Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Mkuu sio lazima rais awe mchagga ili uyaone uliyotegemea kuyaona. Waziri Mramba alitosha kuweka ukabila ndani ya TRA.

First lady wa awamu ya tatu alitosha kuwafanya wadogo zake wawe na ushawishi mkubwa kwenye uchumi wa nchi.

Haya mambo ya ukabila yanaletwa sana awamu hii kwa nia ya kutaka kumkwaza mkuu pale magogoni, lakini wanaoyaleta wamesahau ni namna gani watu walivyo na data zao za miaka ya nyuma kuhusiana na huo huo upendeleo wa kikabila na kikanda.
 
kama wasukuma hamna huo ushetani wote basi tuambieni uyu mkul na bashite ni warundi au wanyarwanda mbona wana tofauti ndogo sana IS roho ya utu kwao ni 0.00...
 
Binafsi siungi mkono ukabila kwa namna yoyote ile. Ila tuwe wakweli, inakera kuona wasomi wenye kuweza kufanya makubwa hapa nchini, wakidharauliwa kwa sababu hawana mtu wa kutambua uwezo wao na kuwapa vyeo vikubwa.

Wapo wakurugenzi wa mamlaka kadhaa ambao kwa sasa wanafanya mambo makubwa sana kwenye ofisi zao, miaka ya nyuma hawa watu wasingeweza kuwa kwenye hizo nafasi kwa sababu walikuwa sio sehemu ya watoto wa fulani na fulani.

Nchi yetu imekuwa ikipoteza vipaji vingi kwa sababu tu tulijenga mfumo feki ambao uliweka chujio baya la mtu kupewa nafasi kwa sababu anamjua fulani na sio kwa sababu ya uwezo wake.

Hawa wanaoitwa wasukuma ambao wanapewa vyeo hivi sasa, miaka ya nyuma walitengwa na huo mfumo feki lakini haimaanishi kwamba hawakuwa na uwezo. Maamuzi magumu ya awamu ya tano, yanaambatana na baadhi ya watu kununa, na wanaponuna basi wakiongea ndio huishia kuongelea ukabila.
 
kama wasukuma hamna huo ushetani wote basi tuambieni uyu mkul na bashite ni warundi au wanyarwanda mbona wana tofauti ndogo sana IS roho ya utu kwao ni 0.00...
Nyinyi msiokuwa warundi mmeifanya nini nchi hii?. Mbona mliruhusu wenye vyeti feki waongoze taasisi nyeti?, mbona mliruhusu uozo mwingi tu!!.

Badilika kimawazo ndugu yangu, la sivyo utaishia kwenda kwa waganga na wachawi kumbe tatizo ni dogo tu na limo ndani ya uwezo wako wa kufikiri.
 
Wabh'eeja nkoi.tatizo watakupinga tu watu na akili zao
 
Za asubuhi kaka, hiyo point ya mwisho kabisa ndio ambayo hawapendi kukubaliana nayo. Hapo kwenye kula na kufurahia maisha kwa zamu, hawataki kabisa kupasikia.

Yaani kama kuna profesa kutoka Kigoma au Geita basi abakie kufanya kazi zile zile tu bila hata kupewa mamlaka au wizara fulani!!.

Yaani talents za mikoa fulani zisijulikane kwa sababu kuna talents maalumu kwa watanzania, ambazo siku zote zina haki ya kuamua juu ya mustakabali wa Tanzania!!, huu ujinga bora wangeendelea kubakia nao vichwani mwao.
 
unamuongelea bashite? shame upon u humuogopi hata mungu , wameondolewa wangapi kwa vyeti fake bashite kabakizwa?
Jesca alipata ngapi na UDOM alifikaje? na ilivyojulikana alifanywa nini na watoto wa maskini wakifanywa nini?
waliobomolewa Dar na tabora walipewa sababu gani na mwanza kawaanbiaje ivi hata kama hujaenda shule iyo mifano nayo inakushinda and so far kafanya nini zaidi yakuaribu nchi
 
Pathetic!!, hivi maisha ya Tanzania yana bashite peke yake??!!.

Unayajua madudu waliyofanya hao watu special hapa nchini!!??, unazijua hasara walizolitia taifa kwa sababu ya kiburi chao!!??.

Unamuongelea mtu mmoja tu, mbona huongelei mamia ya watu fulani ambao kuanzia awamu ya mzee Mwinyi mpaka ya mzee Kikwete waliifanya nchi hii kama ya kwao peke yao!!??
 
ivi pathetic maana yake ni nini? idiots
tunaongelea current issue za uyo mshamba unaleta habari za past nani aliyesema uongozi uliopita hayakuwepo mafisadi? vitu vilikuwa vinafanyika vibaya but at list walikuwa na utu/ walikuwa wanaficha torturing yao kwa public uyu unayemtetea within two yrs ya rein yake umeona wangapi wanaumizwa direct tena bila haya, doble standard za wazi tena hadi kwenye public speech
 
Mshamba mkubwa ni wewe ambaye unataka jana na juzi ifanane na leo na kesho.

Unaweza ukaweka hadharani hiyo torturing au ni yale yale ya kutegemea habari za magazeti ya udaku na kutoka kwa Mange Kimambi?.

Wewe kuwa mpiga kura sio kigezo cha kuwa na mamlaka ya kumpangia namna ya kufanya kazi yule mtu uliyempigia kura.

Umeamua kuchukua upande wa kinyongo na maumivu, ni uamuzi wako, lakini hauwezi kukusaidia kwa namna yoyote ile, iwe leo kesho au hata baada ya mwaka mmoja kupita.
 
Sasa pascal mnyonge akinyongwa haki yake ataipata wapi?
Mkuu Radika, hata aneyehukumiwa kunyongwa, pia anazo haki zake kabla ya kula kitanzi zikiwemo
  1. Hati ya kifo , death warranty kusainiwa na rais.
  2. Siku ya kitanzi hula vizuri, huoga vizuri na kujiswafi, shaving and look good ikiwemo kuvaa mavazi safi
  3. Kupimwa na daktari kuthibitisha yuko buheri wa afya, akikutikana ni mgonjwa tuu hata mafua, hayongwi kwanza mpaka atibiwe apone sii haki kumnyonga binadamu yoyote huku ni mgonjwa.
  4. Haki ya kuwaaga ndugu zake na kusema neno moja la mwisho.
  5. Haki ya kuswaliwa sala ya toba kama ni Mkristu anaitwa padri kumuombea kama ni Mkatoliki anaungamishwa na kupakwa mpako wa mwisho. Kama ni Muislamu anaitwa Shehe na wakati wa utekelezaji anatizamishwa Kibla.
  6. Waathirika na makosa ya mtuhumiwa, ndugu na jamaa wanaruhusiwa kushuhudia utekelezwaji wa adhabu hiyo.
  7. Utekelezaji hufanywa na mtu wa dini yake, kwa vile Wakristu huwa hatunyongi hivyo hatuna neno lolote la kunyongea ila kama ni Muislamu, mnyogaji hupiga Bisumilahi.
  8. Baada ya kutelezwa daktari anathibitisha kuwa amenyongwa hadi kufa. Akikutwa bado anahema, humaliziwa kwa nyundo fulani kichwani.
  9. ndugu wanaruhusiwa kukuchukua mwili wa ndugu yao kwa mazishi kwenye makaburi ya gereza.
  10. Ibada ya mazishi hufanyika ila hairuhusiwi kuweka msiba wala matanga.
Hivyo hata mnyonge wa kunyongwa, anyongwe ila haki zake apewe.

NB. Sorry kuwapa detailed process ya kunyongea kwa kwa sababu mimi ni miongoni mwa wapiga vita adhabu ya kifo
Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo | JamiiForums | The Home of Great ...
Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika? | JamiiForums | The ...
Wana JF tuungane kusema NO hukumu ya kifo | JamiiForums | The Home ...

Paskali
 

hahahaha hapo kwenye NB shukrani mkuu pascal.
 
Huu ni ukweli kabisa usio kuwa na kipingamizi kwa mtu yyte aliye ishi usukumani. Binafsi mimi sio msukuma na wala sio wa kabila lolote la ki tanzania ila nimezaliwa usukumani nimekulia usukumani nimeenda shule usukumani sijawahi kubaguliwa na wasukuma na wala hawana udini, na ni down to earth people, na hawajui kuomba rushwa, sijaona watu kama wasukuma tz, nimetembea tz nzima lakini nikikutana na msukuma popote pale tz nakuwa very comfortable najisikia niko nyumnani, naongea kisukuma kama wao. Na magufuli alipo chaguliwa kuwa rais nilisema sasa ndio tz itakuwa streight fwd. Mpe mda achape kazi ugumu wa maisha kwa sasa ni ya mda mfupi tu kiasi anarudisha watu kwenye reality ambayo wa tz wengi walikuwa wakiishi kwa dili dili. Kumbukeni hata Roma haijajengwa kwa miaka 2.
 
Wachaga na wapare jamii moja, Cleopa Msuya, Augustin Mrema.
 
Well said. Umemaliza!
 
Mr.mayalla
Kama wasukuma ndio wenye sifa miaka yote hizo sifa na vigezo havikuonekana mpaka awamu hii.
Aliye kivulini hawezi tambua shida ya aliyekaa juani.
Unapotaka kuchota minds za majority ni vema kijipima kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…