DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hivi unamjua Adinani kwenye story hii.?
Adivasi ni mfanyakazi mpiga dili tu na target ya boss ilikuwa kumuua Adinani bali alikosea akamchapa mlinzi wa kilungu....soma vizuri
Bado kesi ya kuua iko palepale iwe adinani au mlinzi sio sawa.
Mlinzi nae alikua mwizi tu alifata nini upande ule aliokuwepo adinani anafanya wizi
 
Mkuu jela pasikie kwenye redio tu.
Umeshaingizwa mahabusu ya Buguruni mkuu? Ile ni jehanam +++
Niliwai lala pale aisee,
Wale watu walitoka kufanya patrol kule nyuma ya Sewa wamekamata wahuni kibao wanarudi nao.
Sina hili wala lile nangoja daladala la gomz pale sokoni wakaniunganishia funga shati huyo.
Nikajikuta kituoni najieleza wapi,
Nikasachiwa wakakuta hela nyingi tu.
Tupa ndani,usiku kucha ikawa ni ndani nje tunadiscuss rushwa.
Mi nagoma kwamba sina kosa inakaribia asb wakachukua buku 40 wakarudisha zingine,
simu motorola vile vidogo slide silver enzi hizo wakalamba.
Wale mbwa mungu awalaani huko waliko hata km wamekufa.
Ile hela walichukua ilikua nimpelekee bi mkubwa usiku ule ya sikukuu na matumizi mengine badae kashangaa nafika asubuhi nalia tu .
Nikamweleza kilichotokea tukasikitika tu.
Sikupita ile njia miaka mingi Sana.
 
Ndiyo maana hawa jamaa wa MGas huduma imekuwa mbovu sana, kuishiwa gas walikuwa wanakuletea kabla haijakata sasa hivi inakata ndiyo wanaoleta,

Wateja kibao wanataka huduma ila vifaa hawana.

Kifupi ufanisi umepungua
Ndio upuuzi wa waafrica mkuu.
Huyo bilionea uchwara, kaanzisha mradi umekubalika vizuri kapata visenti kidogo kaanza kuua watu.
Uko mbele angefanyaje.
Huku tayari biashara inayumba.
Partners badala wakae nae kujadili kukuza biashara wanaanza kuhangaika kumtoa mahabusu.
 
Pole sana Mkuu, tumshukuru Mungu kwa kila Jambo, Dunia ina mitihani mingi sana!!
 
Duh pole sana,waliyokufanyia hivyo
Lazima sahivi hawapo au wamekufa ,kama wapo watakuwa wanaishi maisha mabovu

Ova
 
The point is bila pombe asingefanya hilo jambo
 
Ameharibu furaha yake kwa hasira za kijinga.
 
Mbona kesi YA Mbowe ilikuwa inajadiliwa kila kona
 
Asante kwa taarifa mkuu naongezea
Aliyeuwawa Alikuwa mtu wa Tanga Lushoto Bumbuli na siyo Muheza
Baada ya polisi kufanya ngonjera taarifa zikamfikia bwana Ramadhani Kingai DCI yeye pia wa BUMBULI na ndiye aliyepigilia msumari wa mwisho hadi Adrian kudakwa
Katika hili pia wapewe shukrani wabunge wote wa mkoa husika kwani walitoa ushirikiano mkubwa sana
special thanks to JANUARI MAKAMBA and UMMY MWALIMU
 
Hakika ametumia muda mwingi, hii story mwenyewe nilikuwa nayo japo siyo kama ulivyoisimulia. kuna baadhi ya info nilikuwa sina. kilichonishinda kuzipata na kupost ni muda. japo sisemi alipwe au laah
 
Alikuwa anafanya kazi TRA huko ndio alipiga hela akaacha kazi ili aendeleze kopa gas yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…