagala, mw/nyamala, kinondoni, kimara nk anaweza kupita.

Kwa mantiki hiyo sio kila anaepita barabara hiyo watu wanamjua. Wengine wanaishi Buguruni lkn anaweza kupita hapo kwenda kumpeleka, au kumchukua mteja, sasa nyinyi raia wa kawaida mtajuaje kama dereva huyo ni muhuni.

Lakini pia chanzo cha ugomvi ni mjeda kupaki barabarani, lkn pia kumpiga jamaa makofi mbele ya watu bila sababu, hali iliyopelekea jamaa nae ajihami na kusababisha mauaji.

Dunia ya leo kila mtu anatembea na matatizo yake kichwani japo hatakwambia, sasa hauwezi kukurupuka na kuanza kumpiga makofi mtu mzima (pengine ana mke na watoto) kama mtoto wako tena mbele ya watu et kisa wewe ni kanal wa jeshi.

Ebu fikiria vizuri kama huyo kijana ndo angekuwa wewe ungejisikiaje kupigwa makofi barabarani kama mtoto mdogo na mtu usiemfahamu. Hata baba yako mzazi kuna umri fulani ukifikia hawezi kukupiga barabarani mbele ya watu, sembuse mtu tu uliekutana nae barabarani hamjua hakujui.

No that it was not fair.

Siungi mkono kijana kumuua kanal, japo inaonesha hakuua kwa kukusudia maana alikuwa anapita zake. Lakini pia siungi mkono kitendo cha kanal kumchapa makofi jamaa, pia kitendo cha jeshi kupiga raia ambao hawakuwepo wala kuhusika eneo la tukio sio cha kiungwana hata kidogo.
 
Afisa ameuwawa baada ya kuleta utemi wa kishamba.

Kaziba barabara, dogo akamuomba kistarab tu afisa huyo apaki gari yake vizuri ili dogo apate njia ya kupita na bajaj yake. Ofisa kuona macho ya watu akaona kadharauliwa na kutembeza makofi kwa dogo.

Dogo nae hakupenda unyonge uendelee, ndo akachomoa cha mkunjo na kulenga sehemu husika iliyomuangusha ofisa na kupelekea kupotez maisha.
duh
 
Duh! Kumbe mshikaji hata mbingu za combat karate hana halafu analeta ubabe?
Hii ni warning kwamba wasipende kuwa wanavamia na kuwaonea raia.

Kuna wengine wamevurugwa na maisha, hivyo ukimchokoza haoni hasara kuchukua hatua yoyote ili mradi hakubali kufanywa mnyonge nchini kwake.
 
we kenge mkaiheshimu jeshi, kaa mbali na wanajeshi. Mmezidi kuwawajuaji, hata hapa umeandika utumbo we hujui majukumu ya jeshi. Mnapimana nguvu na wanajeshi. Mbona wapumbavu hivyo? Au ulifikiri jeshi km hicho chama chenu ambapo mmezoea malamishi na uwongo? Mi naona hao wanajeshi wa Kawe ni wastaarabu sana, ingekuwa makambi mengine leo hii kusingelikuwa na kijana wa kiume hapo kawe. Mnamwua mwanajeshi? Kweli halafu unakuja kuandika humu bila hata haya? Nyie ni vile vitoto vya single mothers, Pumbav kabisa
We lazima utakua mjeda tu si kwa hilo povu..
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
wanajeshi sio vichaa mpaka wawapige raia umejiuliza hili? kutakua na jambo raia wamewakosea tumia akili kidogo pia tambua jeshi ni jeshi raia ni raia
 
We lazima utakua mjeda tu si kwa hilo povu..
Huyo kweli ni mjeda, tena anaonekana ni wale wanaopakatwaga na ma MP wa jeshi, alaf hasira zake anakuja kuzimalizia huku JF 😂😂😂
 
wanajeshi sio vichaa mpaka wawapige raia umejiuliza hili? kutakua na jambo raia wamewakosea tumia akili kidogo pia tambua jeshi ni jeshi raia ni raia
Na wewe pia tumia akili kabla ya kutetea jambo. Fuatilia kwanza chanzo cha tatizo kati ya mwanajeshi (kanal) na huyo raia ni nani alieanza kumchapa mwenzake makofi. Kwanza alivaa kiraia, hivyo dogo hakufahamu kama marehem ni mwanajeshi. Lakini pia sidhani kama wewe mtu mzima na familia yako unaweza kukubali, au kuruhusu mtu usiemfahamu akupige makofi barabarani mbele ya watu, huku aliekupiga akiwa yeye ndio mwenye makosa ya kupaki gari hovyo kwa sababu tu ya cheo chake.

Usifikiri pia raia ni mjinga, kwamba atoke huko alipotoka aache watu wote aliokutana nao barabara kilometa kibao, eti akamvamie tu mjeda bila sababu. Ukweli ni kwamba ni lazima kuna sababu ambayo imepelekea raia apate hasira na kuamua na yeye kujihami kwa silaha kama njia ya kulipiza kisasi kwa kile alichofanyiwa ambapo bahati mbaya kisasi hicho kikasababisha mauaji.

Nina imani ingekuwa raia ndio kamuanza mwanajeshi alaf mwanajeshi kampiga raia hadi kifo, hilo swala lingeisha kimya kimya na wala mtuhumiwa wa mauaji ya raia asingekamatwa kama alivyokamatwa raia. Hata mzazi wako aliekuzaa kuna umri fulani ukifikisha hawezi kukupiga hovyo barabarani. Kama kuna kosa umefanya ni lazima baba yako au mama yakoi atakwita myamalizie ndani. Sembuse mtu mliekumbana tu barabarani akupige makofi na wewe pengine una mke au mume na watoto nyumbani.

Kama hayajakukuta, au hayajamkuta ndugu yako, usipende kukimbilia kuwa defend wanajeshi kwa sababu ya magwanda yao. Kumbuka hao ni binadam kama ulivyo wewe na mimi. Hivyo wanaweza pia kukosea kama wakoseavyo binadamu wengine. Kuna video iliwahi kurushwa mitandaoni (kama uliwahi kuiona) askari trafiki alikuwa anamsimamisha mwanajeshi, ila yule mwanajeshi hakusimama badala yake akawa anaendelea kwenda mdogo mdogo huku akimpushi yule trafiki aliesimama mbele yake na gari lake.

Baada ya video kuvuja na watu kupiga kelele mitandaoni, ndo tukasikia kwamba yule askari amekamatwa kwa kosa la kumzuia yule trafiki kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria. Na hapo bado kuna matukio mengi tu ya jeshi kupiga raia kwa visingizio mbali mbali, alaf ukifatilia kwa kina sometimes unagundua kwamba sababu ni raia mmoja kutembea na demu wa mjeshi nk.

Nikija kwenye point ya kupiga watu. Kwanza kisheria dunia nzima hauwezi kumhukumu mtu kwa kosa la mungine. Ndo maana wewe leo ukimpiga mtu alaf ukakimbia askari hawawezi kuja wakamkamata kaka yako au mzazi wako kwa sababu ya kosa lako. Watachofanya ni kukutafuta wewe mwenyewe kwa kosa ulilofanya mwenyewe.

Sasa inashangaza jamaa wa bajaji (alieuwa) aishi zake msumi huko, aje zake Kawe kufuatilia mambo yake, akumbane na mwanajeshi, yatokee ya kutokea alaf jamaa akimbie zake kuelekea kwao Msumi, then jeshi lifike na kuanza kuwapiga raia hovyo, tena mbaya zaidi wengi wao hawakuwepo eneo la tukio na wengine hawakufahamu kilichotokea.

Jeshi linalopiga raia zaidi ya mia moja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja, ni sawa sawa na Hamas au Jeshi la Israel ambapo matatizo yao yamesababisha maelfu ya raia wa Israel na Palestina wengi wao ni wanawake na watoto kuuwawa bila sababu yoyote.

Wangetumia upelelezi wao kujua jamaa anaishi wapi, wamkamate na kumfikisha katika vyombo vya sheria, maana sheria zipo kwa ajili ya kutoa hukumu kwa kesi kama hizi.
 
Back
Top Bottom