Tuhuma za Kabendera dhidi ya Magufuli na ukimya wa Kikwete. Je, tuamini ni kweli?

Magufuli anasingiziwa kila baya ila watanzania wamegoma kumchukia
Watanzania walio wengi wenye akili waliujua ubaya wa Magufuli tangu akiwa hai, hawahitaji kuambiwa na mtu.

Wanancji wa Nyanda za Juu Kusini wanajua jinsi mbao zao na mahindi yalivyokosa soko mpaka kufikia gunia la mahindi la kilo 100 kuuzwa kwa sh 20,000 utokana na Magufuli kuharibu mahusiano mazuri ya kibiashara yaliyokuwepo kati ya Kenya na Tanzania.

Kanda ya Kaskazini wanaujua ubaya wa Magufuli kwa jinsi walivyoshuhudia namna biashara ya utalii ilivyokuwa imeanguka na TRA walivyoweza kuwababikizia kesi wafanyabiashara na kufunga biashara zao.

Kanda ya Kusini wanaujua sana ubaya wa Magufuli jinsi alivyoua biashara ya korosho.

Tanzania nzima wafanyabiashara na wawekezaji kwenye sekta ya mahoteli wanajua Magufuli alivyoua biashara zao.

Wanasiasa wanajua jinsi ambavyo Magufuli alivyowanyima uhuru, na kuua kabisa demokrasia.

Watanzania wote wenye akili timamu na waeio wanafiki wanajua namna marehemu alivyoporomosha ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%; ukuaji wa sekta ya utalii alivyouporomosha toka 15% mpaka 3.6%. Wanajua namna alivyoua utawala wa sheria, wanajua alivyoua demokrasia.

WanaCCM wanajua namna Magufuli alivyoua demokrasia ndani ya chama kwa kupachika majina ya wagombea aliowataka bila ya kujali wala kuongozwa na kura za maoni.

Watanzania wanamfahamu Magufuli namna alivyokuwa dikteta, alivyokuwa mpenda sifa, na asiyekubali kukosolewa kwa lolote.
 
Chukua Mo Energy hapo kwa Mpare.

Nimeikumbuka ile Hilux Surf ya Mombo leo
 
Tuhumu nyingi ni za uongo.Ndio maana hazimalizi siku tatu.Hii inatokana kuwa Watanzania wengi wanapenda story za uongo na za kupuuzi.Hawapendi kazi .Na hata ww mleta mada unapenda story za kipuuzi na kijinga.Magufuli hayupo duniani.Lakin alifanya makubwa sana kiasi kwamba wapumbavu wote wanataka kumchafua .Wakati wao hawajawahi kufanya cha maana zaidi ya story za kihuni na kioumbavu Kama hizi.
 
Tuhumu nyingi ni za uongo.Ndio maana hazimalizi siku tatu.Hii inatokana kuwa Watanzania wengi wanapenda story za uongo na za kupuuzi.Hawapendi kazi .Na hata ww mleta mada unapenda story za kipuuzi na kijinga.Magufuli hayupo duniani.Lakin alifanya makubwa sana kiasi kwamba wapumbavu wote wanataka kumchafua .Wakati wao hawajawahi kufanya cha maana zaidi ya story za kihuni na kioumbavu Kama hizi.
 
 
Kwa hiyo wewe kwa unavyomjua JK hawezi kufanya hivyo? Yaani from nowhere tu jiwe ambananishe mtu. Mbona anajua gesi ya mtwara iliuzwa na hatuna chetu iweje asimkamatie hapo
 
We nae kiazi yaani madhara ya Corona kwenye uchumi unakuja kusema Magufuli alisababisha. Hebu fafanua aliuaje utalii kwa mfano. Mmeshasahau enzi za JK tembo walivunwa hadi wakataka kuisha
 
Jiwe alikuwa ni ibilisi mwenye sura ya binadamu.
 
Unataka kikwete akanushe wakati yeye ndo muwindwa,mwambie kabendera athibitishe tuhuma zake. We wa wapi?
 
Na wewe umeamini huo utopolo wa Kabendera?
Hata kama Magufuli alikuwa dikteta lakini kwa hili atakuwa anasingiziwa.
Kwani katiba ya kutoruhusu Rais mstaafu asishtakiwe ingebadilishwa?
Kwa hili tu,nadiriki kusema huu ni utopolo..
Hata hivyo sio kila kitu ni cha kujibu kwa watu wakubwa kama kina Kikwete
 
Jaribu kumkosoa huyo mama ako uone. Muulize ndugai.
 
Kwa hiyo wewe kwa unavyomjua JK hawezi kufanya hivyo? Yaani from nowhere tu jiwe ambananishe mtu. Mbona anajua gesi ya mtwara iliuzwa na hatuna chetu iweje asimkamatie hapo
Watu mlijazwa ujinga sana na Jiwe... Gesi ya Mtwara ipi?! Kama ni ile ambayo inazalisha umeme Kinyerezi, ile ilianza kuchimbwa wakati wa Mkapa, na shareholder mkubwa alikuwa Artmus.

Baada ya Artmus kufungasha virago, nae akawauzia investors wengine huku TPDC akibakiwa some percentages kwa niaba ya serikali!

Kama ni gesi iliyogunduliwa zama za JK, hadi sasa haijachimbwa hata tone. Sasa gesi unayoisema wewe ni ipi?! Na kwavile JPM aliwadanganya gesi yote imeuzwa, sasa jitihada zilizokuwa zinafanywa na serikali yake kutaka kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia hao walionunua hiyo gesi, ama?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…