Jobless_Billionaire
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 3,106
- 8,101
Wasalaaam.. Nina imani mko poa na mnatekeleza majukumu yenu kama ilivyo ada.
Kabla ya yote, watu tunafanya mambo kulingana na uhitaji wetu, na tunafanya kwa makadirio ya kuridhika na kitu ambacho tunafanya. Kwa mfano, nikiwa nina hamu ya soda nitanunua kwa lengo la kunywa ili kukidhi ile kiu ambayo imenifanya ninunue soda. Ninapokuwa na njaa, naagiza chakula cha kunitosha ili nile nipate kuwa sawa, na mambo mengine mengi ya mfano huo.
Sasa, Kuna mambo kidogo nimekuwa nikikutana nayo hasa mazingira ninayokuwepo ambayo kimsingi sipendezwi nayo (sijajua kwa nyie wengine). Wapo watakaohusianisha jambo nitakalolisema na UCHOYO, lakini kimsingi si hivyo. Kuna watu huwa hawawezi kabisa kujishikilia, na hapa ndio msingi wa kitu ninachotaka kueleza.
Mie sio mnywaji, naweza kwenda mazingira ya viwanja kwa ishu nyingine tu, kwa mfano nahitaji nile kitimoto tu. Unafika huko unakutana na baadhi ya watu ambao mnafahamiana tu, labda wao ni wanywaji wapo kwenye starehe hiyo. Sasa, unashangaa unaagiza kitu roho uako nawewe inapenda, unashangaa watu wanajoin hadi end point. Sasa unajiuliza, hawa wamemudu kununua pombe, kwanini kama walikuwa na hamu ya kitimoto wasingeagiza hadi wajialike kwenye jambo langu?
Sawa, mimi ni mchezaji wa pool table. Naenda kwenye mazingira ya pool table, nakuta wadau wanacheza game dau ni 20000 kwa mfano. Naamua tu, sichezi table ngoja hii hela niliyopanga kucheza niifurahie kwa namna nyingine tu. Naagiza kitu chochote ambacho naona kitanifaa, unashangaa haohao ambao wamemudu kucheza mchezo kwa gharama hiyo wanajialika to the end point. Kama mlikuwa mna hamu na hiki ninachotumia mbona mlikuwa na uwezo huo, kwanini msingejinunulia ingali mna uwezo huo?
Unanunua zako kakitu, mtu anakuja mbiombio anakwambia niachie na mimi. Vitu vingine vidogo tu ambavyo mtu unaona kabisa anamudu gharama zake. Huu ni upuuzi. Ukiona mtu kafanya jambo jua kalifanya kulingana na hitaji lake, unapoingilia kati unamfanya asiwe sastified na kitu husika. Watu wanachukulia kawaida kawaida tu lakini hivi vijitabia sio, kumuona mtu ana kitu halafu unaanza kumn'gong'a ilehali unaweza kuwa na kitu kama hicho. Mara mia mwambie akununulie au akuongeze pesa kama umepeleza nawewe ufanye hivyo.
Wengine mbona tunaweza tu, nakukuta unafanya jambo lakini siwezi kukuingilia. Najua kabisa umefanya kwa ajili yako. Kitendo cha mimi kukuingilia ni kukuharibia bajeti zako na kukufanya uwe na kinyongo hata kama hutoniambia
Haya, unakaribisha mtu ukae nae kwako anaanza kuvaa nguo zako, anavaa na anajiamini kabisa. Huu nao ni upuuzi Pro Max
Mtu anakuomba umsaidie simu awasiliane kwakuwa yake haina balance, anamaliza kuongea anaanza kuipekua. Mara kwenye chats mara picha. Na anakuwa anakuuliza kabisa, hii picha ulipigia wapi😡😡😡😡. Tabia ya kipuuzi sana hii.
Umevaa zako nguo kali umetokelezea, upo mizunguko unakuta jamaa au rafiki yako yupo na wenzake halafu anaanza kukuuliza hiyo jeans au t-shirt umenunua shilingi ngapi?? 😡😡😡
Umenunua simu au nguo ya rangi ambayo wewe unapenda. Mtu anaiona halafu anaanza kuitolea kasoro, mara kwanini usingechukua ya bluu? Kama blue kwako ni nzuri nenda kajinunulie, nimeenda kwenye ile ambayo ni favourite kwangu.
Una mwanamke wako au mwanaume wako unampenda na anakupenda, mnaishi na mnayafurahia kabisa maisha yenu halafu mtu anatokea anakwambia demu au jamaa yako hamuendani.😡😡
Kuendana vipi unataka? yaani mnaishi wote na mnapendana halafu jitu la pembeni linataka ufanye mambo kuliridhisha jenyewe. Mara mia aje na hoja ya msingi labda demu/jamaa hajatulia, lakini ni hoja za kipumbavu tu ambazo zinaweza kusababisa ukalinasa hata makofi
Tabia zipo nyingi, mnaweza kuongezea wakuu. Kwangu mimi hizo ndio nazizichukia vibaya mno...