Watanzania walio wengi wenye akili waliujua ubaya wa Magufuli tangu akiwa hai, hawahitaji kuambiwa na mtu.
Wanancji wa Nyanda za Juu Kusini wanajua jinsi mbao zao na mahindi yalivyokosa soko mpaka kufikia gunia la mahindi la kilo 100 kuuzwa kwa sh 20,000 utokana na Magufuli kuharibu mahusiano mazuri ya kibiashara yaliyokuwepo kati ya Kenya na Tanzania.
Kanda ya Kaskazini wanaujua ubaya wa Magufuli kwa jinsi walivyoshuhudia namna biashara ya utalii ilivyokuwa imeanguka na TRA walivyoweza kuwababikizia kesi wafanyabiashara na kufunga biashara zao.
Kanda ya Kusini wanaujua sana ubaya wa Magufuli jinsi alivyoua biashara ya korosho.
Tanzania nzima wafanyabiashara na wawekezaji kwenye sekta ya mahoteli wanajua Magufuli alivyoua biashara zao.
Wanasiasa wanajua jinsi ambavyo Magufuli alivyowanyima uhuru, na kuua kabisa demokrasia.
Watanzania wote wenye akili timamu na waeio wanafiki wanajua namna marehemu alivyoporomosha ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%; ukuaji wa sekta ya utalii alivyouporomosha toka 15% mpaka 3.6%. Wanajua namna alivyoua utawala wa sheria, wanajua alivyoua demokrasia.
WanaCCM wanajua namna Magufuli alivyoua demokrasia ndani ya chama kwa kupachika majina ya wagombea aliowataka bila ya kujali wala kuongozwa na kura za maoni.
Watanzania wanamfahamu Magufuli namna alivyokuwa dikteta, alivyokuwa mpenda sifa, na asiyekubali kukosolewa kwa lolote.