DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sema nini mwamba awape mzigo mrefu familia na wao wakubali kama fidia mambo yaishe tu.
Ukishampeleka jela ndio marehemu atarudi? By the way kwa li-nchi hili la u-ovyoovyo wakikaza fuvu hawatapata haki yoyote. Hata ningekua mimi ningepambana yaishe nisiende jela nani anataka kwenda jela.
Watabaki kushindana kwenye ndumba tu wakikaza fuvu mambo ya mahakamani.
Tatizo alienda kutupa mwili huko msituni
 
Haki haipotei, unaweza kuhonga Polisi unavyotaka lakini taarifa zote zitakuwa salama sehemu ili siku haki itendeke. Huwezi kukimbia jinai haifi hata uhonge vipi.

kosa la mwamba sio zito kusababishia laana ama malipo baadae maana aliua kwa bahati mbaya.

kosa lake liko kisheria zaidi kwamba aliitupa maiti,so uwezekano wa kuliweka mezani hili swala ni mkubwa,hasa kama itahusika zaidi kuwapoza wategemezi wa marehem.
 
Sawa kakosea history yake vipi na Hilo tukio kakosea ?
Kakosea sehemu kuu tatu:
1. Aliposoma
2. Kwamba hiyo Sio Mara yake ya kwanza!
Kama yawezekana angetuletea na matukio yake mengine na aliowaua ili nasi tufahamu majina yao! (Huwezi andika kwa uma kitu usichokithibitisha)
3. Kwamba ukoo wake wote huko Babati una historia ya hasira kali.
 
Naomba jina la Twitter lenye hyo story mkuu .... na km Andron sie aliyefyatua risasi why afiche .... na Adinani alipata wapi hyo silaha ya kumuua mlinzi....Naona ndugu Adnani anataka kuangushiwa jumba bovu apo....pesa inataka kufunika mambo
Weee ujaelewa uzi. Adinan ni mwendesha pikipiki ialiyekuwa antibacterial gas na kuwauzia vibopa. Tajiri aliweka mtego amuse lakini bahati mbaya akamuua mlinzi
 
jamaa wamuheza haki isipotendeka tunguli lazima zifanye kazi pale Bonde au watasogea kwa ndugu zao wa kicheba.

Adron ni Mpumbavu fulani pamoja na akili zake za darasani lakini akili za kimtaa hana na ndio akili muhimu zinazoweza kukufanya ukaishi salama duniani, ukiona unatabia yakuonyesha onyesha bastola hovyohovyo hadharani na kutishia watu ujue wewe ni PUMBAVU NA MSHAMBA mmoja hivi.
Wabondei lazima walale nae mbele
 
Hii kesi ni kubwa,lakini kwa bongo ya michongo,itamalizwa faster!!kama kesi ya Yule Binti aliyeua mama yake akamfukia uhani,DPP aliishia kusema"serikali Haina Nia ya kuendelea na kesi"Binti akawa huru!sasa hv anakula maisha na mganga wake walieshirikiana kuua,
Kwahiyo mganga alifanya yake? Lakini hizo raha zitakuwa za muda tu nakwambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli huyu mwandishi anapotosha sana, bwana Andron nimefanya nae kazi kampuni flani ya Insurance akiwa mhasibu pale Mikocheni kabla hajawa Billionaire, alikuwa humble person wala sio mlevi au mtu wa hasira kama anavyosema huyu mwandishi uchwara labda kama pesa imembadilisha sasa.!
Kwani kabadilika tabia kunachukua siku ngapi? Ulifanya naye kazi vipi alivyopata ubilionea ulikuwa naye tena? Kabla ya tuhuma tuliza mungari wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara ya mwisho ni lini kuonana na Bilionea? Katika hii dunia usibishe kila jambo linawezekana na tabia kubadilika ni kitu kidogo sana. Kabla haujaanza kukashfu mtoa taarifa ungejiongeza kupata taarifa zaidi. Kama Mendez alikuwa rafiki yako na wewe unatabia hizi sioni cha ajabu Mendez kuua.
Ndiyo hao akipelekewa tuhuma za mtu wake wakaribu anakataa mpaka siku akute kachomwa moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba jina la Twitter lenye hyo story mkuu .... na km Andron sie aliyefyatua risasi why afiche .... na Adinani alipata wapi hyo silaha ya kumuua mlinzi....Naona ndugu Adnani anataka kuangushiwa jumba bovu apo....pesa inataka kufunika mambo
Pesa Mzee ni kila kitu
 
Kampuni ya Ulinzi (HOMASA SECURITY) inapata bahati ya kuingia mkataba na Bilionea ANDRON MENDES

Mkataba huu unahusisha kumlinda Bilionea huyu nyumbani kwake na Pia kulinda kwenye ofisi ilipo kampuni yake ya KOPA GAS huko maeneo ya Skansca Tegeta karibu na IPTL
Bilionea huyu wa kitanzania alipiga “mshindo” wa kutakata baada ya kugundua tekinolojia ya “Lipa kadiri unavyotumia” (Pay as you go) Katika matuzi ya gesi za kupikia hasa majumbani.

Yaani unaweza ukanunua hata gesi ya buku moja, Sio lazima uwe na pesa ya limtungi looote la gesi

Ugunduzi huu unawavutia kampuni ya Uingereza ya CIRCLE GAS kununua technology wakishirikiana na Safaricom ili tekinolojia hii itumike kenya pia.

Deal hili linageuza kabisa maisha ya ANDRON MENDEZ akiwa na umri wa miaka 35.

Tarehe 20 November 2022

Saa 4 Usiku, Katika ofisi za KOPA GAS, anafika pale mmiliki wa ofisi ile bwana ANDRON MENDES aliwa na mkewe kwa kutumia gari aina ya Toyota Harrier Nyeusi yenye namba za usajili T 698 DRN

Anaonekana akiwa “Matingas” kwa sana.

Na anafika hapa baada ya ujumbe ambao mkewe alikuwa ametumiwa kwenye simu yake kutoka kwa kichomi kumuhusu mfanyakazi wao aitwaye ADINAN almaarufu kama “Uchebe”

Huko ndani watu wanaendelea na kazi zao yaani wako busy kama vile mchana wakipakua mitungi mitupu ya gas na kupakia iliyojazwa kwa ajili ya wateja.

Ndani kuna walinzi wawili.

Mwenye bunduki aliyepo Getini na mwenye kirungu aliye ndani kabisa inapofanyika kazi.

Mara Unasikika mlio wa risasi kwa nje.

Wote waliokuwa wanafanya kazi ndani wakaganda kama vinyago.

Mkao wa kimasta kusikilizia kuna nini huko nje?

ANDRON akaenda getini na kumtaka mlinzi amfungulie.

Kwa kuwa yule ndio mwenye ofisi, mlinzi akamfungulia mlango bila ubishi

ANDRON akafika katikati ya eneo la biashara yake (Godown lenye ukubwa kama nusu ya playground)

Pale katikati kuna mitungi ya gas lakini pale tena akafyatua risasi nyingine hewani.

Wafanyakazi wakaona huu mzaha sio mzaha, Kila mmoja alishindana na mwenzake mbio kutoka nje.

Dakika chache wakiwa nje ukasikika tena mlio mwingine wa risasi huku ikisikika sauti ya mkewe akisema “Andron Usimuue usimuue”

Sasa Andron akawa ameshafika kwenye eneo la kibanda cha mlinzi alipokuwa amekaa yule mlinzi mwenye siraha.

Akamwamuru aweke chini Bunduki.

Mlinzi kwa kujua Mteja wao hayuko tena kwenye masihala

Akagoma kuachia bunduki lakini akakimbilia nje huku akiwa amesahau simu yake kwenye kibanda chake.

Akaenda zilipo Ofisi za N Gas maeneo ya karibu na pale kuomba msaada wa simu awataarifu waajiri wake kilichojili.

Alifanikiwa kutoa taarifa na kurudi lindoni kwake ambapo hakumkuta Andron wala Mkewe.

Alipoingia getini mbele kidogo akaona dimbwi la damu hali hiyo ikamshtua akaanza kumtafuta mlinzi mwenzake kimya kimya bila kutoa sauti.

Alipomkosa akaanza kumuita kwa sauti bila mafanikio

Akaenda getini na kuchukua simu yake ili ampigie huyo mlinzi mwenzake.

Alipopiga simu, Simu ikapokelewa lakini ikaachwa hewani bila yeyote kuzungumza.

Baadae simu hii ikazimwa kabisa.

Baada ya kama Dk 20 ANDRON akarudi na kumtaka mlinzi afukie ile damu na atambadilishia maisha.

Mlinzi akataa lufuta damu asizojua ni za nani.

Baada ya muda Operesheni Manager wa ile kampuni ya ulinzi akafika pale na akawa anamhoji mlinzi aliyekuwepo nini kimejiri.

Muda ule ule Mkurugenzi bwana JOE wa kampuni ya ulinzi naye akafika na kumfata ANDRON

Akamuuliza Andron kuna shida gani pale?

Andron akajibu hakuna shida kuna mambo tu anaweka sawa.
Wakamhoji ile damu pale ndani ni ya nini na mlinzi mwenzao yuko wapi?

Badala yake Mkurugenzi akajibu kuwa Kuanzia siku hiyo hataki huduma za ulinzi kutoka kwao.

Akaondoka

Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi akaamuru ulinzi uinarishwe pale kwani hawezi kuacha lindo kiholela

Kisha yeye na Yule mlinzi aliyekuwepo tukioni na OP manager wakaongozana kwenda kituo cha polisi Wazo Hill.

Ajabu wakamkuta ADRON pale polisi.

Viongozi wa Kampuni ya Ulinzi walimkuta Andron akitoa maelezo lakink wao walipofika Mkurugenzi huyo akaacha kutoa maelezo mapaka watolewe nje wale watu wa kampuni ya Ulinzi.

Kweli bwana!

Viongozi wale wa kampuni ya ulinzi wakatolewa nje hivyo Andron akaendelea kutoa maelezo ndani akiwa peke yake.

Alipomaliza kutoa maelezo Polisi, Viongozi wa HOMASA SECURITY na Andron wakaongozana kwenda eneo la tukio.

Kule wakakuta damu na kuokota maganda matatu ya risasi.

Timu nzima ikarudi tena polisi kituoni.

Andron akaambiwa asalimishe silaha iliyotumika ambapo baada ya kuulizwa juu ya umiliki wake akasema siyo ya kwake bali ni ya mkewe. Alipoulizwa nani alifyatua risasi? Androni akakili ni yeye ndiye aliyefyatua japo sio mmiliki wa silaha ile.

Kisheria hili tayari ni kosa la Kwanza.

Andron akasema kuwa silaha ile ina risasi 15 na yeye alifyatua tatu hewani.

Katika hali ya kushangaza polisi wakawataka wote, Yaani Andron, Mkewe na Viongozi wa Homasa Security kuondoka na warudi kesho yake asubuhi.

Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakahoji inawezekana vipi watu ambao ni wanatuhuma kubwa ya uhalifu kama ile waruhusiwe kuondoka?

Yaani mtu afyatue risasi, kisha mlinzi mmoja apotee asijulikane alipo na zinakutwa damu zisizo na maelezo ya kutosha kama ni za binadamu au mnyama na zaidi ya yote gari iliyotumika kwenye eneo la tukio waachiwe washukiwa kuondoka nalo?

Ndugu msomaji, Pesa ina nguvu bwana!

Polisi wakawajibu kuwa swala lile bado liko kwenye uchunguzi na hakuna mshukiwa hivyo waondoke na warudi kesho yake kufungua kesi.

Usiku wa deni haukawii!

Kesho yake majira ya saa 3 asubuhi viongozi wa Homasa Security walifika pale kituoni lakini cha ajabu si bwana Andron au mkewe walikuwa wamefika kituoni.

Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakatoa maelezo yao na pia wakataka gari iliyokuwa eneo la tukio ifikishwe pale kituoni.

Polisi wakawa wanampigia simu bwana Andron, Sio kwamba aende yeye kituoni na mkewe kama walivyoamuru jana, bali walimtaka apeleke pale kituoni gari kama inavyotakiwa na walalamikaji.

Ukwasi una nguvu ya ajabu sana!

Andron hakutokea tangu apigiwe simu saa 3 ile asubuhi mpaka alipopeleka gari saa 10 jioni.

Lazima hapa katikati alikuwa katika harakati za kuficha ushaidi.

Naam! utamweleza nini mtuhumiwa huru?

Sasa ndugu Andron alikuwa ni kama mtu ajifichaye kwenye jani la tembele akiamini amepata maficho ya kutosha.

Kwa nini nasema hivi?

Ni kwamba pale kituoni alienda na gari Toyota Harrier New Model nyeusi yenye namba za usajili T 605 DXG akidai ndio iliyokuwa tukioni.

Alikuwa amesahau kabisa kuwa Kampuni iliyokuwa ikimlindia ofisi ndiyo ilikuwa ikilinda nyumbani kwake hivyo ilikuwa inayajua magari yake yote.

Viongozi wa kampuni ya Ulinzi wakasema gari ile siyo ambayo ilikuwa tukioni.

Cha ajabu bado bwana Andron aliachiwa kuondoka huru kabisa akiwa na gari ile aliyokwenda nayo.

Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakajiaminisha kabisa haki haitatendeka pale katika kituo cha polisi Wazo.

Wakaamua kwenda kushitaki katika kituo kikubwa cha Mabwepande.

Polisi wa Mabwepande wakaenda kumkamata bwana Andron pia wakaipeleka gari zote mbili, Iliyokuwa kituoni na ile aliyoipeleka awali kituo cha Wazo.

Tarehe 24 November 2022 jalada la kesi ile likahamishiwa kituo cha polisi Oysterbay.

Hivyo Andron naye akahamishiwa kituo kile.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kichomi wangu ambaye alikiwa amewekwa korokoroni pale kituoni cha Oysterbay anadai Kituo kilikiwa kinajaa wazungu wengi kwenda kumuona Andron.

Aliponiuliza ni kwa nini nikampa inawezekana kutokana na sababu mbili

Andron anamiliki kampuni ya KOPAGAS pamoja na mbia mwenzake ambaye ni raia wa Mexico hivyo inawezekana wazungu wale wakawa ni jamaa wa mbia mwenzake.

Pia kampuni ya CIRCLE GAS ambayo ilinunua teknolojia yao ni kampuni ya Uingeleza hivyo labda wazungu wale wakawa ni sehemu ya watu wanaofanya nao biashara.

Basi kichomi huyu akadai kuwa kuna mazingira ya ushawishi mkubwa wa pesa unaoendelea pale lakini ni kama haelewielewi. (Nitafafanua mbeleni)

Lakini kichomi huyu akanipa taarifa zilizofanya nishtuke.

Alinieleza kuwa alikuwa anamuona mke wa Andron akienda kumuona mmewe pale polisi kwa nyakati tofauti na kuondoka.

Nikashangaa inakuwaje mwanamke huyu anakuwa huru uraiani? Huyu naye alipaswa kuwa ndani kwa sababu:
Alikiwepo kwenye tukio

Gari iliyotumika kwenye tukio ni mali yake

Bastora iliyotumika ni mali yake

Wakati haya yanaendelea, Zikaibuka habari mpya in connection with the case in question.

Kuwa tarehe 21 November 2022, Huko maeneo ya Vikawe mkoani Pwani, Msamalia mwema aliuona mwili wa binadamu asiye na uhai ukiwa umetelekezwa katika msitu wa Vikawe.

Taarifa hizi alienda kuzitoa katika kituo cha polisi Kibaha.

Polisi walipofika walikuta mwili ule ukuwa na jeraha kichwani lililosadikika kutokana na risasi.

Baadae mwili ule uligundulika ni wa yule mlinzi wa Kirungu aliuekuwa akilinda katika kampuni ya KOPAGAS ambaye alitoweka siku ya tukio.

Mlinzi yule alifahamika kwa jina la SALIM ALY HAJI

Mmiliki wa kampuni ya Homasa baada ya kuutambuka mwili ule aliwajulisha ndugu wa marehemu akiwemo mkewe.

Marehemu alikuwa anatokea wilaya ya Mheza mkoani Tanga.

Naamini ndugu msomaji mnaijua tabia ya watani zangu wasambaa wanavyopenda kesi.

Basi ndugu wa kisambaa wakawa wanajaa pale kituo cha Oysterbay kutaka haki juu ya ndugu yao kutendeka.

Yaani jitihada za kuifinika kesi ile zikawa zinazidi kuwa ngumu kwani ndugu hawa walikuwa wanaenda kwa shift pale kituoni.

Kichomi mmmoja akanitonya kuwa mmoja wa ndugu wale aliitwa ofisini ndani ya kituo cha polisi na kuonyeshwa maburungutu ya manoti kuwa awashawishi wenzake wafunge mdomo.
Kwa hiyo kulikiwa na nguvu kubwa iliyokuwa ikitumika kutaka kuzika kesi hii kuanzia kule Mabwepande mpaka Oysterbay ndio maana wazungu walikuwa hawaishi kituoni.

Kwa mujibu wa mmiliki wa Kampuni ya Homasa Bwana Jose Mangesho ni kwamba bwana Andron alifungia sana Kibubu kwenye kila kituo alichopelekwa.

Sasa turudi tena kwenye siku ya tukio.

Ni ujumbe gani aliotumiwa mke wa Andron hadi kusababisha kadhia hii?

Hapa inabidi kumtambua mfanyakazi wa KOPAGAS aitwaye ADINAN aka Uchebe.

Huyu alikuwa ni dereva wa pikipiki zilizokuwa zinatumika kusambaza gesi za KOPAGAS kwenda kwa wateja wao mbalimbali.

Mle ndani ya eneo la KOPAGAS, Kulikuwa kunapakiwa pia magari aina ya Virikuu ambavyo vilikiwa vinabeba mitungi mitupu ya kampuni ya Oryx Gas

Sasa Adinan alikuwa ni ntu ya dili

Ukiachana na kuwa ntu ya dili alikuwa pia na tabia za ubabe, kwani alikiwa akiishia kuwapa wenzake afutatu akishamaliza kupiga matukio yake.

Adnani alikiwa akiishi nyumba moja na jaaa fulani ambaye huyu naye alimletea ubabe wa kumpa afutatu kwenye dili fulani la majiko ya Gas waliyokuwa wamepiga.

Mtu huyu aliyedhurumiwa ndiye aliyekuja baadae kuwa Kichomi wa Adnani kwani alikuwa anaijua michongo yake yoye.

Alikuwa anajua kuwa Adnani alikiwa akiingia Godown Usiku akiwa na pipes ambazo alikuwa akizitumia kunyonya gesi kutoka kwenye mitungi ya M-Gas na kuihamishia kwenye mitungi mitupu ya kilo sita ya kampuni ya Oryx.

Kampuni ya M-Gas ni kampuni tanzu ya kampuni ya Circle Gas yaani wale walionunua tekinolojia ya Kopagas.
Hii ina maaana Adinani alikuwa akimuibia boss wake.

Katika dili hili Adinani alikuwa akipozwa na anawowawekea gesi.

Sasa siku ya siku ndio kichomi akatuma Sms kwa mke wa Andron kumjua kuwa Adinani yupo site akiendeleza wizi ule.

Mkewe alitumiwa sms ile kwa kuwa ni yeye ndiye anahusika na issues zote za store.

Message ile ikasomwa na Andron mwenyewe.

Sasa unaambiwa Andron si yeye tub ali ukoo wao mzima huko Babati una hulka ya hasira kali.

Akachukua bastora akaondoka na mkewe kwenda tukioni.

Huko katika harakati za kupiga chuma Adinani ndio akakosea na kumlipua mlinzi.

Kosa lake kubwa likawa ni kwenda kuficha maiti uko porini kibaha.

Na mkewe ndiye aliyanyoosha maelezo haya polisi siku moja baada ya yeye pia kushikiliwa alipoenda kumtembelea mmewe mahabusu Oysterbay.

Hii ilikuwa ni baada ya mimi kuibuka na Uzi huu Twitter jambo ambalo liliwafanya manjagu baadae waje na taarifa iliyoyanyoosha maelezo kama rula.

Lakini kuna infoma anadai hii sio mara ya kwanza kwa Andron Msomi kutoka DIT kufanya hivi lakini taarifa hizi sijazithibitisha kwani zimehusisha mambo ya kijadi zaidi
Credit: Fortunatus Buyobe (Telegram channel)
Sasa nimeelewa kwanini mtungi wangu wa kupikia zamani ulikua unakaa miezi mitatu ndio unaisha, na sasa hivi mtungi huo huo u akaa mwezi mmoja unaisha.

Sasa nimeelewa kwanini maduka mengi ya kuuza Gas hayakai na mizani ya kupimia uzito wa mitungi.

Ina maana mitungi ya gas tunayouziwa inakuwa imepigwa pipe na watu dizaini ya Adinani.

Ina maana tunauziwa mitungi yenye ujazo nusu kwa bei ya mitungi iliyojaa.

Nitashangaa kama huyo mpiga deal Adinani ataachiwa huru.[emoji848]
 
Sasa nimeelewa kwanini mtungi wangu wa kupikia zamani ulikua unakaa miezi mitatu ndio unaisha, na sasa hivi mtungi huo huo u akaa mwezi mmoja unaisha.

Sasa nimeelewa kwanini maduka mengi ya kuuza Gas hayakai na mizani ya kupimia uzito wa mitungi.

Ina maana mitungi ya gas tunayouziwa inakuwa imepigwa pipe na watu dizaini ya Adinani.

Ina maana tunauziwa mitungi yenye ujazo nusu kwa bei ya mitungi iliyojaa.

Nitashangaa kama huyo mpiga deal Adinani ataachiwa huru.[emoji848]
Kamshitaki Adnan
 
Kama Andron angekwenda bila bunduki pengine angemzaba kibao huyo mlinzi, kisha kugundua kuwa aliyempiga kibao siyo mlengwà, angemuomba samahani na kumpa hata Tsh
Unajuaje mlinzi hakuwa mlengwa ?

Dereva "uchebe" msambaza mitungi, na walinzi wa ndani na wa getini wanaweza kuwa genge la uhalifu lenye nia moja, joint enterprise. Ndo maana akafukuza walinzi wote, pamoja na wa nyumbani ambao wanamuona akitoka wanatuma inteligensia, Mzee anakuja ofisini.

Mitungi mingi ya gesi imenyonywa, mteja huna jinsi ya kupima kabla hujanunua, uneanda kuona nyumbani kimtungi kimeisha ghafla kama kifurushi cha VODACOM.

Defendant Andron is entitled to a presumption of innocense and competent defense.
 
Andron Nichodemus ( cox) jamaa tumelala wote dom 2 pale umbwe nilikua nalala deck ya juu jamaa alikua muhuni flani hivi ( mambo ya kinyamwezi sana) ila kichwa sana ( hasa mathematics) tulikuja kukutana UDSM akichukua B.com nimekuja kusikia jamaa ni billionaire ila tena juzi naambiwa kaua mtu .maisha haya duuh.
Mwaka gani?
 
Hata kesi ikiwa ipo mahakamani, hakuna ushahidi unaoharibika kwa watu kuizungumza mtaani na wala hakuna sheria inayokataza kuzungumza habari za tukio ambalo tayari limefunguliwa kesi mahakamani.

Majaji au mahakimu hawatoi hukumu kwa kusoma mitandaoni au magazetini habari za tukio lihusulo kesi ili mbele yao, au kwa kusikiliza story mitaani BALI wanafikia hukumu kwa kuchambua na kupimanisha ushahidi uliotolewa mahakamani.

Hii ya kusema siruhusiwi kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani, ni WANASIASA waliiweka ili kukwepa kuhojiwa kwa kesi zinazohusu serikali na wao wenyewe, sasa imechukuliwa kama ni sheria au kosa kuzungumzia jambo ambalo lina kesi mahakamani, KITU AMBACHO SIO KWELI, SIO KOSA.
Fact.

Eti tusiongelee kesi iliyoko mahakamani.

sikujua kuna Mtanzania mwenzangu hata mmoja anaepinga huo utopolo, miaka 15 niliyokaa hapa JF.

Majaji, maprofessa wa sheria, maspika, wabunge, wanahabari, Watanzania kwa mamilioni...tumelishwa uongo, tumepikwa tukaiva.

Jaji gani au Hakimu aliwahi kuandika hukumu akasema sehemu ya ushahidi aliotumia aliusikia kwenye kijiwe cha kashata na drafti Tandika sokoni alipoenda kununua matembele na maharage ???
 
Unajuaje mlinzi hakuwa mlengwa ?

Dereva "uchebe" msambaza mitungi, na walinzi wa ndani na wa getini wanaweza kuwa genge la uhalifu lenye nia moja, joint enterprise. Ndo maana akafukuza walinzi wote.

Mitungi mingi ya gesi imenyonywa, mteja huna jinsi ya kupima kabla hujanunua, uneanda kuona nyumbani kimtungi kimeisha ghafla kama kifurushi cha VODACOM.

Andron is entitled to a presumption of innocense and competent defense.
No body is doubting the presumption of innocence because it is an inalienable constitutional right. However ursuping the power of prosecuting and and convicting was crossing the lines of rule of law.

Kama hao walinzi wa geti walikuwa ni sehemu ya wapiga deal ya wizi wa gesi, basi kama kweli Andron ni genius kama tunavyoaminishwa basi angetafuta namna nyingine ya kuwakamata na siyo kwenda mwenyewe physically under influence of hard substances
 
Unajuaje mlinzi hakuwa mlengwa ?

Dereva "uchebe" msambaza mitungi, na walinzi wa ndani na wa getini wanaweza kuwa genge la uhalifu lenye nia moja, joint enterprise. Ndo maana akafukuza walinzi wote.

Mitungi mingi ya gesi imenyonywa, mteja huna jinsi ya kupima kabla hujanunua, uneanda kuona nyumbani kimtungi kimeisha ghafla kama kifurushi cha VODACOM.

Andron is entitled to a presumption of innocense and competent defense.
Adhabu ya mtu anayeimuibia muajiri wake ni kupigwa risasi na kufa? Huyo jamaa ni mjinga, kwa pesa alizonazo angeweza kupeleka kesi mahakamani na kuwafunga hao na kuwa fundisho kwa wengine.

Ujinga mwingine ambao amefanya ni kuubeba mwili na kwenda kuutupa kibaha. Hapo tayari inaonyesha alikusudia kufanya mauaji
 
Back
Top Bottom