Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

wewe ndiye unaye tazama teuzi za Raisi kwa jicho la ukabila, ukanda na dini
 
Ww ndio mkabila kabisa cjui unatoka kulekule wanatunyanyasa sehemu za kazi tangu Uhuru
 
We ndio mkabila mkubwa cjui unatoka kulekule wasukuma mpaka leo wanawabunge mkabila cjui mnawatafutia Ila mnawafumbua macho!!
 
Na ukumbuke pia kuwa mnapokuwa wengi hasa Kiidadi ndiyo inakuwa rahisi sana pia kuzidisha Ukabila katika Sekta / Nyanja mbalimbali. Mfano mzuri tu wa hili wala haupo mbali nasi bali angalia huko nchini Burundi utagundua kuwa Wahutu ni wengi kuliko Watutsi na Wahutu wameendeleza ukabila wao na hivyo hivyo rudi nchini Rwanda ambapo siyo siri kwamba Watutsi ni wengi kuliko Wahutu na kwamba Watutsi wameendeleza ukabila wao mkubwa kwa gharama za Wahutu walio wachache.

Rudi nchini Kenya ambapo makabila yenye idadi kubwa ya Watu pengine hata kuliko Makabila mengine ya Kenya ya Kikuyu na Luo ndiyo yanayopambana usiku na mchana ili kuweza kumiliki ' dola ' kisha ama Ukikuyu au Uluo uzidi kutamalaki na ndiyo maana unaweza kuona hata katika Kampeni zao Kambi zote sasa si za Umoja wa Kikenya bali sasa zimekuwa ni za Umoja wa Kikabila.

Malizia na nchini Uganda ambapo nao wana Makabila mengi kiasi lakini ' Makabila ' ambayo yanaongoza ndani ya ' Mamlaka / Tawala ' za nchi hiyo ni yale tu ya Kusini Magharibi ya nchi hiyo ambayo ni ya Wanyankole, Wahima, Wasoga na Bachiga na ndiyo maana utaweza kuona hata Rais Museveni ambaye ana Unyankole na Uhima amejitahidi sana kuwateua Watu wa hayo makabila tajwa manne ( 4 ) kushika ' nyadhifa ' Kubwa na Nyeti za nchi hiyo nia ikiwa ni kuyaimarisha hayo makabila.

Na nikusaidie tu kwa kukuambia kuwa nchini Tanzania ' Ukabila ' umeondoka tu ' midomoni ' mwetu ila katika ' mioyo ' yetu ukabila upo pale pale na tunauendeleza kila uchao katika maeneo mbalimbali. Tujifunze sana kuacha ' Unafiki ' wa kufichaficha na kutetea vitu ambavyo ' logically ' na ' vividly ' vipo na vitaendelea kuwepo.

Kila la kheri.
 
Tatizo wenye kulalamika haya masuala ya ukabila bahati mbaya hawajui kama nao wana ukabila,maana kama hadi leo mtu unafutilia kujua kabila la mtu ni wazi nawe ukabila haujakutoka.

Ukiangalia malalamiko ya humu si kwamba wanateuliwa wasio na sifa bali wameteuliwa watu kadhaa wa kabila moja,kwa maana hiyo walalamikaji hapa hawalaumu ukabila bali wanacholaumu makabila mengine hayajachaguliwa kwenye huo ukabila.
 
BASHITE anafumbiwa macho kwa vile MSUKUMA, hili ni jambo la hatari sana. Rais namwamini sana ila katika hili hapana.
 
Ukiona jambo linazungumzwa na wengi ujue lipo
 
Watu bhana...
yani inatumika nguvu nyingi sana kutuaminisha tofauti, watanzania nao wanaona na wanaelewa.
hii ni 2017...kubalini tu huyo jamaa kateleza, kukubali ni uungwana.
 
ukweli lazima usemwe wazi kuwa Rais anafanya teuzi kwa kigezo cha ukabila na ukanda!! Miradi mingi ya maendeleo sasa inapamba moto kanda ya ziwa!!!!! ni hatari kwa ustawi wa nchi na amani
Leo hii Raisi atakuwa Itigi-Singida kufungua mradi wa barabara, akitokea Tabora na Kigoma je hii yote ni kanda ya ziwa?

Mwezi ujao atakuwa Tanga na Raisi Mseveni, je Tanga nayo iko kanda ya ziwa?
 
Wewe mzee unajifanya mchambuzi huru, lakini kiukweli you're biased, kila unapotoa hoja lazima iwe na mwelekeo wa upande wako ingawa unajaribu kukwepa kana kwamba hauko affiliated na upande fulani, that's insincerity.
 
Kwa vile na wewe msukuma.....endelea kumpigia chapuo na vile anakufahamu tutakusikia siku moja kwenye teuzi....mana si bado anaendelea kuwaingiza wasukuma wenzie kwenye system...
 
Kweli kuna watu ninawaona wanajadili ukabila humu lkn nikiwacheki kwa jito la tatu kwao ukabila ni Sara!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…