Tujadili uwepo wa idadi kubwa ya wenye nyumba ambao ni maskini hapa Tanzania hasa jijini Dar

Nini kifanyike?

Kiukweli idadi ya wenye nyumba maskini ni kubwa mno jijini Dar na miji mingine nchini kwetu. Je, ni mitazamo mibovu ya wananchi wengi kuhusu kumiliki nyumba? Yaani kwa haraka haraka kuna wapangaji wengi wana maisha mazuri kuliko wapangishaji. Maeneo ya uswahilini ni kawaida kuona mwenye nyumba anamwonea wivu mpangaji wake.

Mimi ninashauri watu waache mambo ya kukurupuka kujenga nyumba huku wakiwa wana vyanzo dhaifu vya mapato. Ni upumbavu wa hali ya juu kukuta kijana mjasiriamali akijitutumua kujenga nyumba ya milioni kadhaa huku biashara yake ikiwa bado haijakaa sawa. Hata wanamuziki, wanafilamu, wanamichezo na watu wa fani zingine zote ninawashauri wasikimbilie kujenga nyumba huku wakiwa hawajajiimarisha kwenye fani zao.

Chanzo cha mapato kikiwa imara utaweza kujenga nyumba nzuri na kuwa baba mwenye nyumba ambaye sie maskini. Kama ni mwanamuziki tumia hela zako za mwanzoni kuwekeza kwenye muziki wako kwanza. Ni upuuzi una nyumba lakini bado unalia lia kwenye biashara yako ya muziki.

Binafsi ninakerwa mno nikiona baba au mama mwenye nyumba maskini kuliko mpangaji. Tubadilishe fikra zetu.
Naam
 
Hao ni wale baada ya kustaafu au kufukuzwa kaI wanaamua kupangisha upande ili wajikimu, so lazima awe masikini
 
Akili Matope za Akina Wema Sepetu na Bongo Fleva wa wakati huo leo wanawaoneo Wivu wadogo zao. Waliishia kupanga Sinza, Mbezi na Osterbay kwa bei ya Kupata Kiwanja Goba leo Filamu na Mziki wao vimebuma wanajuta.
Cha kwanza jilipue jenga nyumba mengine yafuate nikiwa ndani kwangu hizo habari za ujuaji zimeponza wengi.
Well
 
Nitapingana na mleta mada, na sababu ni hizi.

Kwanza hajatupa tafsiri yake ya maskini ni ipi. Kwa tafsiri ya kijamii na kiserikali, mtu yoyote mwenye kumiliki nyumba mjini huyo sio maskini na hayupo kabisa katika kundi la maskini.

Pili, mtu yoyote aliyefanikiwa kujenga nyumba mjini hapa Tanzania kiujumla jumla ni mtu mwenye mipango mizuri ya kimaisha ya muda mrefu na nidhamu nzuri zaidi ya kipesa kuliko asiye na nyumba. Huyo apongezwe.

Tatu, ni ndoto za karibu kila mtu mwenye mbio za kutafuta fedha huku akiwa na kiu ya kuwa na maendeleo kutaka siku moja kuwa na nyumba yake binafsi. Karibu kila mpangaji ana kiu ya kumiliki nyumba yake na anaona kuendelea kupanga ni utumwa ambao unapaswa siku moja ukome.

Nne, mtanzania mwenye kipato cha kuweza kujenga nyumba halafu akwepe kujenga nyumba, mara nyingi (kama sio mara zote) pesa zake nyingi huishia katika kununua magari, kustarehe (pombe, ngono nk), kusafiri, kufanya sherehe, kuvaa, kula, kununua vitu vidogo vidogo vya kisasa (simu, vito, runinga nk).

Tano, kufanya biashara sio mbadala wa kujenga nyumba au kujenga nyumba sio mbadala wa kufanya biashara. Watu hawajengi ili kukwepa kufanya biashara na watu hawafanyi biashara ili kukwepa kujenga. Maisha ni kupanga, na kupanga ni kuchagua.
 
Mleta mada ulishawahi kujiuliza ni kwanini watu wengi hutamani kumiliki nyumba. Majibu ni haya;

1. Kuwa na uhakika na usalama wa maisha yao ya sasa (wakati huu wako hai au wana nguvu) na baadaye (wakati wameshoka, kuzeeka au kufa (kwa ajili ya familia zao)).

2. Kuwa huru kimaisha (mmiliki wa nyumba ni mtu mwenye kujiamini na matumaini makubwa zaidi kimaisha)

3. Kupunguza gharama za kila siku za kupangisha.
 
Nini kifanyike?

Kiukweli idadi ya wenye nyumba maskini ni kubwa mno jijini Dar na miji mingine nchini kwetu. Je, ni mitazamo mibovu ya wananchi wengi kuhusu kumiliki nyumba? Yaani kwa haraka haraka kuna wapangaji wengi wana maisha mazuri kuliko wapangishaji. Maeneo ya uswahilini ni kawaida kuona mwenye nyumba anamwonea wivu mpangaji wake.

Mimi ninashauri watu waache mambo ya kukurupuka kujenga nyumba huku wakiwa wana vyanzo dhaifu vya mapato. Ni upumbavu wa hali ya juu kukuta kijana mjasiriamali akijitutumua kujenga nyumba ya milioni kadhaa huku biashara yake ikiwa bado haijakaa sawa. Hata wanamuziki, wanafilamu, wanamichezo na watu wa fani zingine zote ninawashauri wasikimbilie kujenga nyumba huku wakiwa hawajajiimarisha kwenye fani zao.

Chanzo cha mapato kikiwa imara utaweza kujenga nyumba nzuri na kuwa baba mwenye nyumba ambaye sie maskini. Kama ni mwanamuziki tumia hela zako za mwanzoni kuwekeza kwenye muziki wako kwanza. Ni upuuzi una nyumba lakini bado unalia lia kwenye biashara yako ya muziki.

Binafsi ninakerwa mno nikiona baba au mama mwenye nyumba maskini kuliko mpangaji. Tubadilishe fikra zetu.
Najaribu kukuelewa kiongozi.

Embu twende taratibu. yani wewe mpangaji unaemiliki sembe ya kununua kwa mangi na sabuwufa yako ya kuskiza singeli na mwenzio mwenye hati yake ya nyumba, ana uwanja, ana nyumba yake, ana miembe yake, maji unayokunywa yanasoma jina lake, umeme unaotumia wew mpangaji unasoma jina lake.

Kwaiyo apo bado wewe mpangaji unafanana na faza hausi?
 
Sijasema wenye nyumba wote ni maskini.
 
Kwa vile umejenga wapangaji wote unataka wawe ni wa hali ya chini au? Helewa kuwa kujenga sio kuwa na hela ni maamuzi tu, unajenga na umaskini wako uko palepale na kujenga hakujawahi kua mtaji labda ujenge nyumba ambayo sio ya viwango vyako,
 
Kuna mama mmoja mjin yeye ukipanga kwake utajuta yan hela anapata sijui anapeleka wapi unampa hela baada ya mwezi anaanza kulilia shida umkopeshe usipompa ni vijembe na kukukasirikia uswazi hapana aisee
 
Una uhuru wa kufanya utakavyo juu ya maisha yako bila kupangia watu wengine maisha yao,your life your choices.
Nini kifanyike?

Kiukweli idadi ya wenye nyumba maskini ni kubwa mno jijini Dar na miji mingine nchini kwetu. Je, ni mitazamo mibovu ya wananchi wengi kuhusu kumiliki nyumba? Yaani kwa haraka haraka kuna wapangaji wengi wana maisha mazuri kuliko wapangishaji. Maeneo ya uswahilini ni kawaida kuona mwenye nyumba anamwonea wivu mpangaji wake.

Mimi ninashauri watu waache mambo ya kukurupuka kujenga nyumba huku wakiwa wana vyanzo dhaifu vya mapato. Ni upumbavu wa hali ya juu kukuta kijana mjasiriamali akijitutumua kujenga nyumba ya milioni kadhaa huku biashara yake ikiwa bado haijakaa sawa. Hata wanamuziki, wanafilamu, wanamichezo na watu wa fani zingine zote ninawashauri wasikimbilie kujenga nyumba huku wakiwa hawajajiimarisha kwenye fani zao.

Chanzo cha mapato kikiwa imara utaweza kujenga nyumba nzuri na kuwa baba mwenye nyumba ambaye sie maskini. Kama ni mwanamuziki tumia hela zako za mwanzoni kuwekeza kwenye muziki wako kwanza. Ni upuuzi una nyumba lakini bado unalia lia kwenye biashara yako ya muziki.

Binafsi ninakerwa mno nikiona baba au mama mwenye nyumba maskini kuliko mpangaji. Tubadilishe fikra zetu.
 
Nini kifanyike?

Kiukweli idadi ya wenye nyumba maskini ni kubwa mno jijini Dar na miji mingine nchini kwetu. Je, ni mitazamo mibovu ya wananchi wengi kuhusu kumiliki nyumba? Yaani kwa haraka haraka kuna wapangaji wengi wana maisha mazuri kuliko wapangishaji. Maeneo ya uswahilini ni kawaida kuona mwenye nyumba anamwonea wivu mpangaji wake.

Mimi ninashauri watu waache mambo ya kukurupuka kujenga nyumba huku wakiwa wana vyanzo dhaifu vya mapato. Ni upumbavu wa hali ya juu kukuta kijana mjasiriamali akijitutumua kujenga nyumba ya milioni kadhaa huku biashara yake ikiwa bado haijakaa sawa. Hata wanamuziki, wanafilamu, wanamichezo na watu wa fani zingine zote ninawashauri wasikimbilie kujenga nyumba huku wakiwa hawajajiimarisha kwenye fani zao.

Chanzo cha mapato kikiwa imara utaweza kujenga nyumba nzuri na kuwa baba mwenye nyumba ambaye sie maskini. Kama ni mwanamuziki tumia hela zako za mwanzoni kuwekeza kwenye muziki wako kwanza. Ni upuuzi una nyumba lakini bado unalia lia kwenye biashara yako ya muziki.

Binafsi ninakerwa mno nikiona baba au mama mwenye nyumba maskini kuliko mpangaji. Tubadilishe fikra zetu.
Umeongea point muhimu sana ila kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria tulionao wengi wetu kulikopelekea hadi kuwa na maisha ya kukaririshwa utaishia kuonekana huna akili, kama baadhi ya wachangiaji humu walivyochangia.
Nyumba zimepelekea watu wengi kuwa maskini bila wao kujua.. hapa simaanishi nyumba siyo muhimu, nyumba ni ya mihimu ila kama mtoa mada alivyosema, kuwa kwanza na uchumi imara msingi imara kiuchumi mengine yatafuata wabongo wengi tunaishi kwa uoga sana.
 
Bado najiuliza,wahindi/warabu na ubilionea wao bado wanakaa NATIONAL HOUSING,bado Wana kaa maeneo karbu na mijini kwenye Kodi kubwa sana.

Najiuliza mtu anakaa/amepanga chanika ambapo kwenda na kurudi nauli karbu 10000 na daily yupo town na mtu aliyepanga town akilipa laki6 kwa mwezi wanatofauti gani?Au sisi ngozi nyeusi hesabu zetu ni za kuhesabu namba TU na si magazijuto
 
Hakuna investment nzuri kama real estate, nyumba ni investment bora ambayo inakupa vitu vingi kwa wakati mmoja. Kwanza inakupa uhakika wa sehemu ya kuishi bila kusumbuliwa kodi, inakupa uhakika wa kukupa pesa ya uhakika iwapo unafanya biashara ya kupangisha au unapofanya maboresho ya nyumba n kuziuza, pia inakupa uhakika wa kukopa na kukuza biashara zako kwa kuitumia kama collateral security.

Nilichogundua ni kua watu wanaofanya kazi rasmi wanajiona wanamaalifa sana na uhodali wa kujifanya wanaweza kumeneji na kujenga wakati wowote watakaojisikia, jamani mambo hubadilika sana na umri unapozidi kwenda opportunity zingine zinaanza kuwa mbali na wewe sasa unakuta mtu anajenga baada ya kustaafu anaona ni rahisi kisha anakwamia ktk renta, stress zinaanza upya.

Ukiangalia watu wenye kipato cha chini yani wao kipao mbele chao kikubwa huwa ni kujenga, na mafanikio yao hupimwa kwa kuwa na sehemu ya kulala, hivyo ni rahisi kukuta, mama ntilie, muuza genge, wauza mitumba wamejibana wakajenga kibanda kizuri hadi watu waliopo katika sekta rasmi wanashangaa kumbe ni nidhamu tu ya pesa. Ukitaka kujua ni muhimu kua na japo kibanda chako, mipango yote ya kawaida iharibike na usiwe tena katika nafasi ya kupata pesa kama ulivyotarajia kwa mwaka mmoja tu utajua kweli ni muhimu.

Hapa sizungumzii zile nyumba za kifahali!! hapana ni nyumba tu ya kuweza angalau kujificha usiku ukalala angalau.
 
Umeongea point muhimu sana ila kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria tulionao wengi wetu kulikopelekea hadi kuwa na maisha ya kukaririshwa utaishia kuonekana huna akili, kama baadhi ya wachangiaji humu walivyochangia.
Nyumba zimepelekea watu wengi kuwa maskini bila wao kujua.. hapa simaanishi nyumba siyo muhimu, nyumba ni ya mihimu ila kama mtoa mada alivyosema, kuwa kwanza na uchumi imara msingi imara kiuchumi mengine yatafuata wabongo wengi tunaishi kwa uoga sana.
Unajua kua thamani ya kiwanja inapanda kila siku, sasa kama ni umesikini umeletwa na nyumba basi unaweza kuuza ukaenda kujenga sehemu ambayo mji unakuja na ukapata angalau kamtaji ka kuanzia au kuendelezea biashara.
 
Kuna mama mmoja mjin yeye ukipanga kwake utajuta yan hela anapata sijui anapeleka wapi unampa hela baada ya mwezi anaanza kulilia shida umkopeshe usipompa ni vijembe na kukukasirikia uswazi hapana aisee
Poleeeeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom