Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!


Actually kwa kumnyanyasa Tundu Lissu ndio wanazidi kuthibitisha kuwa alichosema ni kweli ndio maana wanataka kumnyamazisha. Katika moja ya hotuba zake Nyerere aliwahi kusema kuwa hata yeye aliwahi kutuhumiwa kwa udini. Hakuwakamata waliomtuhumu.

Badala yake aliitisha mafaili ya wateule waliodaiwa kuwa amewateua kwa udini, na majibu aliyatoa hadharani, kuwa kumbe katika cabinet ile waliyomtuhumu ina udini kulikuwa na watu wawili tu wa dini yake ambao ni yeye mwenyewe na Sir George Kahama, na tena akatania kuwa hata Sir Kahama hakushika dini ipasavyo kwani alikuwa "ameendelea" zaidi kwa kuchukua mke wa pili.

Siamini kuwa serikali ya JPM imeshindwa kutolea ufafanuzi haya mambo, mbona mengine yakisemwa tu unaona Msigwa anawahi kukanusha, hili lina shida gani?
 
Hii hatujaanza kuisikia leo,kila awamu inatupiwa hii lawama so tushawazoea.
 
BASHITE anafumbiwa macho kwa vile MSUKUMA, hili ni jambo la hatari sana. Rais namwamini sana ila katika hili hapana.
Hata ukimya wa Maaskofu ni kwa sababu Magufuli ni !wanaparokia mwenzetu, hii nchi imejaa wanafki.
 
Dawa ya ukabila nyerere alikuwa amisha ipata na solution yake alisema si vyema mtu kutoka kabila kubwa apewe urais.Kuhusu insu ya wakurya jeshini kutokana na mazingira ya kipindi kile ambacho technolojia ilikuwa chini Wakurya ndio kabla pekee Tanzania ambao ni wajasiri hilo lipo wazi hawakupelekwa sababu ya ukanda.

kama nyerere angekuwa hivyo basi Mkoa wa mara ndio ungekuwa mkoa wenye maendeleo katika mikoa yote.
 

Paskali,
Naona umeshindwa kujificha kabisa kutetea ukanda. Kwa hiyo kwakuwa wasukuma ni wengi basi ukileletewa watu watatu wote wana sifa sawa utachukua msukuma?

Kumbuka kama wewe ni Raisi wa nchi, kitendo tu cha kuwa Raisi ni sababu tosha ya wewe kutumia busara kuwa hata kama hawa wadogo watatoka makabila mengine hawawezi kuishinda nguvu yako wewe Raisi.

Hicho unachosema kinawezekana tu pale ambapo Raisi ni mtenda haki na mwenye busara kinyume na hapo nipo kinyume na wewe!!!
 
Raisi hateui viongozi kwa kuangalia dini au kabila. raisi anateua viongozi kwa kuzingatia sifa na uwezo wa kazi
Tupe uthibitisho mubashara Otherwise mnaendelea kutetea usukuma tu hapa. Yuko sheakh mmoja alikuja na data za wasomi wa kiislamu zaidi ya 600 ambao serikali ya magufuli imewamarginilized,je mliifanyia kazi orodha ile?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: SDG
Safi kabisa!! Na kinyume chake ni kwamba kama basi mmeshindwa kabisa kumtoa Raisi kwenye kundi la wachache, ili kubalance power of representation ukizingatia mamlaka makubwa ya Rais aliyo nayo kama wa kwetu, ni vema viongozi wengine asilimia kubwa zaidi ikatoka kwingine si kwenye kabila la Rais tena. Kumbuka kuna madhara ya kuwa na Rais aliyezungukwa na kabila lake. Haya maneno ya kutaka kumuongezea muda mkulu yakizidi kupamba moto yatazimwaje kama serikali yote asilimia kubwa ni watu wa kabila la Rais? Paskali bado sikuungi mkono.
 
Hili kuupata ujumbe huu maridhawa,yahitaji uwe na jicho la tatu
 
Shida nin kuwa kwa mfumo wa katiba yetu ambao unampa rais mamalaka makubwa ktk teuzi mkisha kosea kwa rais madhara yake ndio haya,hatat hivyo hii ilitokana na CCM Kuwa na hofu ya kutopata dola ndio maana walimchagua jamaa ili wapate kura nyingi za ukanda huo
 
Marginalization ya kiongozi ipo katika dola zote. Kumuacha kiongozi madarakani kisa utaonekana una udini au ukabila au ubaguzi flani ni udhaifu mkubwa kabisa. tena huu udhaifu ndio hulitumbukiza taifa katika ubaguzi uliopindukia.
Lazima vitengo vya serikali vishikiliwe na watu wenye sifa na uwezo
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…